KUVUNJA MAAGANO YA UKOO.

KUVUNJA MAAGANO YA UKOO.

Unatafuta kujua namna ya kuvunja maagano ya ukoo?. Upo sehemu sahihi fuatilia somo hili hadi mwisho kabisa utafahamu njia rahisi ya kuondokana na hizo laana milele zisikurudie tena.

Biblia inasema:

Yohana 8:36  “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”

Unaweza ukajiuliza ni kwanini pale msalabani Bwana Yesu alisema neno moja tu IMEKWISHA!!(Yohana 19:30), Na sio YAMEKWISHA?…Ukilifahamu hilo utajua ndio sababu kwanini huwezi kuona maneno kama laana za ukoo, laana za kifamilia, laana za mababu, laana za mapepo, kifungo vya kikabila n.k katika biblia..kwasababu hayo yote yamejumuishwa katika hicho kitu kimoja kilichokwisha pale msalabani  nacho si kingine Zaidi ya DHAMBI.

Dhambi ndio mzizi wa matatizo imefananishwa na  ugonjwa wa ukimwi, Ambao vijidudu vyake vinafanya kazi  moja tu nayo ni kwenda kushambulia kinga ya mwili  basi, havileti madhara mengine yoyote mwilini, havisababishi kutokwa na vidondo, havisababishi kutapika, havisababisha kuugua, havisababishi kukohoa La!..Lakini vinaua kinga ya mwili, sasa ile kinga ikishakufa, ina maana kuwa mwili hauna ulinzi tena, hapo ndipo kila aina ya ugonjwa unapata nafasi ya kuingia, mara malaria, mara Tb, mara mkanda wa jeshi, mara homa ya ini n.k. n.k. Na hivyo ndivyo mwisho wa siku vinakwenda kummaliza mtu…

Ogopa sana ugonjwa  mmoja  unaokwenda kushambulia kinga ya mwili kuliko magonjwa 99 yanayokwenda kushambulia sehemu nyingine zote mwilini.

Sasa dhambi na yenyewe ndio inafanya kazi hiyo hiyo, Adamu na Hawa walipoasi pale Edeni, dhambi iliingia ndani yao, ikamaliza kinga yao yote ya ulinzi Mungu aliokuwa amewawekea pale Edeni, Na ghafla uuaji ukaingia, dhuluma ikaingia, magonjwa yakaanza, uchawi ukaanza, laana zikaingia, vita vikaingia, matabaka na matambiko yakajitokeza ndio maagano zote za ukoo zikatokea huko huko n.k. Na hili likawa ni tatizo lisilokuwa na tiba kwa vizazi na vizazi, kwa karne na karne..Dawa ya dhambi haikupatika kama vile dawa ya ukimwi usivyopatikana leo, kwa Zaidi ya maelfu ya miaka.

Lakini Bwana Yesu alipokuja miaka karibia 2000 iliyopita hakuja kushughulika na tawi Moja la dhambi labda tuseme maagano ya ukoo, au laana za kifamilia, hapana angefanya hivyo basi tatizo lote lisingeondoka, lakini alikuja kuung’oa mzizi wote wa DHAMBI, kiasi kwamba mfano mtu aking’olewa mzizi huo ndani yake basi hakuna vimelea vyovyote vya laana yoyote ile itakayomwandama.

Jambo ambalo watu wengi hawafahamu, ni kuwa wanadhani kwenda kuombewa au kufanyiwa maombi fulani ya muda mrefu labda tuseme ya kufunga, na kukaa milimani na kutumia masaa mengi kuomba na kukemea ndio kunaondoa laana na maagano ya ukoo au maagano ya kifamilia, wengine wanadhani kutoa sadaka fulani maalumu ndio kunaondoa maagano ya kiukoo hapana, mtu anaweza akafanya hivyo na bado hayo mambo yasiondoke ndani yake, kama ikiwa bado yupo nje ya wokovu.

Kama mtu hajakusudia kweli kuokoka, mambo hayo hayawezi kuondoka hata iweje, yataendelea kumfuata tu, lakini kama leo hii ukasema mimi na dhambi basi, nimeamua kujitwika msalaba wangu na kumfuata YESU popote atakapotaka mimi niende, sirudi nyuma tena, ukatubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako zote, kisha ukatii agizo la Ubatizo, ukaenda kubatizwa katika ubatizo wa kuzamishwa kwenye maji mengi, na Kwa jina la Yesu Kristo sawasawa na Matendo 2:38, ili upate ondoleo la dhambi zako, na kuanzia huo wakati ukawa unaishi Maisha ya kama mkristo aliyeokoka, nataka nikuambie, sio tu maagano ya ukoo yatafutwa juu yako, bali pia hata na yale maagano mengine usiyoyajua ya kipepo yaliyokuwa juu yako yote hayo yatafutwa..

Usihangaike kwenda kuombewa huku na kule, ukifika kule kila mmoja atakuambia hichi, mwingine kile. Kumbuka Wokovu ni muujiza mkubwa sana ambao unatokana na neema ya Kristo tunaoupata bure bila kujisumbua wala kugharamia chochote, wewe ni kutii tu, hivyo pale ulipotubu basi jua vyote vimefutika,..Lakini kitu shetani anachokifanya ni kukutisha, kukufanya ujione kuwa bado upo chini ya maagano hayo, atakuletea hichi na kile, hapo unapaswa usimsikilize wewe sema tu maneno haya..

Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”

Atafanya hivyo kwa muda tu, lakini kwa jinsi unavyozidi kujifunza maneno ya Mungu na biblia, kwa bidii Zaidi ndivyo utakavyomfanya aende mbali na wewe Zaidi na mwishoni asikusumbue kabisa, kwasababu shetani huwa anamsumbua mtu na kumletea vitisho kutokana na ujinga wake, kutokana na uzembe wake wa kutokuzingatia kujifunza maandiko,..hivyo unapaswa ujifunze sana maandiko ili uweze kumshinda atakapokuletea majaribu yake.. Na ndio maana biblia inasema.

Yohana 8:32  “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”.

Na “KWELI” ni Neno la Mungu biblia inasema hivyo katika (Yohana 17:17)..Hivyo ukiwa ni mtu wa kujifunza na kuyatafakari Maneno ya Mungu kwa bidii shetani atakaa mbali na wewe sikuzote. Hiyo ndio njia pekee ya kuvunja maagano ya ukoo, ukiipata hiyo huhitaji kwenda kuombewa, wala kufanyiwa maombi yoyote ya ukombozi, lakini kama Maisha yako ya wokovu yapo mbali na Kristo halafu unatafuta njia mbadala ya kuondoa tatizo hilo, kumbuka hayo mambo yalishafanyika zamani sana, na yakashindikana..Hivyo na wewe pia usijaribu kuyarudia hayo..bali Mkaribishe leo YESU maishani mwako, awezaye kuondoa mzizi wote wa dhambi na laana zake zote. Na kukufanya kuwa kiumbe kipya. Na hakika atayavunja maagano yote ya ukoo, babu zako, na mababu zako waliyoingia na kuapa iwe ni katika afya, au mafanikio, au furaha vyovyote vile vitakwisha ndani yako.

Ubarikiwe sana.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Kwanini kuna watu wanafanyiwa deliverance (Maombi ya kufunguliwa), lakini baada ya muda wanarudiwa tena na hali ile ile sababu ni nini?

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

IPO NGUVU ITUVUTAYO KWA KRISTO, ITHAMINI!.

KWANINI MOTO NA UPEPO VINAWAKILISHA TABIA ZA MUNGU?

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
7 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kevin
Kevin
1 year ago

How can i deal with the SPIRIT OF BACKSLIDING?

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Nataka kufaham biblia lakin najikuta nasoma tu wakt mwingne kama kitabu kawaida lakin pia uvivu

Armon
Armon
2 years ago

I want to succeed in my education level and become an Engeneer so that I can help my parents in their oldest time please I ask you consider my prayers into yours while praying

Mario DonBosco Moshi
Mario DonBosco Moshi
2 years ago

Mahubiri mazuri sana