SAKRAMENTI NI NINI, NA JE! IPO KATIKA MAANDIKO?

SAKRAMENTI NI NINI, NA JE! IPO KATIKA MAANDIKO?

Kulingana na kanisa Katoliki Sakramenti Ni ishara ya wazi ionekanayo, ya neema isiyoonekana, iliyofanywa na Yesu Kristo mwenyewe, itumike kutuletea au kutuongezea neema mioyoni mwetu.

Yaani kwa lugha nyepesi ni ishara za nje zionekanazo zilizobeba neema ya wokovu,  zilizofanywa  kwanza na Bwana Yesu, ambazo tukizifanya na sisi zitatuongezea neema moyoni mwetu ya kumkaribia Mungu Zaidi.

“Kulingana na kanisa Katoliki SAKRAMENTI hizi zipo saba (7), Nazo ni:

Ubatizo:

Kwamba kila mtu anayekuja katika ukristo ni sharti aupokee ubatizo, haijalishi ni Watoto wachanga, au vijana,au watu wazima, hawana budu kuupokea ubatizo. Ni ishara ya nje ya kuingizwa katika imani ya kikristo. Hii ni sakramenti ya kwanza.

Kipaimara:

Kipaimara ni Neno lenye maana ya “uthibitisho”. Kulingana na imani ya kikatoliki, ubatizo peke yake hautoshi, unahitaji kukamilishwa na tendo lingine la kipaimara kwa kuwekewa mikono. Hivyo Siku ambayo mtu huyo anapokea kipaimara hicho huwa anapakwa mafuta ya kunukia kwenye paji la uso wake yajulikanayo kama KRISMA, kama ishara ya kutiwa muhuri kuwa mtu huyo ni milki halali ya Bwana, kufuatana na andiko hili (Yohana 6:27). Hii ndiyo sakramenti ya pili.

Ekaristi Takatifu:

Kushiriki meza ya Bwana. Kuula mwili wa Bwana na damu yake.. (1Wakorintho 11:23-25). Kama vile Bwana Yesu alivyowaagiza wanafunzi wake wafanye vile kwa ukumbusho wake.

Mpako Mtakatifu:

Hii ni ibada maalumu kwa ajili ya wagonjwa kama ilivyofanywa na mitume kwa agizo la Yakobo (Yakobo 5:14) ..Mathayo 10:1, Marko 6:3…Hii nayo ni moja ya sakramenti ya Bwana.

Kitubio:

Inahusisha kuungama dhambi, na hii ni lazima uende mbele za Padri na kuzikiri dhambi zako mbele zake, na yeye atakuombea na dhambi zako zitaondolewa kama agizo ambalo Kristo aliwapa mitume wake..(Yohana 20:23).

Daraja Takatifu:

Uteuzi wa Vyeo katika kanisa..kama vile ukasisi, ushemasi, na uaskofu.Kama vile jinsi Bwana Yesu alivyowachagua mitume wake,.Na vivyo hivyo uteuzi katika kanisa ufanyike katika kuliongoza kundi, hiyo inafuatana na kuteuliwa na kuwekewa mikono na askofu wa jimbo.

Ndoa;

Ndoa ya wakristo ni sakramenti ya Yesu na kanisa lake. Ufunuo 21;9..Kama vile Kristo alivyoona na kanisa lake, vivyo hivyo ndoa inafunua sakramenti hiyo.

  • Kulingana na imani ya katoliki Sakramenti tatu za kwanza ni za kumuingiza mtu katika Ukristo.
  • Sakramenti mbili zinazofuata ni za uponyaji wa roho na mwili.
  • Sakramenti mbili za mwisho ni za kuhudumia ushirika katika kanisa na katika familia iliyo kanisa dogo.

Lakini Je! Maagizo haya yote ni ya kibiblia na Je ni lazima kila mkristo ayafuate ili apokelewa na Mungu?..

Ukweli ni kwamba agizo la ubatizo ni agizo la msingi katika Imani, lakini ubatizo unakuja kwa mtu aliyetambua kwanza kuwa yeye ni mwenye dhambi na hivyo anahitaji KUOKOLEWA. Hapo ndipo anapotubu na kwenda kubatizwa kwa hiari yake mwenyewe. Lakini mtoto mchanga hajatambua bado  jema na baya, wala yeye mwenyewe hajitambui hivyo ubatizo kwake hauna maana.. wao wanawekewa tu mkono, kama wakfu kwa Bwana. Lakini sio kubatizwa.. Hivyo suala la ubatizo kwa vichanga ni batili.

Ubatizo sahihi ni upi?

Kwahiyo ubatizo sahihi ni ule wa kujimbua kwanza, wewe ni mwenye dhambi na kwamba unahitaji kuokolewa, vile vile ni sharti uwe wa maji tele sawasawa na Yohana 3:23, Na uwe kwa jina la Yesu Kristo sawasawa na maandiko haya (Matendo 2:38, 8:16, 10:48, 19:5), ubatizo mwingine nje ya hapo ni batili kulingana na biblia, hivyo kama ulibatizwa tofauti na hapo unahitaji kwenda kubatizwa tena.

Vilevile Watoto wachanga ni kweli wanapaswa wawekewe mikono kama mbaraka kutoka kwa Bwana. Sawasawa na Bwana Yesu alivyofanya (Mathayo 19:14-15)..Lakini sio kwenda kupitia mafundisho Fulani ya mapokeo kwanza mwaka mzima na ndipo baadaye aje kuwekewa mikono na askofu au Padre..Agizo hilo halipo kwenye maandiko.

Utumizi wa mafuta.

Halikadhalika, utumizi wa mafuta kwa ajili ya kuombea wagonjwa si jambo la kuliundia kanuni..kwasababu sio mafuta yanayomponya mtu bali kinachoweza kumponya mtu ni damu ya Yesu tu peke yake. Kwasababu biblia imetuambia..yoyote tufanyayo tufanye yote kwa jina la YESU Kristo. (Matendo 4:12)

Na mwisho kabisa, kuwekewa mikono kwa ajili ya utumishi na waliokutangulia kwenye Imani ni jambo jema lakini pasipo hilo haimaanishi kuwa huwezi kutumika katika kuifanya kazi ya Mungu sawasawa na wale wengine. Ikumbukwe kuwa mitume 12 walichanguliwa kweli na Bwana Yesu Kristo, wakaishi naye, wakala naye, wakapewa agizo naye.Lakini biblia inatuambia Mtume Paulo alitenda kazi Zaidi ya hao wote, na yeye hakuwa miongoni mwa wale 12, wala hakuwahi kutembea na Yesu duniani,.

Utume wetu unathibitishwa na Roho Mtakatifu ndani yetu. Ni vema kumtafuta Roho Mtakatifu, kuliko kutafuta vyeo. Kwasababu yeye ndiye anayewatia nguvu wateule wake katika kumtumikia. Hata wewe Bwana anaweza kukufanya kuwa mtumishi wake, endapo tu utatii na kuwa mwaminifu kwa kila anachokulekeza kukifanya.

Hivyo ndugu, toka katika kamba za udini, na kamba za mapokeo, ambazo nyingi ya hizi zinakufunga usiomwone Mungu katika utimilifu anaotaka. Rudi kwenye Neno. Penda kujifunza kusoma biblia peke yako huku ukimwomba Roho Mtakatifu akusaidie. Penda pia kujifunza sehemu mbalimbali, na Roho Mtakatifu atakusaidia kuchagua kilicho sahihi na kutupa kisichosahihi, kwasababu ndiyo kazi yake hiyo Yesu aliyosema amemtuma duniani kwayo..(Yohana 16:13)

Je umeokoka?

Je! Unajua kuwa tunaishi katika kanisa la mwisho la saba lijulikanalo kama LAODIKIA, na UNYAKUO upo karibu..Siku yoyote wateule watotoweka na kwenda mbinguni kwa BABA..? Kama hujafanya hivyo ni heri ukamgeukia Mungu wako sasa, kwasababu muda tuliobakiwa nao ni mchache kabla PARAPANDA haijalia. Kama upo tayari kutubu dhambi zako leo na kusema nataka leo hii Bwana Yesu aanze kutembea na mimi maishani mwangu..

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya Kipaimara?..Na je! Ni jambo la kimaandiko?

Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?

UNYAKUO.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

KWANINI WENGINE WANYAKULIWE,NA WENGINE WAACHWE?

JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Mussa
Mussa
3 years ago

Sakrament kwanin loma zipo saba wakat NEW APOSTOLIC CHARCH ZIPO 3