JE! UNAYATUNZA MAVAZI YAKO?

JE! UNAYATUNZA MAVAZI YAKO?

Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)”

Vazi ni kitu kinachositiri mwili…Mwili ukikosa mavazi unakuwa tupu/uchi. Na ni aibu kuwa uchi…Lakini pia upo utu wa ndani ambao nao pia unahitaji mavazi..ukikosa mavazi nao pia ni sawa na upo uchi na aibu yake huo ndio kubwa zaidi.

Katika hichi kipindi cha kumgoja Bwana..Biblia inatuasa tuhakikishe nafsi zetu zina mavazi yapasayo…na Mavazi yenyewe si mengine zaidi ya matendo mazuri ya utakatifu. Tunasoma hilo katika

Ufunuo 19:7 “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu”.

Kitani inayozungumziwa hapo ni “vazi zuri refu la thamani na leupe”…Hivyo hilo ndio vazi la utu wetu wa ndani..Na ndio Vazi la harusi Bwana Yesu alilolizungumzia katika..

Mathayo 22:11 “Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa VAZI LA ARUSI.

12 Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa.

13 Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache”.

Maana yake hakuna mtu atakayeingia katika karamu ya Mwana-kondoo mbinguni kama hana hilo vazi la harusi ambalo ni UTAKATIFU

Biblia inazidi kulisisitiza hilo katika kitabu cha Waebrania..

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;”

Unaona? Anasema “huo utakatifu”..maana yake “Hilo vazi”..pasipo kuwa nalo hakuna mtu atakayemwona Mungu.

Tunaishi kizazi ambacho watu wanasema hakuna watakatifu duniani…Na hiyo ni kutokana na watu kutoelewa nini maana ya utakatifu…utakatifu maana yake sio kujizuia kukanyaga sisimizi barabarani, au kujizuia kutokuchinja kuku…Hiyo sio maana ya utakatifu…Maana kwa viwango hivyo basi kusingekuwa na mtakatifu duniani….(Ukipenda kufahamu kwa urefu maana ya utakatifu fuatilia somo tuliloliandika kipindi cha nyuma kidogo lenye kichwa kinachosema ‘mtakatifu ni nani’ au kama itakuwa ngumu kulifikia unaweza kututumia ujumbe inbox tutakutumia).

Hivyo Nyakati hizi za mwisho wako wasiojua maana ya utakatifu na kadhalika wapo shetani aliowafumba macho wakidhani wao ni watakatifu na kumbe sio…wakidhani kuwa wana VAZI HILO LA HARUSI…kumbe hawana…wapo uchi..kama Bwana Yesu alivyosema katika ufunuo 3.

Ufunuo 3:16 “Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, NA UCHI.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, NA MAVAZI MEUPE UPATE KUVAA, AIBU YA UCHI WAKO ISIONEKANE, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona”.

Je unataka unayataka mavazi hayo uyavae na uchi wako usionekane?…Hatua za awali za kufanya ni kutubu na kumkaribisha Bwana Yesu moyoni mwako…Unatubu kwa kudhamiria kabisa kuacha ulimwengu na mambo yake yote…Unakusudia kuacha ulevi, uasherati, wizi, rushwa, anasa, utoaji mimba, usagaji, ufiraji, ulawiti, utoaji mimba, utazamaji picha na video za ngono, na mambo mengine yote ya kidunia..Na kisha ndio unamwambia Bwana akusamehe kabisa na Bwana Yesu atakusamehe kwasababu anatamani wewe utubu kuliko wewe unavyotamani…Na kama leo hii umeamua kufanya hivyo kwa kumaanisha kabisa…

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, .

NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani … Hatua inayofuata ni Ubatizo, na kudumu katika Kujifunza Neno la Mungu..… VAZI HILO UTAKUWA UMEVIKWA katika roho yako…..Hivyo unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu Hiyo itakusaidia kuliweka safi vazi lako kila siku…. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Kumbuka haya maneno ya Bwana Yesu kila siku.. “Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)”

Huu ni wakati wa kumalizia, hatuna muda mwingi..

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Kwanini yule mtu hakukutwa na vazi la arusi wakati alialikwa?

WANA WA MUNGU, NA BINTI ZA WANADAMU.

USIMPE NGUVU SHETANI.

Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?

NINI KINAFUATA SIKU ILE ILE YA KUOKOKA!

HAKIKISHA UNALIELEWA NENO.

Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Suitbert
Suitbert
4 years ago

Nimebarikiwa kwa midomo haya