LAKINI HAITAKUWA HIVYO KWENU.

LAKINI HAITAKUWA HIVYO KWENU.

Lakini haitakuwa hivyo kwenu.


Shalom, Karibu tuzidi tujifunze Neno la Mungu.

Mathayo 20: 24 “Na wale kumi waliposikia, waliwakasirikia wale ndugu wawili.

25 Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.

26 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu;

27 na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;

28 kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”.

Jinsi dunia inavyoenenda ni tofauti kabisa na wakristo wanavyopaswa kuenenda…Kama Bwana Yesu alivyosema hapo juu, watu wa mataifa huwatawala kwa nguvu na mkubwa wao huwatumikisha…lakini haitakuwa hivyo kwenu..Ikifunua kuwa hekima ya dunia hii ni kinyume na hekima ya Mungu…Hekima ya dunia hii, mdogo anamtumikia Mkubwa…lakini Hekima ya kimbinguni mkubwa ndiye anayemtumikia mdogo….

Hekima ya kidunia inasema ukimbilie ukubwa ili usiwe mtumwa…lakini hekima ya kimbinguni inasema ukimbilie udogo ili uwe mkubwa…

Hekima tena ya kidunia inasema…Mpende akupendaye na umchukie anayekuchukia…lakini hekima ya kimbinguni inasema “mpende adui yako mwombee yeye anayekuudhi”..adui yako akiwa na njaa mlishe, akiwa na kiu mnyweshe…(Soma Mathayo 5:44 na Warumi 12:20).

Hekima ya dunia hii inasema ukiipatia nafsi yako kila kitu chema cha ulimwengu huu ndio maana ya maisha…lakini hekima ya Mungu inasema “aipataye nafsi yake ataipoteza na aipotezaye kwa ajili ya Kristo ataipata”…Kwahiyo karibia mambo yote ya ulimwengu yanakwenda kinyume na hekima ya Mungu…Ndio maana inakuwa ni ngumu mtu wa kidunia kumwambia kwamba kuna siku hii dunia tunayoishi itafikia mwisho na kwamba mwisho huo umekaribia sana na siku moja hili jua tunaloliona litatiwa giza…atakuona ni mtu wa ajabu kwasababu yeye anaona dunia mbona bado ni mahali salama?..itawezekanikaje jambo hilo..kwamba eti siku moja jua litiwe giza?..Atakuona kuna kau-pumbavu Fulani kapo kichwani mwako..

Ndio maana biblia ikasema…

katika 1 Wakorintho 1:18 “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

19 Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa.

20 Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?

21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa.”

Unaona?..Hebu leo hii itafute hii hekima ya Mungu..ambayo imekataliwa na watu wengi…kama wewe ni mkristo na ulikuwa hujui kwamba unapaswa uwapende wanaokuchukia anza kufanya hivyo leo…Usiisikilize hekima ya dunia ambayo kwa nje inaonekana ni tamu, lakini mwisho wake ni upotevu…inayokuambia usimwache adui yako kuishi…na mbaya Zaidi hekima hiyo ya kidunia imeshaanza kuhubiriwa hata mpaka makanisani kana kwamba ni hekima ya ki-Mungu.

Kama ulikuwa hujui kwamba ili uwe mkubwa kuliko wote ni sharti uwe mdogo kuliko wote..anza kufanya hivyo leo…Kama wewe ni boss mahali ulipo tumika kana kwamba wewe sio boss tumika kuliko hata wale uliowaajiri…kuwa mpole kuliko yule mfanyakazi wa chini kabisa uliomwajiri…Ndivyo mbele za Mungu utakavyoonekana Mkubwa…Na ndivyo Mungu atakavyozidi kukupandisha juu. Mungu anasema Musa alikuwa ni mtu aliyekuwa mpole kuliko wote ulimwenguni, lakini kwa kupitia upole wake Mungu alimfanya kuwa kichwa cha wana wa Israeli.(Hesabu 12:3).

Bwana Yesu alikuwa ni mkubwa kuliko wote lakini aliwaosha miguu wanafunzi wake ambao wengine hata walimsaliti na kumkana..Na pamoja na kujua kuwa atasalitiwa na kukanwa lakini aliwaosha miguu hivyo hivyo na kuendelea kula nao na kunywa nao kwa upendo wote…Je wewe unaweza kufanya hivyo kwa watu waliopo chini yako?..ambao unajua kabisa wamekufanyia hiki au kile?..Kama huwezi basi tambua una hekima ya ulimwengu huu lakini hauna hekima ya ki-Mungu.

Na mambo mengine yote ni vivyo hivyo..Hekima hii inaingia ndani ya mtu kwa kujifunza Neno la Mungu…kuna tofauti kati ya kusoma na kujifunza…

Kujifunza Maana yake unajiingiza mwenyewe kwenye darasa ambalo utausoma mstari na kuutafakari kwa kina na kwa msaada wa Roho kupata ufunuo kutoka katika huo mstari..Na hauhusomi wakati kichwa chako kimevurugika na mambo mengine ya ulimwengu…hakikisha unapata utulivu wa kutosha…katika hali ya utulivu ndipo sauti ya Mungu inasikika..Roho Mtakatifu ataanza kukufundisha jambo moja baada ya lingine..na utaona mwenyewe kwa jinsi gani dunia ipo mbali na hekima ya Mungu…na hata wewe binafsi ulivyokuwa mbali na hekima ya Mungu.

Vilevile kama tutaipuuzia hii hekima ya Mungu na kujiona tunajua Zaidi ya Neno lake..Basi tufahamu kuwa Hekima hiyo mbele za Mungu ni upuuzi..

1Wakorintho 3:18 Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.

19 Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.

3.20 Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili.

Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

MAOMBI KWA WENYE MAMLAKA.

JE SALA YA ROZARI TAKATIFU NI YA KIMAANDIKO?

Kwanini yule mtu hakukutwa na vazi la arusi wakati alialikwa?

KUVUNJA MAAGANO YA UKOO.

Je ni wakina nani ambao hawataonja mauti mpaka siku ya kuja Bwana?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments