Yearly Archive 2021

Je! “Mke wa ujana wako” ni yupi kibiblia?

SWALI: Je! Mke wa ujana ni yupi.. Je! siruhusiwi kumwacha Rafiki yangu wa kike (Girlfriend) au wa kiume (Boyfriend) na kwenda kuwa na mahusiano na mwenzi mwingine, kwasababu yule wa kwanza ndio mwenzi wa ujana wangu?


JIBU: Mke wa ujana kama inavyozungumziwa katika biblia sio Rafiki wa kike (GF) Bali ni mke ambaye  ulishafunga naye ndoa tangu ukiwa kijana, hadi sasa umeshakuwa mtu mzima au umeshazeeka. Huyo mke uliyenaye sasa ndio anaitwa mke wa ujana wako.Ulikuwa naye tangu enzi na enzi.

Neno hilo utakutana nalo katika vifungu hivi,

Malaki 2:14 “Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako”.

Mithali 5:18 “Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako”.

Hivyo kulingana na swali lako ni kwamba, hupaswi kumwacha mke wako ambaye ulikuwa naye tangu ujanani, ukaenda kuoa mwingine, hiyo ni dhambi kubwa sana, vilevile hupaswi kumwacha mume wako, uliyeolewa naye tangu ujanani mwako, ukaenda kuolewa na mume mwingine hiyo ni dhambi. Utakuwa unafanya dhambi ya uzinzi, haijalishi hakuvutii tena kwako kiasi gani.

Lakini hapo haizungumzii, Boyfriend au Girlfriend. Katika Imani ni kosa mtu kuishi na msichana au mvulana, au kuwa na mahusiano yoyote ya kimapenzi na mtu ambaye bado hajawa mke/ mume wake.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.

Je! Daudi hakuwa mtoto wa ndoa wa Yese? (Zab 51:5)

UFUNUO: Mlango wa 14

ITAKUFAIDIA NINI?

Fumo ni nini kama tunavyosoma katika biblia? (Hesabu 25:7)

Rudi nyumbani

Print this post

ITAKUFAIDIA NINI?

Marko 8:34  “Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.

35  Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.

36  Kwa kuwa ITAMFAIDIA MTU NINI KUUPATA ULIMWENGU WOTE, AKIPATA HASARA YA NAFSI YAKE?

37  Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake”

Kufaidia maana yake “mtu atapata faida gani, aupate ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake”.

Umepata majumba yote, fedha zote duniani ni zako, magari yote ni ya kwako, madini yote (fedha, dhahabu, almasi) ni yako, ardhi yote dunia ni yako, na kila kitu ni chako, yaani hakuna kisicho chako..Halafu umekufa umejikuta jehanamu!!…Swali tunaulizwa na aliyeacha Mbingu za mbingu akaja duniani, aliyeacha Milki, aliyeacha utajiri, na kushuka duniani kwenye mavumbi…anatuuliza swali… ITATUFAIDIA NINI KUPATA HAYO YOTE HALAFU TUMEPATA HASARA ZA NAFSI ZETU???.

Huyo huyo aliyeacha mbingu na utajiri mbinguni anasema mahali Fulani..

Marko 10:22  “Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

23  Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, JINSI ITAKAVYOKUWA SHIDA WENYE MALI KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU!

24  Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, WATOTO, JINSI ILIVYO SHIDA WENYE KUTEGEMEA MALI KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU!

25  Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu”.

Anasema.. “jinsi ilivyo shida”…sio kwamba “haiwezekani kabisa”..inawezekana lakini… “JINSI ILIVYO SHIDA !!!”.

Mpaka Bwana mwenyewe anasema “Ni shida!”.. tena anakwambia ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia kwenye ufalme wa mbinguni!!!…. Sentensi hiyo moja kwa moja, inaonyesha jambo ambalo uwezekano wake ni mdogo sana… Kwasababu mpaka leo hii bado huo muujiza haujatendeka wa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!!!…. (ngamia huyo awe ngamia mnyama, au kamba..lakini bado hatujaona!!)..

Sasa basi kama uwezekano wake ni mdogo hivyo!!!….Kwanini tunajisumbua sana kutafuta hayo mambo????.

Mithali 23:4 “USIJITAABISHE ILI KUPATA UTAJIRI; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe”.

Ni kweli, Ukimuomba sana Mungu akupe utajiri, na ukiutafuta utaupata..na atakupa nguvu za kuupata kulingana na Neno lake, lakini kumbuka pia…

UNAZIDI KUIFANYA NJIA YAKO YA KUINGIA MBINGUNI KUWA NYEMBAMBA ZAIDI. Kwasababu wewe unakuwa Ngamia, na Mlango wa Mbinguni unakuwa tundu la sindano..

Ushauri huo ametupa!!…yeye aliyetoka mbinguni, ambaye anaujua kila kitu!.. ameona si vyema atuambie tu! Ni ngumu?..bali aonyeshe na mfano wake!..Ni sisi kuchagua kujitanua kuzidi kuwa ngamia, au kujitajirisha katika mambo ya ufalme wa Mbinguni.

Na kwanini katika ule mfano alimwambia Yule kijana akauze kila kitu awape maskini kisha amfuate??…Si kwasababu Bwana Yesu alikuwa anataka kumfukarisha, bali alitaka kumtoa mungu-mali katika moyo wake na kumpa moyo wa unyenyekevu ambao utamtegemea Mungu..ambao huo pekee ndio Mungu anaweza kutembea nao..na si ule moyo wa kiburi cha mali aliokuwa nao. Na kamwe asingeweza kukosa chakula, baada ya pale, kwasababu angekuwa tu kama mmoja wa mitume wake (wakina Petro), labda angekuwa ni mtume wa 13, kwasababu wakina Petro nao, waliambiwa waache nyavu zao wamfuate Bwana. Lakini katika kumfuata kwao kote Bwana hawajawahi kufa njaa, wala kupungukiwa.

Dada/Kaka inawezekana umehubiriwa sana na kuombewa upate mali na utajiri!! … Leo mimi nakushauri ushauri , ushauri ule ule Bwana aliotupa!… “Kwa kuwa ITAMFAIDIA MTU NINI KUUPATA ULIMWENGU WOTE, AKIPATA HASARA YA NAFSI YAKE?”.

Wengi wa wanaokuhubiria kwamba “Njoo uwe tajiri” ni kwasababu wanatafuta kitu kutoka kwako!!..wanataka wapate kitu kutoka kwako, lakini hawataki Roho yako iende mbinguni, ndio maana hawatakuambia kamwe hili neno >> “JINSI ITAKAVYOKUWA SHIDA WENYE MALI KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU!”..

Itakuwa ni shida!.. Itakuwa shida!..

Bwana anasema tujikane nafsi, tunapoanza kumfuata Yesu, ni wakati wa kupunguza mizigo yetu, hata ikiwezekana mali, na si kuiongeza.. ili zisitusonge kuingia mbinguni… si wakati wa kutia jitihana kutafuta utajiri!!!.. Ni wakati wa kuupunguza..Kama  kazi yako ya Bar ndio iliyokuwa inakupa utajiri na mali! Unaiacha…Ni rushwa ndio zilikuwa zinakutajirisha unaacha…

Ulikuwa una maduka matau yaliyokuwa yanakufanya ufanye kazi masaa 24, hebu punguza bakiwa na moja tu! Litakalokufanya ufanye kazi masaa 8 au chini ya hapo, ili upate muda wa kuutafuta uso wa Mungu.. Muda wa kuishi hapa duniani haikusubirii. Itakufaidia nini upate kila kitu halafu upate hasara ya nafsi yako???..Au utatoa nini kuifidia hiyo nafsi siku ile??.

Luka 21:33  “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

34  Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo”.

Kama nitakula chakula cha aina moja kila siku, halafu nitapata muda wa kusali na kusoma neno kwa utulivu kila siku, si ni heri kuliko nile mboga saba, nikae chini ya dari zuri, halafu nakosa hata muda wa kusoma Neno na kuomba!!.. Ni heri niwe mtu wa daraja la chini kabisa lakini ni Tajiri wa Roho kuliko niwe mtu wa daraja la kwanza halafu ni ngamia katika roho, ambaye sitaweza kupenya kuingia katika ufalme wa Mungu!!.. Ni heri niwe na rafiki maskini ambaye atanifundisha na kunishurutisha kumcha Bwana, kuliko niwe na rafiki tajiri ambaye atanipeleka mbali na Mungu.

Bwana mkuu wa hekima zote atusaidie tuweze kuyatafakari mashauri yake na kuchukua uamuzi sahihi.

Kama hujampokea Yesu, kumbuka tupo mwisho wa nyakati, na Hukumu ya ulimwengu huu ni juu ya wale wote waliomkataa Yesu na maneno yake. Hivyo mgeukie leo, tubu dhambi zako kwake, na yeye atakusamehe na kukupokea na kukufundisha.

Maran atha!!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

nini maana ya kujikana nafsi na kujitwika msalaba?

USIOMBE MAOMBI YASIYOKUWA NA MAJIBU NA WALA USIMTUKANE MUNGU.

Jiepushe na tamaa ya Mali/kupenda fedha.

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.

IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.

Rudi nyumbani

Print this post

BADO UPO YERUSALEMU TU..GALILAYA HUTAKI KENDA?

Wakati ule Bwana Yesu anafufuka, utaona, lipo kundi la watu alilitokea akiwa kule kule Yerusalemu, lakini lipo kundi lingine alilipa masharti ni wapi atakapokutana nalo.

Kwa mfano Yesu wale watu wawili waliokuwa wanakwenda kwenye Kijiji kimoja kilichoitwa Emau, karibu na Yerusalemu, Kristo aliwatokea huko huko (Luka 24:13-33). utaona pia aliwatokea wale wanawake waliokwenda Kaburini siku ile ya kwanza ya juma alipofufuka, akazungumza nao, kisha akaondoka.

Lakini hakuwatokea mitume wake 11 hata mmoja akiwa huko Yerusalemu, badala yake, aliwaagiza wale wanawake, kuwa wakawaambie, Bwana  amesema atawatangulia kwenda Galilaya ndipo watakapomuona.

Mathayo 28:9 “Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.

10 Kisha Yesu akawaambia, Msiogope; enendeni, mkawaambie NDUGU ZANGU waende Galilaya, ndiko watakakoniona”.

Unaweza kujiuliza ni kwanini awape masharti ya mahali pa kukutana nao, Kumbuka pia hata kabla ya Yesu kufa, aliwaambia pia wanafunzi wake maneno hayo hayo, utasoma hilo katika

Marko 14:27 “Yesu akawaambia, Mtakunguwazwa ninyi nyote kwa ajili yangu usiku huu; kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo watatawanyika.

28 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya”.

Kwahiyo hilo halikuwa agizo la kila mtu bali lilikuwa mahususi kwa baadhi ya watu wale  ambao aliwaita “NDUGU ZAKE”,tofauti na wale wengine, Na ukisoma pale vizuri utagundua kuwa haikuwa mahali popote tu kule Galilaya, hapana bali Bwana Yesu aliwapa na eneo husika kabisa watakalomwonea, nalo lilikuwa katika ule mlima aliowaelekeza.

Ndipo ukisoma pale utaona baada ya Bwana Yesu kufufuka wakafunga safari kweli, kutoka Yerusalemu, mpaka Galilaya, umbali wa kama KM 120, hivi, , wakaenda moja kwa moja mpaka kwenye huo mlima aliowaagiza, ndipo wakakutana naye uso kwa uso na kuwapa maagizo;

Mathayo 28:16 “Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu.

17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.

18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”.

Sasa unaweza ukajiuliza ni kwanini, ajidhihirishe kwao akiwa Galilaya na sio kule Yerusalemu ,kama alivyofanya kwa wale wengine? Kulikuwa na sababu gani ya yeye kuwachosha wasafiri umbali wote ule mrefu mpaka Galilaya wakati angeweza tu kuwatokea palepale Yerusalemu na kuwapa maagizo?

Jibu ni kuwa Bwana alikuwa anataka mawazo yao kwa wakati ule yaelekee kule.

Utakumbuka kuwa Galilaya ndio mji Yesu alikolelewa, mpaka anaanza huduma, yaani kwa ufupi ni kuwa sehemu kubwa ya Huduma yake aliifanya akiwa Galilaya, hata mitume wake wote aliwaitia huko, ishara nyingi na miujiza yake mingi aliifanya Galilaya, ni sehemu ndogo sana ya huduma yake aliifanya akiwa Yerusalemu.

Hivyo Kristo kuwaambia  mitume wake ninawatangulia Galilaya ni kuwaonyesha kuwa Moyo wake, baada ya kufufuka kwake haukuwa tena Yerusalemu kwa mitume wake.. Hakutaka wamwone kwa jicho ya Yerusalemu, kama wale wengine bali kwa jicho la Galilaya, kule alipotumikia muda wake wote akiifanya kazi ya Mungu.

Huko ndipo alipowaambia enendeni ulimwenguni kote mkawafanya mataifa kuwa wanafunzi, kama mimi nilivyokuwa ninawafanya huku Galilaya, nami nitakuwa pamoja nanyi mpaka ukamilifu wa dahari.

Nini Kristo alitaka tufahamu katika habari hiyo.?

Ni kuwa hata sasa, ikiwa wewe ni mwanafunzi wa Yesu, au unataka uwe mwanafunzi wa Yesu kweli, basi fahamu  kuwa hutamwona Kristo Yerusalemu, aliposulibiwa, hutamwona Kristo katika mafundisho ya msalaba tu kila siku, mafundisho ya kuamini, au ya vitubio, yaani kama  wewe miaka nenda rudi, hujui kingine Yesu anachokitaka kwetu  zaidi ya kutubu na kuokoka, basi, wewe bado upo Yerusalemu.

Kristo anataka uitazame na kazi yake pia, anataka uone alivyofanya yeye akiwa duniani na wewe ukafanye vivyo hivyo, anataka uone kuwa kuna watu wanahitaji kuhubiriwa Injili, kuna watu wanahitaji kupata wokovu, kufunguliwa, kuwekwa huru kutoka katika dhambi na vifungo mbalimbali, hicho ndicho Kristo anataka uone kwa wakati wa sasa. Hiyo ndio Galilaya yako unapopaswa uende ukakutane na Yesu.

Lakini kama wewe ni wa kusikia tu injili, na kusema AMEN,  au kusema mimi nimeokoka, basi, huna cha Ziada, ujue kuwa wewe si “NDUGU” yake Kristo, Wewe si  “MWANAFUNZI WAKE”. Huwezi kumfurahisisha kwa lolote.

Nyakati hizi tunazoishi ni nyakati ambazo, zilitabiriwa kuwa kutakuwa na njaa mbaya sana, sio ile njaa ya kukosa chakula, bali ni ile ya kukosa kuyasikia maneno ya Mungu, Nabii Amosi alionyeshwa hilo

Amosi 8:11 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana”.

Jiulize kwa upande wako, tangu Kristo amefufuka ndani yako, ni kazi gani ya ziada umeifanya kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Bado upo Yerusalemu tu, Galilaya hutaki kwenda..Upo buzy na kazi zako, upo buzy na shughuli za kidunia, upo buzy na familia yako, Galilaya kwako ni mbali sana, kule hakuna pesa, hakuna kujulikana, utaonekana mshamba, utadharauliwa, utachekwa,

Ndugu jitathmini ukristo wako ikiwa hata unaona ugumu kuichangia kazi ya injili, unategemea vipi utaweza kuwahubiria wengine habari za ufalme wa mbinguni, hata hicho kitakushinda tu, Na taji lako litakuwa hafifu, au usipokee kabisa taji huko unapokwenda!

Tuamke sote, tuanze kuwagawia na wengine kile Bwana alichotugawia  sisi, katika kipindi hiki cha njaa cha siku za mwisho.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

RABI, UNAKAA WAPI?

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

KURUDI ISRAELI KWASASA NI KUGUMU, SIO KAMA KULE MWANZONI.

Bahari mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye biblia.

OLE WAKO KORAZINI NA BETHSAIDA.

Rudi nyumbani

Print this post

Hiana ni nini?

Neno “hiana” maana yake ni “usaliti” ule wa mapenzi. Endapo mtu mmoja akimwacha mke wake/mume wake na kwenda kufanya uzinzi , mtu huyo amefanya mambo ya hiana kwa mwenzake. Na Bwana anauchukia usaliti.

Malaki 2:14 “Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, ULIYEMTENDA MAMBO YA HIANA, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.

 15 Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake MAMBO YA HIANA.

  16 Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; BASI JIHADHARINI ROHO ZENU, MSIJE MKATENDA KWA HIANA”.

Lakini mbali na hilo, Watu wote waliokoka mbele za Kristo tunahesabika katika roho kama BIBI ARUSI.. na Kristo ndiye Bwana wetu (2Wakorintho 11:2).

Maana yake tunapoacha kufanya maagizo yake, kama  utakatifu, kuwa na upendo, kuwa watu wa msamaha, wasiolipiza visasi, wasio wazinzi, wezi, walevi, watukanaji, waabudu sanamu  n.k katika roho ni tumemsaliti (Yaani tumefanya mambo ya HIANA). Maana yake tunamtia wivu. Na siku zote kumbuka, Mungu aliposema yeye ni mwenye wivu, hakumaanisha wivu huu wa kawaida, labda mtu anapoona mwenzake kapata kitu Fulani ambacho yeye hanapa! Hakumaanisha huo..kwasababu ni heri ungekuwa huo!… bali wivu alioumaanisha ni a ule wivu wa mtu anapochukuliwa mke wake kipenzi!..Wivu ambao ni mbaya sana, ambao kwetu sisi wanadamu wengi unaishia aidha upande mmoja ufe, au pande zote zife!!..Ndio hapo utasikia aidha mtu kajinyonga..au kaua na yeye mwenyewe kajimaliza!..

Mithali 27:4 “Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu”

Hiyo ndio maana Bwana Mungu alisema katika…

Kutoka 20: 4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; KWA KUWA MIMI, BWANA, MUNGU WAKO, NI MUNGU MWENYE WIVU; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

Wakati Fulani Yuda, na Israeli walimwacha Bwana, na kufanya mambo maovu yasiyofaa ikiwemo kwenda kuabudu miungu mingine, na  Bwana akasema maneno haya juu yao…

Yeremia 3:6 “Tena, Bwana akaniambia siku za mfalme Yosia, Je! Umeyaona aliyotenda Israeli mwenye kuasi? Amepanda juu ya kila mlima mrefu, akafanya huko mambo ya ukahaba, tena, chini ya kila mti wenye majani mabichi.

7 Nami nalisema baada ya yeye kuyatenda hayo yote, Atanirudia mimi, lakini hakurudi; na dada yake, Yuda MWENYE HIANA, akayaona hayo.

8 Nami nikaona, wakati nilipokuwa nimemwacha Israeli mwenye kuasi, nikampa hati ya talaka kwa sababu hiyo ya kuzini, dada yake, Yuda mwenye hiana, hakufanya hofu; bali yeye naye akaenda akafanya MAMBO YA UKAHABA.

9 Hata ikawa, kwa sababu alikuwa mwepesi wa kufanya ukahaba, nchi ikatiwa unajisi, naye akazini na mawe na miti.

10 Na pamoja na hayo yote dada yake, Yuda mwenye hiana, hajanirudia mimi kwa moyo wake wote, bali kwa unafiki, asema Bwana.

 11 Bwana, akaniambia, Israeli mwenye kuasi amejionyesha kuwa mwenye haki kuliko Yuda mwenye hiana.

 12 Enenda, ukatangaze maneno haya kuelekea upande wa kaskazini, ukaseme, Rudi, Ee Israeli mwenye kuasi, asema Bwana; sitakutazama kwa hasira; maana mimi ni mwenye rehema, asema Bwana, sitashika hasira hata milele.

13 Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi Bwana, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti yangu, asema Bwana.

14 Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema Bwana; MAANA MIMI NI MUME WENU; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni”.

Je na wewe leo unafanya mambo ya Hiana kwa kuvaa mavazi yasiyofaa??, unavaa suruali, unapaka wanja, unapaka lipstick, unavaa hereni na kuweka wigi kichwani?..je unafanya mambo hayo ya hiana mbele za Mungu wako kwa kulewa na kufanya uasherati na anasa, je unafanya mambo ya hiana kwa kutazama picha za ngono mitandaoni, na kujichua?.. je umefanya mpira kuwa ndio Mungu wako na kuwa mshabiki wa mambo hayo?…Fahamu kuwa kwa matendo yako unamtia Mungu wivu. Na kuzivuta hasira za Mungu karibu nawe. Kumbuka mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu. Hivyo huwezi kuufanya kama unavyotaka wewe, na pia kumbuka tulinunuliwa kwa thamani kubwa, hivyo hatuwezi kuishi tu kama tunavyotaka sisi.

Soma mistari hii uone ni jinsi gani, mambo ya Hiana yanavyomchukiza Mungu wetu >>Yeremia 9:2, Yeremia 5:11, Hosea 6:7, 1Samweli 14:33.

Rudi leo! Kwa Bwana na kutubu!..choma hizo nguo zisizo za kiMungu unazozivaa, wala usimpe mtu!. Na mwombe Bwana akupe badiliko la kweli maishani mwako. Vunja hizo chupa za bia, na vikao vya ulevi na anasa, achana na huyo mvulana/au msichana mnayefanya uasherati sasa, achana na huyo mke/mume wa mtu unayeishi naye, au kutembea naye. Futa hiyo miziki yote ya kidunia katika simu yako. Ukifanya hivyo hiyo ndio TOBA!.. Kisha Bwana mwenyewe atakuongezea nguvu ya kuweza kushinda dhambi!..Lakini usipofanya hayo kwa vitendo, hakuna nguvu yoyote itakayoshuka juu yako.

Na pia kumbuka tunaishi katika siku za mwisho na Bwana Yesu alisema itatufaidia nini tukiupata ulimwengu mzima halafu tupate hasara za nafsi zetu. Hivyo tafakari hilo siku zote, na ujue kuwa vitu vya ulimwengu huu havina umuhimu sana kama vinavyotukuzwa na watu.. Bwana Yesu anarudi.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

NI KWA NAMNA GANI ROHO HUTUTAMANI KIASI CHA KUONA WIVU?

Maashera na Maashtorethi ni nini?

Nini maana ya “Mwenye hekima huvuta roho za watu”.

IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.

Rudi nyumbani

Print this post

Fumo ni nini kama tunavyosoma katika biblia? (Hesabu 25:7)

Fumo ni mkuki, lakini katika biblia Neno mkuki linatumika kwa namna mbili, upo mkuki wa kuchomea, na pia upo mkuki wa kurusha.

Ule mkuki wa kuchomea ndio unaoitwa Fumo, ambao askari wanaubeba, na kuchoma maadui zao pale wanapowakaribia,  na kwa kawaida unakuwa ni mizito kidogo na mrefu na wenye ncha kali. Lakini ule mwingine wa kurusha wenyewe kibiblia unajulikana kama mkuki tu hivyo hivyo, isipokuwa wenyewe ni mwepesi kidogo na umetengenezwa hivyo ili utakaporushwa uweze kufika mbali zaidi adui alipo. Zote hizi ni silaha za kivita.

Hivyo unaweza kukutana na haya maneno mawili kwenye biblia yakakuchanganya.. kwa mfano baadhi ya vifungu vinayatajwa maneno yote mawili ni kama vifuatavyo.

1Samweli 17:45 “Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana”.

Ayubu 41:26 “Mtu akimpiga kwa upanga, haumwingii; Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha”.

Vifungu vingine ambavyo utakutana na hili neno “Fumo” Ni kama vifuatavyo;

Hesabu 25:7 “Naye Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona jambo hilo, akaondoka hapo katikati ya mkutano, akashika fumo mkononi mwake;

8 akamwandama huyo mtu wa Israeli na kuingia ndani ya hema nyuma yake, naye akawachoma wote wawili kwa fumo lake, yule mume wa Israeli na huyo mwanamke kati ya tumbo lake. Basi pigo likazuiwa kwao wana wa Israeli”.

1Samweli 17:7 “Na mti wa fumo lake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia”.

1Samweli 26:12 “Basi Daudi akalitwaa lile fumo, na lile gudulia la maji, kichwani pa Sauli; nao wakaenda zao, wala hapana mtu aliyeliona jambo hili wala kulijua, wala kuamka; maana wote walikuwa wamelala; kwa kuwa usingizi mzito kutoka kwa Bwana umewaangukia”.

Soma pia 2Samweli 1:6, Ayubu 39:23,

Halikadhalika na sisi  kama wakristo rohoni ni lazima tuwe na FUMO zetu na MIKUKI yetu mikononi mwetu, ili tuitwe askari kamili wa  Kristo, hizo ndio zile silaha za mkono wa kuume zinazozungumziwa katika 2Wakorintho 6:7… Kwa hizo, ndivyo tutakavyoweza kumpiga shetani, tukizikosa, tujue kuwa shetani hatoweza kutuogopa, na silaha yenyewe ni ufahamu wa kuyatambua mamlaka tuliyopewa katika jina la YESU na DAMU yake. Na kuyatumia..

Yeye mwenyewe alisema..

Luka 10:19 “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”.

Kila mmoja wetu ambaye anasema ameokoka anapaswa ajue kuwa mamlaka hayo amepewa, Hivyo simama kama shujaa, hubiri, haribu kazi za shetani, wafungue watu, mwaribu shetani na kazi zake zote katika maombi. Kwasababu Fumo zetu na mikuki yetu ipo  mikononi mwetu.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)

Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?.

Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)

NYAYO TUNAZOPASWA KUZIFUATA.

Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?.

Rudi nyumbani

Print this post

Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?.

Jibu: Kipo kifaa kinachoitwa Birika tulichozoea kukijua, ambacho kinatumika kuhifadhia chai au maji. Lakini pia neno hilo hilo birika lina maana ya “Bwawa” au “Dimbwi dogo”, lilolotengenezwa kwa kazi Fulani mahususi, Na Bwawa hilo linaweza kuwa limetengenezwa kwa utaalamu mkubwa au pasipo utaalamu mkubwa, kufuatia matumizi ya bwawa hilo.

Sasa katika biblia yalikuwepo mabirika mengi, yalikuwepo yaliyotengenezwa kwa kunyweshea wanyama maji mfano hayo ni lile la Yakobo..

Mwanzo 30:38 “Akazisimamisha fito hizo alizozibambua katika mabirika ya kunyweshea maji, pale walipokuja wanyama wanywe; wakachukua mimba walipokuja kunywa.”

Unaweza pia kusoma mfano wa hayo katika 2Nyakati 26:10.

Na pia yalikuwepo mabirika yaliyochimbwa ardhini kwa ajili ya kuhifadhia maji, mfano wa hayo, ni lile Yusufu alilotupwa na ndugu zake..

Mwanzo 37:23 “Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa,

24 wakamtwaa wakamtupa katika birika; na hiyo birika ilikuwa tupu, hamna maji”.

Unaweza kusoma pia 1Samweli 13:6..

Na pia yalikuwepo mabirika  yaliyotengenezwa kwaajili ya kuogea/kunawia. Mfano wa hayo ni yale yaliyotengenezwa katika hema ya Mungu na katika nyumba ya Mungu, maalumu kwa makuhani kujisafisha kabla ya kuingia ndani ya hema, au nyumba ya Mungu kufanya kazi za kikuhani..

Kutoka 30:17 “Bwana akanena na Musa, na kumwambia

18 Fanya na BIRIKA LA SHABA, na tako lake la shaba, ILI KUOGEA; nawe utaliweka kati ya hema ya kukutania na madhabahu, nawe utalitia maji.

19 Na Haruni na wanawe wataosha mikono yao na miguu yao humo;

 20 hapo waingiapo ndani ya hema ya kukutania; watajiosha majini, ili wasife; au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike, kumteketezea Bwana sadaka ya moto”

Pia unaweza kusoma juu ya birika hizo katika nyumba ya Mungu katika 1Wafalme 7:38-43 na 2Nyakati 4:6.

Pia yalikuwepo mabirika yaliyotengenezwa kwaajili ya kuogea makahaba..

1Wafalme 22:37 “Hivyo akafa mfalme, akachukuliwa Samaria, wakamzika mfalme huko Samaria.

38 Wakaliosha gari penye BIRIKA LA SAMARIA, na mbwa wakaramba damu yake; (BASI NDIPO WALIPOOGA MAKAHABA); sawasawa na neno la Bwana alilolinena”.

Lakini pia tunasoma katika agano jipya, yakitajwa tena aina nyingine ya mabirika. Na hayo si mengine zaidi ya birika la Siloamu (Yohana 9:7) na Birika la Bethzatha (Yohana 5:2).

Birika ya Bethzatha ilijengwa kwa lengo la kuhifadhi maji yatakayotumika hekaluni. Birika hii ilijengwa kwa kuzungushiwa “Matao matano”. Matao ni nguzo zilizosimamishwa kuzunguka birika hilo, na kulitia uvuli…na nafasi iliyokuwepo kati ya nguzo na nguzo ilikuwa ndio maingilio ya birika hiyo..

Yohana 5:2 “Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano .

3  Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke ”.

Kama tunavyoijua habari, Yule mngonjwa ambaye aliugua kwa miaka 38, na  hakuwa na mtu wa kumwingiza birikani, pindi maji yanapochemka (yaani nguvu za Mungu zinaposhuka ndani ya yale maji), lakini alipokutana na Bwana Yesu, aliponywa siku ile ile pasipo kuingizwa birikani.

Hiyo ni kutufundisha kuwa hakuna matumaini kwenye maji  ya upako, wala visima vya upako. Huyu aliugua miaka 38, na alikuwa anatumainia maji ya upako. Na kama sio Bwana Yesu kumhurumia pengine angekufa bila kupata msaada wowote.

Kristo mponyaji wa mwili na roho yupo, isipokuwa sisi tumemtupa nje, na badala yake tunatafuta miujiza kwa njia zisizo rasmi.

Hebu jifunze kwenye huo mfano… “Hapo inasema ndani ya hayo matao, JAMII KUBWA ya wagonjwa walikuwa wamelala, wakisubiri maji yachemke.”…wamelala!!  wakisubiri!!..na matokeo ya kusubiri ndio hiyo miaka 38 bila matumaini!…Na wakati wakiwa wanasubiri kumbe mponyaji yupo ulimwenguni akitembea huko na huko akiponya na kufungua watu.. lakini hili kundi lingine kubwa huku limelala likisubiri!! Huku likijitumainisha na maji ya upako!…na kisima cha upako!!.

Na si ajabu huyu Bwana peke yake ndio angalau alikuwa na moyo wa kupokea kitu kipya, ndio maana Bwana akamfuata yeye peke yake.. lakini hao wengine wengi waliokuwa wanasubiria, tunaona Bwana hakuwafuata kuwaponya.. kwanini??.. Ni dhahiri kuwa wengi wao walishamsikia huko nje akifundisha na kuponya lakini kwasababu wanaamini zaidi katika maji yale ya upako, wakamdharau, pengine wamesikia Yesu akikuponya anakwambia acha dhambi, acha kisasi, kuwa mtu wa kusamehe, na ili hali wenyewe hawataki kuacha hayo.. Wenyewe wanataka wakishapona waendelee na maisha yao, wasipewe pewe maelekezo ya maisha, ndio maana wakalipenda zaidi lile birika kwasababu ukishaponywa huambiwi chochote…hata kama ulikuwa kahaba na muuaji, ukishaponywa unaweza kuendelea na ukahaba wako.

Ndugu, jihadhari na miujiza BUBU, ambayo unaambiwa njoo ogea maji haya, upone… lakini hugusiwi habari ya dhambi zilizokufunga!.. Unaambiwa njoo ugea maji haya, lakini huambiwi huyo mke/mume unayeishi naye si wako!..huambiwi kwamba unaishi katika uzinzi na ukifa unaenda jehanamu!!.. Na ndio maana unahangaika miaka na miaka kununua maji haya na yale, mafuta haya na yale, kuzunguka katika kisima hiki na kile, kutafuta uponyaji lakini hupati!!..Ni kwanini?.. Ni kwasababu umemtupa Kristo na maneno yake nje!, halafu unatafuta uponyaji kwa njia mbadala..

Ndugu achana na hivyo visima bubu, Kristo kashavilaani!!…achana na hayo mabirika na madimbwi hayana msaada kwa nyakati hizi!!!…haijalishi yanalitaja jina la Mungu kiasi gani!..hili birika la Bethzatha lilikuwepo karibu sana na Hekalu la Mungu, lakini Kristo hakulitukuza!!!….Na wewe ndio maana pengine umekaa muda mrefu, ukitumainia hivyo visima na hakuna chochote!!.. Achana navyo, mtafute yeye..atakuponya na kukupa Maelekezo bora ya maisha ambayo yataiokoa roho yako, na hata kukuponya….

Na pia kama hujampokea Yesu, saa ya wokovu ni sasa, mwamini leo, na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji tele na kwa Jina la Yesu. Na utakuwa umemfungulia Roho Mtakatifu njia ya kukuongoza katika kweli yote ya maandiko. Bwana Yesu yupo karibu na hicho kisima akitafuta tafuta ni nani aliye tayari kusikia, na kumkubali.. Uwe wewe leo! Katika Jina la Yesu.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

BIRIKA LA SILOAMU.

Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)

Neno Bildi linamaanisha nini kwenye biblia(Matendo 27:28) ?

nini maana ya kujikana nafsi na kujitwika msalaba?

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

Rudi nyumbani

Print this post

Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika..

SWALI: Nini maana ya hili neno,

Mathayo 21:44 “Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.

45 Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao”.


JIBU: Shalom.

Maneno hayo aliyasema Bwana Yesu kuonyesha tabia ya jiwe hilo analolizungumzia.

Hapo anaposema mtu atakayeanguka juu yake atavunjika-vunjika, ni kuonyesha kuwa jiwe hilo ni “Gumu sana”, na sio laini, useme  labda ni la udongo au kitu kingine, hapana ni ligumu kiasi kwamba ukilidondokea tu ni lazima uvunjike hakuna namna.

Vilevile aliposema, na yeyote atakayeangukiwa nalo,litamsaga tikitiki, ni kuonyesha kuwa jiwe hilo ni “zito sana” na kubwa.. kama lingekuwa ni jiwe dogo tu, na jepesi, lisingeweza kumsaga saga mtu pale linapomwangukia. Lakini mpaka linamponda ponda ni kuonyesha kuwa jiwe hilo ni zito sana.

Hivyo hapo ni Bwana alikuwa anaonyesha UGUMU, na UZITO wa jiwe hilo. Na jiwe lenyewe ni yeye mwenyewe.

Lakini badala watu wajenge juu ya jiwe hilo, wawe salama, kinyume chake Wapo watu wanaangukia juu ya jiwe hilo na wengine wanaangukiwa nalo.

Ikiwa wewe ni adui wa injili ya Kristo, unashindana na kazi za Mungu kutwa kuchwa, kazi yako ni kuididimiza kazi ya Mungu isisonge mbele, unafanya uchawi, unaloga, unapiga vita watu wa Mungu au unawavuta watu wasimjue Mungu kama alivyokuwa yule Elima mchawi aliyekutana na Paulo kule Pafo.. Ujue kuwa unahatarisha Maisha yako kwasababu ndivyo unavyoliangukia jiwe hili, na matokeo yake ni kuwa utavunjika vunjika, usiwe na faida yoyote hapa duniani.

Vilevile wapo watu muda wote, ni kuyaasi maagizo ya Kristo kwa makusudi, japokuwa wanaufahamu ukweli, hawa wapo kanisani, utawaona wanazini kwa makusudi na utakuta ni wachungaji au washirika wakongwe, wanafanya dhambi zao kwa siri, japokuwa kwa nje wanaonekana ni wema.. Sasa watu kama hawa, Upo wakati hili jiwe litawaangukia, na likishawaangukia hapo hakuna kupona tena, unasagika tikitiki. Wakati ambapo ghadhabu ya Mungu juu yako imefikia kilele, huwa hakuna kupona tena.

Na ndio maana Bwana Yesu aliyasema maneno hayo, kufuatana na habari aliyokuwa anaizungumzia juu kidogo, ya wale wakuu wa makuhani na mafarisayo ambao kazi yao ilikuwa ni kumvizia wamuue, ndipo akawapa mfano huo, Na kweli jitihada zao ziliishia kuangamizwa na Warumi mwaka 70 WK, ili kutimizwa ule unabii wa Yesu kuwa watazungukwa na maadui zao, watauliwa nao hawataachiwa jiwe juu ya jiwe. Mpaka leo tunavyozungumza wayahudi hawana mwelekeo wowote wa kiimani, kutokana na ile tabia yao ya kushindana na jiwe hilo.

Na jiwe hili ndilo litakalokuja kuangusha falme zote za duniani,

Danieli 2:34 “Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.

35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.

36 Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme”.

Nasi pia sisi tunapaswa tuwe makini sana na hii neema ya Yesu Kristo, badala ya kuliangukia jiwe hilo, au kuangukiwa nalo ni heri tujenge juu yake. Kwasababu yeye ndio mwamba salama. Tukijenga Maisha yetu kwa Kristo, basi tutayafurahia Maisha, ya hapa na kule ng’ambo tutakapovuka.

Je! Yesu yupo moyoni mwako? Kama hayupo ni heri ukamgeukia hivi sasa akufanye kuwa kiumbe kipya, na kukupa tumaini jipya la uzima wa milele. Acha kutanga tanga na hii dunia hizi ni siku za mwisho.

Bwana awabariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

MWAMBA WETU.

NITAFANYA YERUSALEMU KUWA JIWE LA KUWALEMEA .

Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari?”

UFUNUO: Mlango wa 14

Je! Kuna malaika wangapi mbinguni?

Rudi nyumbani

Print this post

MMESIKIA KWAMBA IMENENWA?

Zipo sheria zilizotoka kwa Mungu, na pia zipo sheria zilizotengenezwa na wanadamu lakini Mungu akaziruhusu zitumike kwa watu wake. Kwamfano katika biblia tunasoma kuwa wana wa Israeli waliruhusiwa kutoa talaka kwa wake zao, pia waliruhusiwa kuua (endapo mwanamke/mwanaume atakamatwa katika uzinzi, ilikuwa sharti auawe, kumbukumbu 22:22), Na pia wana wa Israeli, waliruhusiwa walipize kisasi kwa watu waovu, ikiwemo, jino kwa jino, uzima kwa uzima n.k.. Maana yake ni kwamba mtu akmpiga mwenzake mpaka kamng’oka jino, sharti na yeye jino lake ling’olewe, kama kamkata mtu mguu na yeye mguu wake utakatwa, kama kaua na yeye atauawa pia n.k (soma Kumbukumbu 16:21).

Sasa sheria hizi zilikuwepo katika Torati, lakini si Mungu aliyeziagiza.. Mungu tangu awali hakuagiza mtu kumwacha Mke wake au mume wake na kwenda kuoa/kuolewa na mwingine (Mwanzo 2:24), hali kadhalika, hakuaziga mtu kuua!..(Tutakuja kuliona hilo vizuri mbeleni katika somo hili, wakati Bwana Yesu analiweka hilo sawa).

Hivyo hizi sheria zilitungwa na watu wa Kale, kufuatia taratibu zao, kwaufupi zilikuwa ni desturi karibia za dunia nzima, kipindi hata wana wa Israeli wakiwa Misri, sheria hizi walizitumia huko Misri pia, sheria za kuoa na kuachana!, sheria za kulipiza kisasi, (jino kwa jino, jicho kwa jicho n.k)..hivyo walipotolewa huko Misri na kuletwa katika nchi ya Ahadi, bado mioyo yao ilikuwa imeshikamana na hizo sheria na walikuwa hawapo tayari kuachana nazo..MIOYO YAO ILIKUWA MIZITO!! (Migumu). Kwahiyo kutokana na ugumu wa mioyo yao hiyo, kutokuwa tayari kuziacha hizo sheria, ndipo Mungu akaziruhusu waendelee nazo kwa kitambo mpaka Nyakati mpya zitakapofika za Matengenezo (Yaani kipindi cha Bwana na mwokozi wetu Yesu). Ndio maana Bwana Yesu alipokuja akaanza kwa kusema…

Mathayo 19:3 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?

4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,

5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

7 WAKAMWAMBIA, JINSI GANI BASI MUSA ALIAMURU KUMPA HATI YA TALAKA, NA KUMWACHA?

8 AKAWAAMBIA, MUSA, KWA SABABU YA UGUMU WA MIOYO YENU, ALIWAPA RUHUSA KUWAACHA WAKE ZENU; LAKINI TANGU MWANZO HAIKUWA HIVI.

9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini”.

Hapo katika mstari wa 8, Bwana Yesu anasema.. “Kwasababu ya ugumu wa mioyo yao Musa aliwapa Ruhusa ya kuwaacha wake zao”..

Sasa hapo kuna jambo moja muhimu la kuzingatia.

  • Ni Musa ndiye aliyewapa ruhusa.

Kama tulivyozungumza awali, tayari Wana wa Israeli walikuwa na sheria zao kichwani za kuwaongoza, ambazo walitokanazo huko Misri, hawakuwa tayari eti kuishi na wake zao milele, hata kama wamekosea adabu (walichojua ni kwamba mwanamke akikukosea adabu, unamweka kando na kuchukua mwingine).. Na pia mtu hawezi kupewa ruhusa, kama alikuwa hatafuti hiyo ruhusa.. Hapo biblia inasema.. “Musa aliwapa ruhusa”.. Maana yake tayari hicho kitu cha kuachana kilikuwa kwenye vichwa vyao, na walikuwa wanakishinikiza, na pia hawakuwa tayari kusikia mashauri yoyote kinyume na hayo. Hivyo Mungu akamwambia Musa awaruhusu waendelee na sheria yao hiyo, na Musa akawaruhusu, lakini haikuwa mpango kamili wa Mungu.(Warumi 1:28)

Kama tu ule wakati walipong’ang’ania kutaka mfalme, jambo ambalo Mungu hakuwaagiza, wala halikuwa mapenzi ya Mungu.. lakini waling’ang’ania hivyo hivyo na Mungu akaruhusu wajipatie mfalme (1Samweli 8:7), jambo ambalo halikumpendeza Mungu kabisa. Na ndio hivyo hivyo  baadhi ya hizi sheria, zilikuja kutokana na ugumu wa mioyo yao kukataa kusikiliza mashauri bora ya Mungu, wakaruhusiwa kuendelea kuishi kwa sheria zao hizo zisizofaa…

Ndio maana agano la kale, halikuwa agano lililo kamili, mpaka Bwana Yesu alipokuja kulikamilisha..na kusema.. “mmesikia imenenwa”….”mmesikia imenenwa”…. “lakini mimi nawaambia”….. Na sehemu nyingine anasema… “Kwasababu ya ugumu wa mioyo yao, Musa aliwaruhusu kufanya hayo, lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo”.

Ndugu sio mpango wa Mungu kulaani watu, sio maagizo wala mpango wa Mungu kuoa wanawake wengi, sio maagizo ya Mungu kumlaani adui yako..utauliza hiyo ipo wapi kwenye biblia…

Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; 44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki”.

Vile vile Sio maagizo ya Mungu sisi kulipiza visasi,hata kama tumefanyiwa jambo baya kiasi gani, katika ukristo hatuna jino kwa jino wala jicho kwa jicho, Sisi tunaushinda ubaya kwa wema na si ubaya kwa ubaya.

Warumi 12:20 “Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.

21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema”.

Jukumu tulilo nalo ni kuomba Bwana atuepushe na madhara yao, na kuwaombea waokolewe.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

JE YESU AMEJIAMINISHA KWAKO?

Je watu ambao hawajasikia kabisa injili watahukumiwa?

 Nini maana ya “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati”

Alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru

UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.

NJIA YA MSALABA

Rudi nyumbani

Print this post

Ni muda gani Bwana Yesu alisulibiwa. Je! Ni saa 3 au saa 6?

SWALI: Ni muda gani Bwana Yesu alisulibiwa. Je! Ni saa 3 asubuhi kama tunavyosoma kwenye Marko, au saa 6 mchana kama tunavyosoma katika Yohana.


JIBU: Tusome vifungu vyenyewe.

Marko 15:24 “Wakamsulibisha, wakagawa mavazi yake, wakayapigia kura kila mtu atwae nini.

25 Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha”.

Yohana 19:14 “Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu!

15 Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari”.

Shalom.

Sababu ya utofauti wao ni kuwa uandishi wa Marko ulitumia mfumo wa saa za kiyahudi, wakati uandishi wa Yohana ulitumia mfumo wa saa za Kirumi.

Mfumo wa kiyahudi, kwa kawaida siku mpya huwa zinaanzia saa 12 asubuhi, Ndio maana kuna mahali Bwana Yesu alisema “Je! Saa za mchana si kumi na mbili? (Yohana 11:9)”

Inapoanza saa 1 ndio saa ya kwanza, inapofika saa mbili ndio saa ya pili, vivyo hivyo na saa ya  tatu na kuendelea. Hivyo katika Marko, inatuambia Bwana Yesu alisulibiwa taa tatu asubuhi. Na ndio maana katika Marko tunaona Bwana Yesu alisulibiwa saa 3 asubuhi.

Lakini sasa tukirudi kwenye mfumo wa muda wa kirumi ambao, Yohana aliutumia, anatuambia muda wa saa 6 wayahudi ndio walimleta kwa Pilato, ni rahisi kudhani maandiko yanajipinga lakini hapana, kwa mfumo wa muda wa kirumi, saa moja ilikuwa inaanza saa 6 usiku. Kama ilivyo sasa.

Hivyo Walipomkamata na kumpeleka kwa Pilato, ni kwamba saa 6 zilikuwa zimeshapita tangu siku ilipoanza, ambayo ni sawa na saa 12 asubuhi. Hivyo shamra shamra zote, mpaka kumpiga mijeledi na kumtwika msalaba wake na kumpeleka Goligotha, ilikuwa imeshafika saa 3 asubuhi, ndipo akasulibiwa. Sawa sawa na maandiko ya Marko.

Kwa hiyo kwa kuhitimisha ni kuwa, Bwana wetu Yesu Kristo alisulibiwa saa 3 asubuhi,akafa saa 9 alasiri, na katika huo muda kuanza saa 6 mchana mpaka saa 9 alasiri ndio kulikuwa na  lile giza, kisha akakata roho. Lakini Bwana Yesu hakusulibiwa saa 6 mchana.

Luka 23:44 “Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda,

45 jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.

46 Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.

47 Alipokwisha kusema hayo alikata roho. Yule akida alipoona yaliyotukia, alimtukuza Mungu, akisema, Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki”.

Bwana akubariki.

Je! Umeokoka? Je! Una habari kuwa tunaishi katika kizazi ambacho kinaweza kushuhudia tukio la kurudi kwa pili kwa Bwana Yesu Kristo, duniani? Kama bado unashikilia udhehebu au udini, fahamu kuwa Kristo haji kunyakuwa watu wa namna hiyo. Atakuja kunyakuwa watu waliozaliwa kweli mara ya pili, kwa maji na kwa Roho na kusimama katika utakatifu. Hao ndio watakaokwenda kwenye unyakuo. Na kundi hilo litakuwa ni dogo sana, kama biblia inavyotabiri ,lakini wengine wote waliosalia wataingia katika dhiki kuu ya mpinga-Kristo.

Swali nj je! Wewe utakuwa miongoni mwa hilo kundi dogo litakalokwenda kumlaki Bwana mawinguni? Jibu, unalo, injili umesikia, na uzuri ni kwamba wokovu unapatikana bure, ukiukosa ni umejitakia mwenyewe kwa akili zao.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

UNYAKUO.

KWASABABU MUDA TULIOBAKIWA NAO SI MWINGI.

Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “Saa yangu haijawadia?”

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

YAFAHAMU MAPENZI KAMILI YA MUNGU KWA MAADUI ZAKO.

Rudi nyumbani

Print this post

YAFAHAMU MAPENZI KAMILI YA MUNGU KWA MAADUI ZAKO.

Haijalishi utaudhiwa na watu kiasi gani, haijalishi utakuwa na maadui wengi kiasi gani, lakini kamwe Mungu hawezi kuwachukia kama unavyowachukia wewe.

Jicho lako linavyowaona wewe ni tofauti na Mungu anavyowaona, wewe unatamani waangamizwe wapotee, lakini Mungu anatamani waokolewe. Wewe unatamani mabaya yawakute lakini Bwana Mungu anatamani watubu ili wasipatwe na mabaya. Ukiifahamu vyema tabia hiyo ya Mungu, utaacha kupoteza muda, kuwatakia shari maadui zako. Badala yake utawaombea Bwana azidi kuwapa neema watubu, na madhara yao yasikupate.

Lakini ukiwaombea kwa Mungu wafe!.utakuwa unapoteza muda, kwasababu kabla hawajawa maadui zako, Mungu alijua kuwa watakuja kuwa maadui zako na akawaumba hivyo hivyo.. angekuwa na hasira nao sana, kama ulizonazo wewe, angewaangamiza kitambo sana, au hata asingewaumba kabisa.

Kwahiyo mpaka unaona wameumbwa fahamu kuwa tayari ni mpango kamili wa Mungu wao wawepo duniani, na tena Mungu kawaumba kwasababu anawapenda.

Ni maneno magumu hayo lakini ndio ukweli.. Kama mtu fulani unamchukia kwasababu kakusengenya, na unatamani Mungu amwue, hayo maombi yako yatafika ukingoni!..kwasababu Mungu hatamwua kama unavyotaka wewe. Lakini ukitaka maombi yako yawe na nguvu ni heri uombe Bwana Mungu ampe roho ya kutubu, hapo utakuwa umeomba sawasawa na mapenzi yake.

Kama kuna mtu amekufanyia jambo baya, au anakufanyia mabaya yanayokuudhi sana. Na wewe ukaenda kuketi kuomba kwa Bwana Mungu kwamba amwue na kumpoteza kabisa, nataka nikuambie hayo maombi yako unapoteza muda. Kwasababu Bwana Mungu hakumuumba ili amwue, bali aifikilie toba na kubadilika… Ndio lengo lake!..kamwe huwezi kumfundisha Mungu ubaya.

Ezekieli 18: 23 “Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?”

2Petro 3:9b “….bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba”.

Mtu fulani kakuibia mali yako ambayo ni ya thamani, halafu unapiga magoti ukiomba kwamba Mungu amuue na kumuangamiza huko alipo, hayo maombi hayafiki popote. Maombi yenye tija na yanayompendeza Mungu, ni haya>>  “Bwana wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo”.

Mtu fulani kakuendea kwa mganga ili upatikane na madhara fulani, na wewe unapiga magoti na kusema “Bwana waangamizwe na kufa kabisa, hata maiti zao zisionekane”..huku ukinukuu mstari huu katika agano la kale Kutoka 22: 18 “Usimwache mwanamke mchawi kuishi”. Mbona unapomfumania mkeo, au mumeo kwenye uzinzi hunukuu huu mstari wa Agano la kale na kuutumia??.

Kumbukumbu 22: 22 “Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na mume, na wafe wote wawili, mtu mume aliyelala na mwanamke, na yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli”.

Au sio Mungu mmoja aliyezungumza hayo maneno??… Kama ni Mungu mmoja aliyesema usimwache mwanamke mchawi kuishi, ndio huyo huyo aliyesema mtu akishikwa kwenye uzinzi awe mwanamke au mwanaume  sharti auawe, (tena amezungumza hayo kwa kinywa cha Nabii huyo huyo mmoja, Musa)..basi kwanini unachukua mstari mmoja na kuacha mwingine??.

Hivyo ni vyema kufahamu utendaji kazi wa Mungu katika agano la kale ni tofauti na utendaji kazi wake katika agano jipya..Katika agano la kale, kutokana na ugumu wa mioyo ya watu, watu walipewa ruhusa ya kuua wazinzi, kuua waabudu sanamu wote wanaoziabudu nje na kumwabudu Mungu wa Israeli, walipewa pia ruhusa ya kuwapiga kwa mawe wachawi, na watu wote wenye pepo waliokuwa wanaishi katika nchi, walipewa ruhusa ya kuua watu waliomlaani/kumtukana Mungu, walipewa ruhusa ya kuwatenga watu wenye ukoma n.k. Na hiyo yote ni kutokana na ugumu wa mioyo yao, na wala si kwasababu ulikuwa ni mpango kamili wa Mungu. Mpango kamili wa Mungu ulikuja kuletwa na Bwana Yesu pale aliposema..

Mathayo 5:21 “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.

22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto”.

Mathayo 5.38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;

39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.

40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.

41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili”.

Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki”.

Kwahiyo hakuna jino kwa jino katika Ukristo, wala hakuna kumpiga kwa mawe mtu yeyote anayefumaniwa katika uzinzi, wala hakuna kumuua mchawi yeyote, wala haturuhusiwi kuwachukia maadui zetu. Haja za mioyo yetu kwa Mungu, na sala zetu, ni kwamba Bwana atuepushe na madhara yote yanayoweza kufanywa na wao wanaotuchukia, na Bwana azifedheheshe kazi zao, ili mwisho wanapoona kuwa hazina madhara yoyote kwetu, watubu na kumfuata Mungu wetu sisi, hilo ndio lengo la kwanza la Mungu. Lakini si wafe katika dhambi zao hizo.

Kwahiyo huwezi kumfundisha Mungu uovu, yeye atabaki kuwa mkamilifu siku zote, anawaangazia jua lake waovu na wema, huwezi kumbadilisha yeye kuwa hivyo, hata uombe maombi ya namna gani, isipokuwa anachokitaka kwetu ni sisi kuwa kama yeye, tuwe na huruma kama yeye, tuwe wenye rehema kama yeye, tuwe wenye fadhili kama yeye, tuwe watakatifu kama yeye.

Mathayo 5:46 “Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?

48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.

Bwana atubariki wote.

Kama hujampokea Yesu, jitafakari mara mbili unasubiri nini?. Injili si habari za kuburudisha kama tunazozisoma katika magazeti, bali ni ushuhuda, maana yake kila unapoisoma mahali au kuisikia mahali, inarekodiwa kuwa ulishawahi kuisikia, kwahiyo kama ukiipuuzia na kuiacha, na yule mwovu akaja kuchukua kile kilichopandwa ndani yako, kuna hatari kubwa sana itakayokukuta baada ya maisha haya.

Hivyo mpokee leo Kristo leo maishani mwako na wala usingoje kesho, kwasababu hujui yatakayozaliwa ndani ya siku moja, biblia inasema hivyo katika Mithali 27:1, na pia katafute ubatizo sahihi wa maji tele (Yohana 3:23) na kwa Jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38),kama bado hujabatizwa ubatizo sahihi. Na Roho Mtakatifu atashuka juu yako kukuongoza katika kweli yote.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

VITA DHIDI YA MAADUI

MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Je! Kuna malaika wangapi mbinguni?

Rudi nyumbani

Print this post