Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?

Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?

SWALI: Shalom Naomba kuuliza Je, ni halali kwa mimi kumuoa binti ambaye alishazaa na mtu mwingine bila kuishi nae Je, naweza kufunga naye ndoa ya kikristo na ikawa halali?


JIBU: Hapo yapo mambo mawili. Ikiwa binti huyo alikuwa ameshaolewa, halafu akaachika kwa sababu yoyote ile, labda pengine amekosana na mume wake, au amefumaniwa katika uzinifu na hivyo ameachwa, au sababu nyingine yoyote tofauti na kifo cha mumewe tu! Au kwasababu ya kufukuzwa kwa ukristo wake..Mtu huyu hapaswa kuolewa na mwanamume yeyote Yule.. Maana akifanya hivyo biblia inasema anazidi, na Yule pia aliyemuoa biblia inasema naye pia azini.

Marko 10:11 “Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;

12 na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini”.

Luka 16:18 Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.

Hivyo ili uwe katika mkono salama, usiangukie hukumu, ikiwa umegundua mwanamke huyo yupo katika hali hiyo unapaswa umuache mara moja..hata kama ulishazaa naye watoto.

Lakini kama mwanamke huyo, alipata tu mimba akiwa katika dhambi, kwa uasherati,  Hivyo na baadaye akaja akatubu na kumgeukie Mungu wake. Na sasa anataka kwenda kuolewa  basi hapo ni uchaguzi wako mwenyewe wewe unayetaka kuoa, ukiridhia kuwa naye  katika hali hiyo akiwa na watoto, ni sawa hakuna shida yeyote ukimuoa, kwasababu hapo mwanzo alikuwa hajaolewa. Lakini kama hajaridhia hafanyi dhambi pia kutokumuoa, ukitafuata ambaye hana watoto.

Na hiyo inalenga pande zote mbili, hata na kwa mwanaume pia..Ikiwa ameacha ndoa yake akaenda kuoa tena, biblia inasema azini, na Yule aliyeolewa naye vilevile azini..Lakini kama alikuwa hajaoa, lakini kazaa katika uzinzi na sasa amemgeukia Mungu katubu na amekuwa mkristo, anaweza akaoa, na isiwe anafanya dhambi mbele za Mungu.

Hizi ndio sababu pekee zinazoweza kumfanya mtu iwe halali kwake kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto.

Ubarikiwe.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

NDOA NA HARUSI TAKATIFU.

Je! ni halali kutoa cheti kwa wakristo wanaooa?

NDOA NA TALAKA:

Yeshuruni ni nani katika biblia?

Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments