Biblia imemaanisha nini kusema Nyoka atakula mavumbi?

Biblia imemaanisha nini kusema Nyoka atakula mavumbi?

Naomba ufafanuzi wa mwanzo 3:14..kwamba hivi laana iliyotamkwa pale na Mungu kwamba nyoka atakula mavumbi…..hivi ni kweli nyoka anakula mavumbi leo?.


Jibu: Jibu ni la! Nyoka hali mavumbi leo na hakuwahi kula mavumbi kabla, na hakuna kiumbe hai cha Mungu chochote kinachokula mavumbi, kwasababu mavumbi si chakula.

Lakini kwanini biblia iseme Nyoka atakula mavumbi,

Labda tusome mistari hiyo, ili tuweze kuelewa kidogo..

Mwanzo 3:14 “BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako”

Hapo utaona matokeo ya Nyoka kuambiwa atatembea kwa tumbo ni kula Mavumbi.

Maana yake hapo kwanza alikuwa hatembei kwa tumbo, hivyo alikuwa hali mavumbi.

Maana yake sababu nyoka kula mavumbi ni kwasababu anatembea kwa tumbo.

Sasa anakulaje mavumbi? Hali kama chakula kwasababu vumbi haliwezi kuwa chakula, bali katika ile hali nyoka waliyopo ya kutembea kwa tumbo, maana yake nyuso zao, pua zao, na macho yao yapo katika usawa wa ardhi, hivyo kitendo cha kuchafuka kwa mavumbi wakati wanatembea kwa tumbo ni sawa na kula mavumbi, kwasababu kimo cha mdomo kipo karibu na usawa wa ardhi, tofauti na wakati hajalaaniwa.

Hebu wewe tengeneza picha sasahivi unaambiwa utambae kwa tumbo umbali wa kilometa moja, hebu jiulize safari yako mpaka iishe utakuwa umekula vumbi kiasi gani?. Ndivyo ilivyokuwa kwa Nyoka.

Hapo kwanza kabla Nyoka hajalaaniwa, alikuwa hatembei kwa tumbo hivyo alikuwa hali mavumbi, ni viumbe wengine tu wanaotambaa ndio waliokuwa wanakula mavumbi, kama mijusi, kenge n.k hivyo Nyoka naye akawa kama hao..

Utauliza ni wapi katika maandiko panaonyesha kuwa kuna viumbe wengine wanaokula mavumbi tofauti na nyoka.

Mika 7:17 “Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako”.

Lakini ni somo gani tunalipata kwa Nyoka kutembea kwa matumbo na kula mavumbi?.

Umeona?..sio Nyoka peke yake anayelamba mavumbi.

Somo kuu tunaloweza kulipata ni kwamba tunapoasi na kujitenga na Mungu, basi tunajipeleka wenyewe mavumbini, kiroho na kimwili, Nyoka alikuwa hatembei kwa matumbo lakini akajikuta anatembea kwa matumbo na kuyalamba mavumbi ya nchi.

Lakini habari nzuri ni kwamba tunapotubu, Bwana anatutoa mavumbini, na kutupandisha juu.

1 Samweli 2:8 “Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu,
Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu, Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake”

Inawezekana leo upo mavumbini, na unakula mavumbi pasipo kujijua.

Tubu leo, mpokee Yesu naye atakupa uzima wa milele, na kukutoa mavumbini kiroho na kimwili.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

NJIA YA KUPATA WOKOVU.

Je! Shetani alitolea wapi uovu?

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.

DALILI NYINGINE INAYOUTAMBULISHA UZAO WA NYOKA

UWEZO WA KIPEKEE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments