ALAMA ZA BENDERA YA ISRAELI ZINAWAKILISHA NINI?

ALAMA ZA BENDERA YA ISRAELI ZINAWAKILISHA NINI?

Wakati Mungu anawatoa Israeli kutoka Misri, Mungu hakuwapa bendera kuwa kama Ishara ya Taifa hilo, Hivyo bendera kwa Israeli ni kitu kilichokuja kuzalika miaka mingi baada ya Kristo kuja duniani katika harakati za kutafuta uhuru.

Sasa swali, ni je zile rangi katika bendera hiyo zinawakilisha nini?, Na ile nyota iliyopo katikati ya bendera inawakilisha nini?.

Bendera ya Israeli ina rangi mbili tu! Nyeupe na Blue (kwa kiswahili Samawi).
Rangi nyeupe inawakilisha utakatifu wa Mungu. Na Blue inawakilisha utukufu wa Mungu.

Tukitazama juu mbinguni, anga linaonekana la rangi ya Blue(Samawi).

Kufunua utukufu wa Mungu.Hata vitu vingine vya asili kama milima, bahari utaona vina mwonekano wambwa wa rangi hii ya blue kufunua utukufu wa Mungu.

Lakini kitu cha mwisho katika bendera ya Israeli, ni ile alama kama ya Nyota, yenye pembe sita, iliyopo katikati ya bendera hiyo.
Alama hiyo inajulikana kama Nyota ya Daudi au Ngao ya Daudi.

Imejulikana hivyo, kwasababu inaaminika Ngao ya Daudi ilikuwa na umbile hilo mfano wa hiyo nyota, na inaaminika ngao hiyo ilikuwa ina nguvu fulani ya kiungu.
Vile vile zile pembe sita katika hiyo ngao zinawakilisha zile tabia sita za Roho wa Mungu katika Isaya 11.

Isaya 11:2 “Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA”.

Na vile vile kama ilivyokuwa na pembe tatu mbili, moja inaangalia juu na nyingine chini, inawakilisha uhusiano wetu sisi na Mungu.

Ingawa hakuna mahali popote katika torati wala biblia nzima, nyota hiyo ilitajwa kwa sifa hizo, lakini wayahudi wa karne ya 17, walishawishika kuamini hivyo na kuitumia hiyo kama ishara ya Nembo ya Taifa lao, na hata kuitumia katika bendera yao.

Lakini katika jicho lingine, nyota hiyo inaaminika kama ishara ya Masihi, yaani Yesu Kristo, yeye ndiye Uzao wa Daudi, na ndiye ile nyota ing’aayo, ambaye Mataifa yote watamtumainia.

Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi”.

Lakini swali ni je! Bendera hiyo kwetu sisi wakristo, ina manufaa yoyote kiroho?, Kwamba tunapokuwa na bendera ya Israeli katika makanisa yetu, au katika vyombo vyetu vya usafiri, au katika nyumba zetu, tunakuwa tunajiongezea baraka??.

Jibu ni la!. Bendera ya Taifa la Israeli haituongezei chochote, zaidi sana mtu anapoiweka ndani kwake, na kuifanya kama mungu wake atakuwa anajizombea laana badala ya baraka. Kwasababu kwake yeye ni kama mungu.

Baraka pekee tunayoweza kuipata sisi ni kuishi kulingana na Neno lake na kanuni zake, utakatifu sawasawa na Waebrania 12:14, ndiyo bendera yetu, na alama ya kukubaliwa na Mungu..na sio bendera ya Israeli ndani kwetu.

Hivyo hakuna ulazima wowote wa Mkristo au mhubiri kutembea na bendera kana kwamba ndio kitovu chake cha baraka, labda atembee nayo kwa lengo lingine lakini sio hilo la kutafuta baraka kupitia hiyo.

Maandiko yaliposema “ambarikiye Israeli amebarikiwa” hiyo sio maana yake..Maana yake ni nyingine kabisa.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kama utapenda uwe unafikiwa na masomo ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP basi bofya hapa ujiunge moja kwa moja  >>>> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU

WEKA KUMBUKUMBU YA MAMBO BWANA ANAYOKUFANYIA KWASABABU YATAKUFAA MBELENI.

Neno Kupatiliza maana yake nini katika biblia?

Babewatoto ni nani katika biblia?(Isaya 34:14).

Ni kosa gani Daudi alilolifanya katika kuwahesabu watu, mpaka kupelekea vifo vya waisraeli wengi?

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jeremiah
Jeremiah
2 years ago

Asante kwakutu juza haya. Ubarikiwe.