SWALI: Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe, kwanini asingeyatoa tu na kuyaacha yaende sehemu nyingine mbali na wale nguruwe, kwani kufanya vile si ni kama aliharibu biashara au mali za wengine?
JIBU: Kulikuwa na sababu kuu mbili kwanini lile tukio litendeke vile:Sababu ya kwanza ni kwasababu yale mapepo yenyewe yalimwomba Bwana yawaingie wale nguruwe..Na sababu ya pili ambayo ndio kuu, ni ili Mungu atengeneze ushuhuda wenye nguvu zaidi utakaoweza kuwavuta wanadamu wengi watubu kirahisi.
Kumbuka kuwa pale awali, Yesu alipoliuliza lile pepo jina lako ni nani..lilijibu na kusema jina langu ni LEGIONI kwasababu tupo wengi..Na Legioni kwa zamani lilikuwa ni jeshi lenye askari si chini ya 82,000..Hivyo piga hesabu mapepo yaliyokuwa ndani ya Yule mtu hayakupungua idadi hiyo, jaribu kufiria jambo hiyo si rahisi kuamini na wengi kama lingewezekana mtu kuwa na idadi kubwa ya mapepo namna hiyo .
Hivyo Yesu kuona vile, kuwa wameomba jambo ambalo litaufanya ushuhuda uwe na nguvu zaidi, na kwamba kwa kupitia huo utawahakikishia kuwa mapepo kweli yapo, na kwamba yanaweza kumuingia mtu kwa wingi wa idadi ile, na kwamba yanaweza kumvaa mtu na kumfanya afanye vitu ambavyo yeye mwenyewe hajataka kuvifanya ikiwemo hata kujiua..Ndio akaruhusu yawaingie wale nguruwe ambao walikuwa 2,000,.Ambayo kwa hesabu za haraka haraka nguruwe mmoja aliingiwa na mapepo si chini ya 40,..aliruhusu hivyo ili watu waone kwa macho yao, kwamba mapepo yapo na jinsi mapepo yakimwingia mtu yanavyomfanya na yanapompelekea mwishoni..MAUTINI..Kwahiyo kwa tukio lile ndipo tulipofahamu kuwa mapepo sio nadharia bali ni vitu halisi kabisa…
Hivyo wale wachungaji walivyoshuhudia kitendo kile tu, waliondoka na kwenda kuhubiri mashambani na na vijijini matendo makuu waliyoyaona kwa macho yao, ndipo wale watu waliohubiriwa na wachungaji pia wakaja kushuhudia kwa macho yao..kuona wale nguruwe wakielea ziwani wote wamekufa, na mtu Yule ni mzima kabisa wataachaje kuamini?…Kwasababu hakuna mtu mwenye nguvu ya kwenda kukamata nguruwe 2000 na kuwazamisha baharini..ni lazima kuna nguvu nyingine ya zida imehusika hapo.
Vile vile na Yule mtu aliyekuwa kichaa alipokwenda kuhubiri na kutoa ushuhuda ule mzito sio ajabu biblia inatuambia alipoenda kuhubiri huko Dekapoli watu wote WALISTAAJABIA, walichokistaajabia ni nini kama sio huu ushuhuda wa nguruwe kuingiliwa na mapepo?. Na hapo pia bila shaka wengi walitubu kwa kupitia ule. (Soma Marko 5:12-20)..Kama vile ulivyokuwa ushuhuda wa Nabii Yona…watu waliposikia jinsi alivyokaa tumboni mwa samaki siku tatu bila kufa..wakaamini na kutubu kwa ishara ile.
Hivyo hata leo hii, Kristo anaweza kuruhusu mtu apate hasara Fulani ili uwe ushuhuda wa kuwaponya watu wengine. Shetani alimwomba Mungu ampige Ayubu, kama tu haya mapepo yalivyoomba ruhusa Bwana Yesu kuiharibu mifugo ya wengine..Lakini kwa kupitia maisha ya Ayubu sisi leo hii tunaponyeka. Hivyo si kila adhabu ambayo hukustahili inapokupata, ikufanya umchukie Mungu, mengine ni kwa utukufu wa Mungu, zaidi zidi tu kusonga mbele maadamu wewe bado ni mwana wa MUNGU.
Ubarikiwe.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
USIPOKUWA MWAMINIFU, NAFASI YAKO ITACHUKULIWA.
INGIENI KWA KUPITIA MLANGO ULIO MWEMBAMBA.
TAZAMA KRISTO YUPO HAPA,AU YUKO KULE MSISADIKI.
MAMBO 5 AMBAYO KILA MKRISTO ANAPASWA KUFAHAMU.
TUUTAZAME PIA MWISHO WA UJENZI WETU.
Uasherati wa Kiroho maana yake nini?
Rudi Nyumbani:
Print this post
barikiwa sn
Amen nawe pia ndugu yetu..