Ni kosa gani Daudi alilolifanya katika kuwahesabu watu, mpaka kupelekea vifo vya waisraeli wengi?

Ni kosa gani Daudi alilolifanya katika kuwahesabu watu, mpaka kupelekea vifo vya waisraeli wengi?

Mfalme Daudi aliwahesabu wana wa Yakobo apate kujua idadi yao kamili, 1Mambo ya nyakati 21:7, jambo lililoonekana chukizo kwa bwana, mpaka kusababisha watu elfu sabini waangamie kwa tauni. SWALI. ni uovu gani hapo Daudi aliufanya ulete madhara hayo yote? au torati ilisemaje kuhusu watu kuhesabiwa?


JIBU: Hakukuwa na uovu wowote mkubwa kivile katika kuhesabu watu, japo Daudi alifahamu hakupaswa kufanya vile kwa wakati ule lakini yeye aliendelea kufanya ndio maana baadaye alikuja kujutia makosa yake, na kumwomba Mungu msamaha!. Lakini sasa swali linabaki pale pale ni kwanini kwa kosa lake mwenyewe lisababishe zaidi ya watu ya elfu 70 kuangamia kwa tauni? Mpaka kufikia hatua Daudi mwenyewe kumlalamikia Mungu, na kumwambia kwanini unawaadhibu watu wengine wasio na hatia kwa kosa langu mwenywewe? Kwanini Mungu afanye vile? Kwanini awaadhibu na watu wasio na hatia kwa kosa la mwingine?… Daudi hakufahamu sababu ya Mungu kufanya vile. Sasa ukisoma vizuri biblia, hiyo habari katika kitabu cha Samweli utaona jambo fulani pale la kuzingatia …

2 Samweli 24: 1 “TENA HASIRA YA BWANA IKAWAKA JUU YA ISRAELI, AKAMTIA DAUDI NIA JUU YAO, akisema, Nenda, ukawahesabu Israeli na Yuda. 

2 Basi mfalme akamwambia Yoabu, jemadari wa jeshi la askari, waliokuwa pamoja naye, Zunguka sasa katikati ya kabila zote za Israeli, tangu Dani mpaka Beer-sheba, mkawahesabu watu, nipate kujua jumla ya hao watu”.

Unaona hapo ukisoma mstari wa kwanza utaona, kuna jambo wana wa Israeli walilifanya hapo kabla mpaka kupelekea hasira ya Mungu kuwaka juu yao..Kama ukisoma huko nyuma utagundua kuwa Mungu alikuwa hapendezwi na njia zao tangu siku nyingi, na ndio maana wakati mwingine alikuwa anawatia katika mikono ya wafilisti, na hapa pia vivyo hivyo, kuna mambo maovu walikuwa wanayafanya pengine kwa siri au hadharani (japo biblia haijaeleza hapo ni mambo gani) lakini ni dhahiri kuwa matendo yao yalimudhi Mungu sana, mambo kama kuabudu miungu migeni, rushwa, kudhulumu watu, mauaji yasioyo na hatia, kuhalifu sabato, kupitisha wana wao motoni, kuwaonea wajane na mayatima ni miongoni mwa vitu walivyokuwa wanavifanya wana wa Israeli kwa wakati ule..Hivyo Mungu akaamua kumtumia Daudi nia kama sababu ya kuwaadhibu makosa yao…

Na ndio hapo tunakuja kuona Daudi anaingiliwa na shetani kufanya vile, kama tu vile Mungu alivyotaka kumwangamiza mfalme Ahabu akaruhusu Pepo la uongo likawavae wale manabii wake 400, kadhalika na Daudi naye aliingiwa na shetani kufanya mambo ambayo Mungu hakumwagiza , na baadaye tunaona tauni inakuja kuachiliwa juu ya Israeli ili Mungu kujilipizia kisasi juu yao wote waliomuudhi.. Hivyo wakati mwingine hata sisi kama taifa au mtu binafsi, tunaweza kufanya makosa, na Mungu akakusudia kutuadhibu kwa kupitia viongozi wetu, na ndio hapo unaweza kushangaa viongozi wanaonyesha tabia za ajabu kwetu au kwako, anakuwa mkatili au dikteta,sisi tukidhani kuwa yule kiongozi ndio kakengeuka, lakini kumbe nyuma yake ni Mungu kasimama kumruhusu kwa makusudi kabisa mtu yule atumiwe na ibilisi ili au kutufundishwe sisi adabu.

Mfano unaweza kuona Mfalme Nebkadneza alikuwa ni diktekta, aliteka mataifa yote ulimwenguni kwa nguvu na akayatawala kwa mabavu..na hata Taifa la Mungu Israeli liliwekwa chini wa utawala wa Nebkadneza lakini ukiisoma biblia kwa makini utaona kuwa Mungu ndiye aliyemtia Nebkadneza nia ya kwenda kuteka mataifa yote ulimwenguni pasipo hata yeye Nebukadneza kufahamu chochote…Na Mungu alifanya vile ili kujilipizia kisasi kwa mataifa yote yaliyomwacha ikiwemo na Taifa la Israeli watu wake. Hivyo tunapaswa tuwe makini na njia zetu tumwombe Mungu kila siku..Ili wengine wasifanyike kuwa fimbo ya Mungu kutuadhibu sisi.

Ubarikiwe.


Mada nyinginezo:

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU:

KAMA UNAPENDA MAISHA, NA KUTAKA SIKU YAKO IWE NJEMA.

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE:

JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?

JE! NI HALALI KUTOA CHETI KWA WAKRISTO WANAOOA?

JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments