TAFUTA KUWA NA AMANI NA WATU WOTE.

TAFUTA KUWA NA AMANI NA WATU WOTE.

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”.

Ni agizo la Mungu kwamba tuwe na amani na watu wote..Ukijiona una shari na mtu au watu basi kuna tatizo mahali…Sio kila jambo ni la kupambana nalo, na njia ya kupambana na moto ni kuuzima na si kujitosa ndani ya moto. Hivyo tunapoudhiwa si wakati wa sisi kulipiza kisasi, ni wakati wa kuyazima hayo maudhi, kwa hekima na upole.Na mara nyingi kitu kinachowasha moto katika miasha yetu ni ULIMI.

Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.

6 Nao ULIMI NI MOTO; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum”

Unaona hapo? Biblia inasema pia ukiweza kuuzuia ulimi wako hata SIKU YAKO ITAKUWA NJEMA…na ndivyo utakavyopata amani..

1Petro 3:10 “Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.

11 Na aache mabaya, atende mema; ATAFUTE AMANI, aifuate sana”

Hivyo mara zote tukijifunza kukaa kimya na kuwa wapole na wenye busara…basi ni lazima tu tutakuwa na amani na watu wote….Sisemi kwamba hautakuwa na watu wanaokuchukia kabisa,…hapana watu wanaokuchukia watakuwepo tu! lakini hawatakuwa na la kufanya kwako kwasababu muda wote watakuona ni mtu wa amani. Watatafuta maneno kwako lakini hawatayapata…hivyo mwisho wa siku wataachana na wewe, na kuendelea kufikiri mambo yao mengine.

Lakini ukiwa ni mtu wa kujibiza, kamwe vita kwako havitaisha..na hakuna siku utapata amani…kama mtu akikuudhi wewe nawe unajibu mashambulizi kwa kumrudishia maneno…nataka nikuambia hakuna siku utakuwa na amani, utakuwa ni mtu wa kugombana tu kila siku, na wa kukosa raha, na muda mwingine kuweka vinyongo tu…na pasipo kujua kuwa tatizo kubwa lipo upande wako.

Mithali 15:1 “Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu”.

Kila mahali jaribu kuwa mpole…hiyo ndiyo njia ya kupata Amani na watu wote…Na kuwa mpole sio “udhaifu”….Bwana wetu Yesu alikuwa ni mpole(Mathayo 11:28) na mtu mpole mara nyingi sio mtu wa kuzungumza sana, na sio mtu wa kuzungumza mambo ya wengine (msengenyaji).

Wafilipi 4:5 “Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu”.

Sisi kama wakristo tukiudhiwa kwa maneno sio lazima tujibu neno,.. ukiumizwa hupaswi na wewe kumuumiza..kila wakati tafuta namna ya kulitatua tatizo badala ya kulichochea…na kwa jinsi utakavyoonesha bidii ndivyo Mungu atakavyozidi kukupatanisha na wale ambao wanaonekana ni maadui zako wa kudumu..Na hivyo utazidi kuwa na amani.

Mithali 16:7 “Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye”.

Hivyo Bwana anavyotuambia tutafute kwa bidii (maana yake tufanye kila tuwezalo) tuwe na amani na kila mtu, kama vile tunavyofanya bidii kuutafuta utakatifu ambao hakuna atakayemwona Mungu asipokuwa nao.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

KAMA UNAPENDA MAISHA, NA KUTAKA SIKU YAKO IWE NJEMA.

NI NINI TUNAJIFUNZA JUU YA MT. DENIS WA UFARANSA?

Mtu astahiliye hofu ni yupi?

FAHAMU ZA WATU HUWA ZINAONDOLEWA NA NINI?

DANIELI: Mlango wa 9

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

Kwanini biblia inasema mtu wa rohoni huyatambua yote?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
DEBORA ANDREW
DEBORA ANDREW
2 years ago

Amen, Mungu akubariki sana

Gloria
Gloria
3 years ago

Mafundisho ni mazuri sana Mungu awabariki kwa kazi njema mnayoifanya.