Shalom, Ni siku nyingine Bwana ametupa kuiona kwa neema zake, hivyo nakukaribisha tuzidi kuyatafakari maneno ya uzima..
Leo tutajifunza juu ya wazazi wa mitume wawili wa Yesu, (Yohana na Yakobo)..Na tutaona pia ni jinsi gani wazazi wanavyoweza kuyaathiri maisha ya watoto wao ya rohoni kwa kiasi kikubwa. Kama tulivyotangulia kuona katika masomo yaliyopita, kwamba mzazi akimlea mtoto wake, na kumfundisha kumuheshimu, Basi Mungu anaamvika kilemba cha neema kichwani pake. Na neema hiyo si nyingine Zaidi ya ile ya kumjua Kristo kwa mapana yake na marefu yake(Mithali 1:8-9) na kuja kuwa msaada kwa wengine.
Na tutaona pia mwitikio wa wazazi jinsi unavyopaswa uwe kwa watoto wao pale wanapochukua uamuzi wa kumfuata Yesu. Tutajifunza kwa kuziangalia tabia za wazazi wa Yohana na Yakobo. Lakini awali ya yote,nataka utafakari jambo hili, Ulishawahi kujiuliza kwanini miongoni wa wale mitume 12 ni watatu tu ndio waliokuwa karibu sana na Yesu?.
Na miongoni mwa hao watatu, wawili walikuwa ndugu, na huyo mwingine ni Petro. Na mtume ambaye alipendwa na Yesu kuliko wote, ambaye kila wakati alikuwa akiegema kifuani mwa Yesu alikuwa ni mmojawapo wa hao wawili..Ni kwanini? Je! Mitume wengine walikuwa na mapungufu mengi? Jibu ni Hapana…Lakini kwanini Yesu aliwapenda hao wawili mpaka akawapa jina lao spesheli, akawaitwa Boanerge yaani wana wa ngurumo..(Soma Marko 3:17).
Yote hayo si kwa bidii zao tu peke yake lakini pia juhudi za wazazi zilichangia,..Embu tuwatazame kwa ufupi wazazi hawa tukianzana na Baba yao..tusome.
Mathayo 4:18 “Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. 19 Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. 20 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. 21 Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita. 22 Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata”.
Mathayo 4:18 “Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.
19 Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.
20 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
21 Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita.
22 Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata”.
Mwanzoni kabisa mwa wito, Yesu alipowaona vijana hawa wawili kuwa wanamfaa kwa kazi yake ya utume..Moja kwa moja alikwenda na kuwaita wakiwa katikati ya baba yao..katikati ya biashara ya baba yao waliyokuwa wanaifanya..Lakini Utaona baba yao hakuleta ukinzani wowote katika jambo hilo,..Aliwaachilia Watoto wake waende kwa moyo wote, afadhali ingekuwa ni mmoja, bali aliwaacha wote wawili wamfuate Yesu..
Jambo ambalo, si rahisi kwa mzazi yeyote wa kawaida wa leo kufanya hivyo, kuwaachilia Watoto wake wamtumikie Kristo,..Lakini kwake ilikuwa tofuati hakuona shida aachiwe vyombo vyake vya kazi, aitende kazi ile peke yake,pamoja na watu wa mshahara na uzee wake ilimradi tu wanawe waupate wokovu..
Tukimwangalia mama tena..
Mathayo 20:20 “Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno. 21 Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako. 22 Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza. 23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.
Mathayo 20:20 “Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.
21 Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.
22 Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza.
23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.
Embu jaribu kutafari mama huyu alivyokuwa anawatakia mema Watoto wake, aliona kufuatana na Yesu tu haitoshi hapa duniani haitoshi, bali pia wawe karibu na Yesu hata katika huo ulimwengu unaokuja. Alikuwa anawatafutia tu fursa nzuri Watoto wake huko mbeleni.. Wewe unadhani Watoto hao..wataachaje kupendwa na YESU, na kuwa vinara kwa Kristo. Kwasababu hawamtumikii Kristo kwa presha, bali kwa sapoti yote kutoka hata kwa wazazi wao.
Unadhani, wazazi wa mitume wengine walikuwa hawajui kuwa Watoto wao wanatumika na Bwana?. Walikuwa wanajua sana, lakini hakuna hata mmoja mzazi wake anaorodheshwa katika huduma za Yesu isipokuwa wazazi wa hawa vijana wawili.
Pengine walikuwa hawaoni umuhimu wowote, wa wao kuongozana na Yesu..Wameacha shughuli zao, fedha zao, biashara zao, ya nini tena kuwasapoti..hawakuwa na muda..Lakini wazazi wa mitume hawa wawili walikuwa bega kwa bega na Watoto wao, hadi hatua ya mwisho kuhakikisha kuwa hawamkosi Yesu..Na mwishowe wakawa miongoni mwa wale watatu waliopendwa na Yesu.
Hata leo hii, ikiwa wewe ni mzazi, au unajiandaa kuwa mzazi..Utakapomwona mtoto wako anaonyesha uelekeo wa kumpenda Mungu, unapaswa uwe wa kwanza kumsapoti. Kama unaweza kuwa wa kwanza kumsapoti kumnunulia kitabu cha shuleni, kwanini usimsapoti kumnunulia biblia, na vitabu vyenye mafundisho ya Neno la Mungu. Kwanini usimweke chini wa wachungaji wako wamfundishe Neno la Mungu?..Unajuaje kuwa kwa bidii yako hiyo utamkuza Samweli, au Yakobo, au Yohana?.
Bwana atusaidie tunapojifunza mifano ya wazazi hawa ili na sisi tuwe na mioyo kama hiyo hiyo kwa Watoto wetu.
Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
KUTOKUIHUBIRI INJILI,KUNA MADHARA GANI?
Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?
Je! ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku yake ya kuzaliwa.[Birth day]?
Rudi Nyumbani:
Print this post