IVUMBUE INJILI YA KRISTO KUTOKA KATIKA KILA JAMBO.

IVUMBUE INJILI YA KRISTO KUTOKA KATIKA KILA JAMBO.

Shalom..Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe…

Karibu tujifunze biblia…

Katika biblia kama wengi wetu tujuavyo…Kuwa maisha yanahubiri Injili, kadhalika vitu vya asili vinahubiri Injili…maana yake Mtu akijaliwa hekima mno kwa kuvisoma tu vitu vya asili anaweza kupata ufunuo mkubwa sana wa vitu vya ufalme wa Mbinguni..

Tukimwangalia kama Bwana wetu Yesu Kristo, kila mahali alikuwa anasema ufalme wa mbinguni umefanana na hiki au kile…Utaona kuna sehemu anasema

“ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;

lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Mathayo 13:24-26”..

Sehemu nyingine anasema Ufalme wa mbinguni umefanana na mpanzi aliyetoka kwenda kupanda mbegu zake, nyingine ziliangukia njiani ndege wakazila, nyingine kwenye miamba, nyingine kwenye miiba na nyingine kwenye udongo mzuri.. Maana yake ni kwamba kumbe hata katika ulimaji na upandaji kuna injili ya Kristo mule.. kwamba inahitajika hekima kiuvumbua.

Hata jinsi wezi wanavyovunja usiku na kuiba..kuna injili ndani yake…(Bwana Yesu alilifananisha tukio la kuja kwake na tukio la wizi usiku wa manane wakati tulalapo)…Hata katika mafisadi kuna injili ndani yake (kasome Luka 16:1-12)..Hivyo inahitajika hekima ya kiMungu kuivumbua bila kuiga mabaya hao.

Vivyo hivyo ukirudi katika miti kuna injili(Mathayo 13:31-32), katika ndege kuna injili (kasome Mathayo 6:26)..katika mapishi kuna injili (kasome Mathayo 13:33)..katika kufanya biashara kuna injili (Mathayo 13:45)…katika wavuvi kuna injili (kasome Mathayo 13:47)….katika kutafuta Ajira kuna injili pia (soma Mathayo 20:1-10).

Kadhalika katika kuoa na kuolewa na kualikwa katika harusi kuna injili (kasome Mathayo 22:1-13)..

Kwahiyo utaona karibia kila kitu kinahubiri Injili…Hakuna kitu hata kimoja kisichohubiri Injili…Inahitajika tu hekima kupata fundisho au funzo la kiMungu katika kila kitu.. Na ndio maaana mtu kama Sulemani Mungu alimpa hekima nyingi ya kufahamu kanuni za ki-Mungu duniani kwasababu alitazama karibu kila kitu kwa jicho la kumwona Mungu ndani yake, ndipo Hekima ikaingia ndani yake..

1Wafalme 4:32 “Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano.

33 Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki.

34 Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake”.

Hivyo huu sio wakati wa kulala tena bali wakati wa kumwomba Roho Mtakatifu atufungue macho ya rohoni tuweze kuielewa injili inayojihubiri yenyewe katika kila kitu na kuifanyia kazi…Tukiwatazama ndege na wanyama hatuoni wanyama mashoga wala wasagaji hiyo ni injili ikitufundisha kuwa usagaji na ushoga si mpango wa Mungu..ni machukizo mbele za Bwana Yesu.

Tv tulizonazo, internet pamoja na simu zinatuhubiria Injili…Leo hii tukio dogo tu likitokea katika kijiji Fulani ndani sana kwa kupitia simu za mkononi..ndani ya dakika chache sana litaweza kuwa limeshamfikia hata Raisi wa nchi…ikifunua kuwa hata mtu chochote anachokifanya akiwa hapa duniani ndani ya muda mfupi sana kitakuwa kimeshamfikia Mungu wa mbingu na nchi..

Mahakama zinahubiri Injili..kama mtu akikutwa na kosa ambalo linamfanya asiendelee kukaa katika jamii yake tuchukue mfano labda kaua…cha kwanza atakamatwa na mapolisi, na kupelekwa mahabusu, kabla ya kuhukumiwa kisha atapandishwa kizimbani mahakamani kusomewa hukumu yake na baada ya hapo magereza..atakaa huko bila kurudia maisha yake ya asili kwa kipindi cha chote cha maisha yake..

Na hukumu ya Mungu mwenyezi ndio ipo hivyo hivyo…

Leo hii mtu akifanya dhambi hata zikamfikia Mungu, na alishaonywa na hataki kutubu anaendelea tu kufanya kwa makusudi…mtu Yule atakufa katika dhambi zake..hapo ni sawa na amekamatwa, na moja kwa moja atapelekwa jehanamu/kuzimu kafungwa huko…ambapo ni mfano wa mahabusu(magereza ya kitambo)…atakaa huko kwa kipindi Fulani akingoja siku atakayopandishwa mbele ya kiti cheupe cha Hukumu cha Mungu mwenyezi..ambapo atahukumiwa kulingana na matendo yake na kasha kutupwa katika lile ziwa la moto ambalo linafananishwa na magereza ya milele katika mazingira ya dunia yetu.

Mambo yote tukiyatafakari kwa jicho hilo..hatutaendelea kuuchukulia wokovu wetu kama ni jambo si la kuchezea bali tutauheshimu na kuushikilia sana kwa maana ni kitu cha thamani tulichopewa. Hizi ni nyakati za mwisho.

Bwana atusaidie sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Mada Nyinginezo:

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA

Mbona Mungu anaruhusu watu wapate shida, ilhali ana uwezo wa kutuepusha?

LOLOTE ATAKALOWAAMBIA FANYENI.

Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?

JIHADHARI NA KUOSHWA MIGUU ISIVYOPASWA.

UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.

Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?

UBATILI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments