Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?

Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?

SWALI: Naomba kufahamu Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena, tunaopaswa tuwe nao ni ule wa Roho Mtakatifu tu peke yake kama vile Yohana Mbatizaji alivyosema katika Mathayo 3:11 “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto”?


JIBU: Katika mistari hiyo hakuna mahali popote Yohana amesema sasa ndio watu waache ubatizo wa maji, wautazame ule wa Roho Mtakatifu peke yake..Hakuna na Hiyo yote ni kutokana na utafsiri mbaya wa maandiko ambao unasababishwa na baadhi ya waalimu ambao hawamtegemei Roho Mtakatifu katika kuyatafsiri maandiko.

Embu leo tuangalie mtu mmoja katika biblia ambaye alilielewa hilo andiko na akachukua hatua stahiki katika kuwaelekeza watu katika njia ya kweli.

Kama tukisoma kitabu cha Matendo sura ile ya 10 kwa ufupi pale tunaona habari ya mtu mmoja aliyeitwa Kornelio, ambaye alikuwa anamcha Mungu sana kwa sadaka zake, lakini siku moja akatokewa na malaika na kupewa maagizo ya kwenda kumuita Petro aje kuwaelekeza cha kufanya.. Ndipo Petro alipoeletewa taarifa akaenda na alipowakuta akaanza kuwaeleza habari za Yesu, pindi tu anaanza kuwaeleza habari zile Roho Mtakatifu alishuka palepale, na watu wote wakajazwa na Roho Mtakatifu wakaanza kunena kwa lugha mpya.

Matendo 10:44 “Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.

45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.

46 Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu,

47 Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?

48 Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.

Sasa utaona hapo mara baada ya Petro kuona watu wamejazwa Roho Mtakatifu hakusema yatosha sasa, hakuna haja ya kubatizwa tena, Roho Mtakatifu anatosha kwasababu Yohana alisema hivyo…

Ukitaka kujua kuwa Petro naye aliufahamu huo mstari vizuri hata Zaidi yetu sisi, aliukumbuka pia hata alipokuwa palepale anawahubiria, Tunalithibitisha hilo mbele kidogo wakati sasa amesharudi Yerusalemu anawasimulia wayahudi tendo hilo la watu wa mataifa kupokea Roho Mtakatifu kama wao aliwaeleza mstari huo embu tusome alichokisema..

Matendo 11:15 “Ikawa nilipoanza kunena Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.

16 Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, YOHANA ALIBATIZA KWA MAJI KWELI, BALI NINYI MTABATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU.

17 Basi ikiwa Mwenyezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu?.

Unaona hapo?, Petro alilielewa hilo andiko kuwa hatupaswi kuuacha ubatizo wa maji, na ndio maana hata baada ya kuona Roho Mtakatifu alishuka juu yao kabla ya ubatizo bado aliagiza wakabatizwe. Hivyo na sisi pia agizo la ubatizo ni moja ya maagizo muhimu sana Bwana Yesu aliyotupa yanayoukamilisha wokovu wetu. Kila mtu aliyeamini hana budi kwenda kubatizwa haraka sana iwezekanavyo..Kama Bwana Yesu alivyosema..katika Marko 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.

Na tena katika ubatizo ulio sahihi wa mitume ambao ni ule wa kuzamishwa katika maji mengi (Yohana 3:23). na kwa jina la YESU KRISTO (Matendo 2:38, 8:16, 10:48, 19:5)..Ubatizo mwingine tofauti na huo ni batili. Mtu anapaswa akabatizwe tena.

Ubarikiwe.

Maran atha

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

MTUMAINIE YESU ASIYEISHA MATUKIO.

KWANINI AWE PUNDA NA SI MNYAMA MWINGINE?

WAKAMTUKANA MUNGU, WALA HAWAKUTUBU.

ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI?

NGUVU ILIYOPO KATIKA MAAMUZI.

UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.

KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments