KWANINI WENGINE WANYAKULIWE,NA WENGINE WAACHWE?

KWANINI WENGINE WANYAKULIWE,NA WENGINE WAACHWE?

Ni kwasababu ile ile kwanini Henoko alitwaliwa, na wengine wakabaki, Na Eliya alinyakuliwa na wengine wakabaki. Mungu aliruhusu kwa makusudi kabisa watu hawa wawe mfano wa mambo hayo ili kutupa sisi picha halisi kitakachotokea siku ile ya Unyakuo…Tukianzana na Henoko biblia imeshatupa majibu kabisa ni kwanini alinyakuliwa ..Inasema Ni kwasababu alitembea na Mungu (alimpendeza Mungu) kwa miaka mia tatu (Mwanzo 5:22).

Mwanzo 5:24 “Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa”.

Waebrania 11:5 “Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu”

Unaona Hawa ni watu ambao walivuka viwango vya kawaida vya kuishi Maisha ya kumpendeza Mungu tofauti na watu wengine..Na hivyo Mungu akaona si vema waendelee kuwepo mpaka siku ya mwisho ya uhai wao, akawatwaa. Ndivyo itakavyokuwa siku ile ya Unyakuo. Wengi tunavyodhani watakaonyakuliwa watakuwa ni wengi sana, kwamba hata kama mtu anaishi Maisha ya kutouthamini wokovu wake hapa duniani, naye pia atakwenda..Jibu ni hapana, watakuwa ni wachache sana nao ni wale watu ambao watakidhi hivyo vigezo vya kumpendeza Mungu kama Henoko…Soma Mathayo 7:14,na Luka 13:23.

Na ndio maana siku ile muda mfupi kabla ya kuja kwa Bwana biblia inatuonyesha kuwa kutakuwa na makundi mawili wa wakristo. Kundi la kwanza litajulikana kama wanawali wapumbavu, na kundi la pili litakuwa la wanawali werevu (Mathayo 25). Hawa werevu ndio wale ambao watatambua majira ya kujiliwa kwao, kutokana na dalili za mwisho wa dunia zinavyojionyesha, hivyo wataanza kutengeneza mambo yao sawa mapema kabisa kabla ya wakati ule kufika kama Henoko alivyojuwa kuwa dunia inakaribia kuangamizwa akatengeneza mambo yake sawa …

Hivyo ule wakati utakapokaribia na Mungu kuiona Imani yao , na utayari wao kuwa macho yao siku zote yapo mbinguni..Hao ndio watakaonyakuliwa na kutoweka ghafla..hawataonekana…Mungu atawaepusha na ile hukumu inayokuja pamoja na dhiki kuu.

Lakini wengine ambao ndio wale wanawali wapumbavu, wanasema wanamngojea Bwana lakini Maisha yao sio kama watu wanaomngojea Bwana kama biblia inavyotuasa katika Luka 12:35-36..Nusu dunia, nusu Mungu, hawajibidiishi kwa Mungu, wao wakishaokoka na kubatizwa hiyo tu inatosha,hakuna haja ya kujua Zaidi chochote kinachohusiana na Maisha baada ya hapa, kusikia habari za kwenda mbinguni kwao ni kama habari za kale,..Sasa hawa ndio siku ile watajikuta wameachwa…

Sasa Tukirudi kwa Eliya naye Kama vile Elisha alivyomshuhudia akiondoka mbele zake, na akalia kilio kikubwa sana..Ndivyo itakavyokuwa kwa kundi hili la wakristo hawa

vuguvugu,watakavyolia siku ile.. kwasababu siku hiyo watakuwa karibu sana na wale watakaonyakuliwa au watawashuhudia wakitoweka ..

Mathayo 24:40 “Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;

41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa”.

Unaona, unabii huu utatimia siku hiyo kwao, kwasababu watakuwa karibu sana na wale watakaonyakuliwa kwasababu wote ni watu wa kanisani?. Je! Utajisikiaje siku ile yule jirani yako anayejulikana kama mlokole ambaye unajua alikuwa amejikana nafsi hayupo?..Huyo rafiki yako ambaye unaenda naye ibadani kila siku ghafla tu anatoweka mbele ya macho yako? Utajisikiaje..Kuona huyo mke wako/mume wako ambaye hakuruhusu Maisha ya dhambi yamkaribie usiku ule ukiwa naye nyumbani ghafla anatoweka..Utajisikiaje, tafakari ndugu kuona mchungaji wako aliyekuwa anakukemea kila siku habari za kuvaa vimini, na suruali, na uzinzi hayupo tena.. Itakuwa ni kilio na kusaga meno kwako wewe unayejiita mkristo lakini ni vuguvugu..Na cha kusikitisha ni kuwa kundi hili litakaloachwa litakuwa ni kubwa sana.

Wakati huo wenye dhambi hawataelewa chochote, watasikia tu uvumi, lakini kwao haitakuwa habari ya kushutua kama kwako..Wenyewe watasikia tu kwenye vyombo vya habari kuwa watu fulani wachache sana wamepotea lakini watapatikana,..kwasababu hawatakuwa wengi, kama tunavyodhani leo hii… kumbuka alinyakuliwa Henoko tu peke yake kati ya mamilioni ya watu waliokuwa duniani wakati ule, alinyakuliwa Eliya tu kati ya mamilioni ya watu waliokuwa duniani wakati ule..Vivyo hivyo watanyakuliwa wachache sana katika ya mabilioni ya watu waliopo duniani leo hii..

Huu sio wakati wa kumwangalia mjomba, au shangazi, au ndugu, ili kumfuata YESU, Huu ni wakati wa kujitwika msalaba wako wewe kama wewe. Sio wakati wa kusema mbona fulani yupo hivi, mbona mchungaji wangu anaishi vile.. kumbuka wewe sio yeye, na yeye sio Mungu kwamba unaouhakika siku ile atanyakuliwa..Fanya bidii wewe kama wewe kuutafuta uhusiano wako binafsi na Kristo ili siku ile isikupite. Vivyo hivyo na mimi ninafanya hivyo..Na mtu mwingine yeyote anayejiita mkristo anapaswa afanye hivyo. Kwasababu kwenda katika unyakuo sio lelemama..

Tusipumbazwe na kundi hili kubwa la wanawali wapumbavu tulionao katika ukristo. Sisi tusonge mbele na Bwana atakuwa pamoja na sisi hadi siku ile ya uyakuo itakapofika.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Mada Nyinginezo:

KWANINI MUNGU ALIMTUMIA MUSA KWA VIWANGO VILE?

MAMBO 5 AMBAYO KILA MKRISTO ANAPASWA KUFAHAMU.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?

Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?

WANA WA MUNGU, NA BINTI ZA WANADAMU.

NDUGU,TUOMBEENI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments