KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?

KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?

Hili ni swali ambalo lilikuwa sana katika kichwa changu kabla sijamfahamu Yesu Kristo, vilevile lipo katika vichwa vya watu wengi leo hii duniani, na nimeshaulizwa pia mara nyingi na baadhi ya watu?.. Hili swali linaibuka kutokana na jinsi watu tulivyojikuta tu ghafla tumetokea duniani bila hata ya kikao Fulani cha makubaliano, na jinsi tunavyoondoka ghafla bila hata ya taarifa zozote,.. Hapo ndipo tunajiuliza sasa maana ya Maisha ni nini? Na ni nani aliye nyuma yake?..Hivyo inatufanya kila mmoja kwa njia yake mwenyewe aanze kuchunguza na kutafiti na kujaribu kila njia na kila mbinu, ili mwisho wa siku apate jibu lake moja ambalo litampa sababu ya yeye kuwepo hapa duniani..

Hata kama ni wewe leo hii unajiuliza swali hilo, hujakosea hata kidogo kufiria hivyo, unawaza vyema kabisa.. Lakini nataka nikupe ushauri mmoja, kabla hujaanza kuchunguza kwa njia zako wewe mwenyewe embu jaribu kwanza kutafuta waliowahi kujiuliza swali kama hilo na hatua walizochukua na mwisho wao ukawaje?..Ili usije ukajikuta unarudia njia zilezile za kwao, na mwisho wa siku ukafikia pale pale walipo ukawa umepoteza muda mwingi wa utafiti ambao sio wa lazima.

Lakini leo hii nitakupa majibu ya kibiblia.. Na kitabu pekee ambacho kimetoa majibu ya maswali hayo ni kitabu cha Muhubiri..Hivyo kama unahitaji kupata jibu la swali hilo nakushauri ukisome kitabu chote kile kwa utaratibu na kwa umakini kisha utapata jibu lake mwishoni.

Aliyeandika kitabu kile ni Sulemani mwana wa Daudi, ambaye biblia inarekodi sio tu alikuwa ni mfalme mkuu sana bali pia alikuwa ni mtu mwenye Hekima kuliko watu wote waliokuwa wanaishi duniani wakati ule, na alikuwa pia ni mtu Tajiri ambaye hakukuwa na mfano wako, kabla yake na hata baada yake..

Sasa ilifikia kipindi akatamani kujua sana nini maana ya Maisha, na atafanya nini ili apate raha duniani, au apate jibu moja la uhakika kuhusu Maisha ya wanadamu,..Akasema nitajaribu kila kitu, na kila njia kwanza naanzana na Elimu, akaitafuta elimu kwa bidii, akaipata akawa na elimu kubwa ya kufahamu kila kila mnyama, na mmea, na viumbe vyote duniani (1Wafalme 4:33-34) na hekima iliyopo ndani yao, akaweza kutatua mafumbo magumu sana, akatunga mithali nyingi sana. Na akaandika vitabu vingi sana, hiyo yote ilikuwa ni kwa lengo la kupata labda jibu Fulani la Maisha pengine angegundua jambo Fulani ambalo lingemsaidia kupata kanuni rahisi ya watu kuishi duniani, au Maisha ya raha, na ya uhuru au ya furaha..lakini alipojaribu kufanya hivyo, ndivyo alivyozidi kuongezea huzuni na masikitiko anasema hivyo (Mhubiri 1:18) ..

Akasema nitajaribu wanawake..Akaenda kuoa wake 700 wazuri wanaotoka katika majumba ya kifalme tu, na Masuria 300, aangalie labda akiwa na hao atayafanya Maisha kuwa bora duniani, au ya furaha ..hilo nalo halikumletea majibu aliyokuwa anayatafuta..

Akajajiengea makasri makubwa, na kujiwekea posho ya chakula cha mwaka mzima, kila siku kwake ilikuwa ni sherehe..lakini bado hakukipata alichokuwa anakitafuta..

Akajaribu pombe, akawa anakunywa divai, lakini bado hakuna lolote aliloliona ndani yake lingeweza kufichua fumbo kubwa la maisha..akajaribu “upumbavu na wazimu” biblia inasema hivyo katika (Mhubiri 1:17), yaani mambo yote ambayo unaweza kuona ni ya kipumbavu, au wendawazimu kama vile kujitukuza, pengine kucheza dansi, n.k. lakini hakuna hata mmoja liliweza kumpa maana ya mambo yote, ..

Akajaribu kuwa na malengo makubwa akawa mfanya biashara mkubwa duniani, aione labda akishafanikiwa hapo atakipata kitu alichokuwa anakitafuta..lakini bado anasema hakukipata..

Ndipo katika dakika za mwisho, sasa katika uzee wake..Anagundua siri hii kuwa mambo yote ni ubatili, mito inapotoka ndipo huko huko inaporudi, jua linapochomozea ndipo huko huko litakuja kuchomozea tena, upepo unapovuma ndio kulekule utakaporudi kila kitu kipo katika mzunguko wake, Yule Mungu niliyeanzana naye, nitakapojitaabisha kwenda mbali naye, nitakaposema simtaki tena nataka nitafute mwenyewe akili zangu niijue ukweli wa Maisha, ndiye yule yule mwisho wa siku nitamrudia…

Unaweza Ukaona kumjua yeye kunakunyima uhuru wa kuishi..Utakwenda kutafuta unachokitaka katika moyo wako, lakini mwisho wa siku utamrudia yeye..Na hapo utakuwa umeshachelewa sana..

Ndio maana Mhubiri anamalizia kwa kusema…Jumla ya mambo yote ni UMCHE MUNGU…

Mhubiri 12:13 “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya”.

Unaona,..Mhubiri ni mmojawapo wa waliotusaidia sisi kufanya utafiti, ili na sisi tusianze tena kupoteza muda mwingi kukimbizana na mambo ya Maisha tuanze kutafiti kwa akili zetu..tukidhani kuwa tutafika mahali Fulani paki pekee ambako wengine hawajafika kuhusu maisha,…kumbe tupo kwenye mzunguko ule ule wa zamani..

Leo hii tutamwacha Mungu tukatafute fedha, lakini tukishaiapata bado tutaona mbona hatujalipata lile kusudi lenyewe ndani yetu?..Tutamdharau Mungu tutasema tukatafute hekima yetu wenyewe…ni kweli tutafahamu vyote lakini mwisho wa siku swali litaendelea kubakia pale pale maana ya Maisha ni nini?

Jibu pekee la maana ya Maisha lipo kwa yeye aliyetuumba?

Mche yeye basi!… Na kumcha yeye ni kuingia katika kanuni yake.. Ambayo aliiweka tangu zamani kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwenguni.. Na kanuni yenyewe ndio hii..

Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.

Ukimpata Yesu Kristo, hapo pekee ndipo utakapojua maana ya Maisha ni nini.. Kwasababu yeye anakupa uzima wa milele..Ukiwa na uzima wa milele wasiwasi wako utakuwa ni nini tena?….hutakuwa na hofu yoyote, na Maisha yako yatakuwa ya amani na furaha hapa duniani sikuzote..yaliyo mbali na utumwa wa hofu za Maisha..Hofu za kuogopa kesho itakuwaje..kwasababu Sulemani ndivyo alivyosema katika ..

Mhubiri 8:6 “Kwa maana kwa kila shauri kuna wakati na hukumu; kwa sababu mashaka ya mwanadamu yaliyo juu yake ni makubwa;

7 kwa kuwa hajui yatakayokuwako; kwa maana ni nani awezaye kumweleza jinsi yatakavyokuwa?

Hivyo kama na wewe bado unatafuta maaana ya Maisha, basi leo hii fahamu kuwa jibu ndio hilo hapo juu..acha kutanga tanga, mfuate YESU, akuponye nafsi yako, akupe tumaini la uzima wa milele..Uishi kwa amani siku zako zote ulizopo hapa duniani..Kwasababu kwingine kote hutapata..na kama ukijaribu kutafuta peke yako, ukweli ni kwamba utarudi hapo hapo kwa Mungu..Na wakati huo utakuwa umeshachelewa tayari.

Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo..Na kwamba unataka Kristo aingie ndani ya Maisha yako, akupe tumaini hilo na amani hiyo ya wokovu..

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ukizingatia hayo Bwana atakuangazia Nuru zake za wokovu daima hadi siku ile ya mwisho.

Ubarikiwe sana

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

IVUMBUE INJILI YA KRISTO KUTOKA KATIKA KILA JAMBO.

Nifanye nini ili niwe na uhakika nikifa naenda mbinguni?

KARAMA YA MUNGU NI UZIMA WA MILELE.

Ikiwa sisi tuliumbwa na Mungu,Je! Mungu aliumbwa na nani?

NITAPOKEAJE NGUVU YA KUSHINDA DHAMBI?

JE UNAMTHAMINI BWANA?

CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

NIilikuwa kipofu sasa naona amen na immanuel naitwa ibrahimu

starring
starring
1 year ago

this is beutiful

John John kevela
John John kevela
2 years ago

Ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu,Mungu akuinue hakika nimekua nakaa uweponi mwa Mungu MDA wotr kupitia mandiko yako,Amen kwa majina naitwa John