Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze Neno la Mungu.
Kama
wengi wetu tunavyojua kuwa hakuna wokovu nje ya Yesu Kristo, wala
hakuna Maisha nje ya Yesu Kristo. Kama Mtume Paulo alivyoandika kwa
uweza wa Roho kwamba ‘Mauti ilikuja kwa njia ya mtu
mmoja(Adamu)…kadhalika uzima utaletwa kwa njia hiyo hiyo ya mtu mmoja
(ambaye ni Kristo)’.
Kwahiyo
yeye peke yake ndio njia iliyo sahihi na iliyothibitishwa ya kumfikia
Mungu..njia nyingine zote tofauti na yeye ni za upotevu, haijalishi zina
wafuasi wengi kiasi gani.
Bwana
Yesu alipokuwa hapa duniani, alizungumza kwa mifano mingi, yote ni kwa
lengo la kumfanya mwanadamu aelewe mpango wa Mungu juu ya Maisha
yake…Alitumia mifano ya miti, mashamba, wafanyabiashara,
wakulima,familia, wageni, wafalme na mingine mingi ambayo hata
haijaandikwa kwenye biblia, kwasababu kama yangeandikwa mambo yote
aliyoyafanya moja moja…biblia inasema hata dunia isingetosha kwa jinsi
vitabu vingekuwa ni vingi (Yohana 21:25)..
Lakini
tunaona baada ya kuondoka alikuja tena kuzungumza na Mtume Yohana
katika maono , alipokuwa katika kisiwa kile cha Patmo na kumpa mfano
namna ambayo huwa anavyowajilia watu wake alimwambia…
Ufunuo 3: 20 ‘’Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami’’.
Mfano
huo Bwana Yesu aliutoa kuonyesha ujio wake kwa mtu ni kama wa
mgeni…Ujio huu sio wa kulichukua kanisa…kwasababu ujio wa kuja
kulichukua kanisa alisema utakuwa kama ujio wa mwizi…hata kuja kwa
kugonga na kusihi, bali atakuja usiku watu wakiwa wamelala na atachukua
walio wake na kuondoka….ndio maana unyakuo ukipita sio watu wote
watajua…Kwahiyo kuna kipindi Bwana Yesu atakuja kama mgeni na kuna
kipindi atakuja kama mwivi.
Sasa
katika mfano huu..anasema tazama nasimama mlangoni nabisha! Kubisha
maana yake ni kugonga mlango huku unatoa sauti Fulani kama hodii hodii!!
Hiyo ndiyo maana ya kubisha!..Kwahiyo hapa Bwana anasema nasimama
nabisha, halafu anasema mtu akiisikia sauti yake na kuufungua mlango
ataingia…hii ikiwa na maana kuwa mtu anaweza akaisikia sauti yake na
asifungue…au mtu anaweza asiisikie kabisa sauti yake…labda kutokana na
kwamba amelala au kutokana na usumbufu uliopo ndani ya nyumba kuwa
mkubwa (labda kelele za miziki au watu).
Na
baada ya kuingia utaona anasema…’nitakula pamoja naye na yeye pamoja
nami’…sasa tafakari hapo kwa makini, hasemi tutakula pamoja
hapana!…bali anasema nitakula pamoja naye…na yeye pamoja nami…ikiwa na
maana kuwa alipokuwa anangonga alikuja na chakula chake, hakuja mikono
mitupu…kadhalika na yule mtu aliyemfungulia atamkuta na chakula chake…na
hivyo kila mmoja atashiriki na mwenzake kile alichokiandaa.
Sasa
ukiingia ndani Zaidi kuutafakari mfano huu utaona kuwa unahusu wakati
wa jioni…lugha yetu ya Kiswahili haijajitosheleza katika maneno
mengi…lakini kama ukisoma tafsiri nyingine kama zile za kiingereza au
kigiriki utaelewa vizuri kuwa ni wakati wa jioni ndio Bwana alikwenda
kugonga mlango.. ni wakati wa chakula cha jioni (evening supper).
Kwahiyo
katika mfano huo Bwana anakuja kugonga mlango wakati wa jioni…akiwa na
chakula chake, hajaja kudoea wala kula vya watu bure!…Inaashiria kuwa
Kristo anapotaka kuja kuingia katika Maisha yetu sio kwa lengo la kutaka
vya kwetu, au kutuharibia Maisha hapana! Bali ni kwa lengo la kutupa
sisi faida. Na atakuja jioni, hizi ni nyakati za jioni, wakati wa
kumalizia wa mwisho wa dunia ndugu.
Na kama tunavyojua tabia ya mgeni anapogonga, huwa hagongi mfululizo kama vile analazimisha mlango ufunguliwe…bali utaona anagonga kidogo kwa utaratibu kisha anatulia kidogo, akiona hasikiwi atarudia tena kwa sauti kidogo baada ya muda Fulani kupita..atafanya vile kwa kipindi Fulani, akiona hakuna kabisa majibu labda yule mtu amelala usingizi mzito hawezi kusikia hatavunja mlango ataondoka arudi tena baadaye au arudi wakati mwingine…Lakini akigundua yule mtu kule ndani anamsikia lakini hataki kumfungulia makusudi tu! Basi ataondoka asirudi tena…kwasababu anajua hahitajiki mahali pale.
Na
Ndivyo hivyo Kristo anavyogonga mioyoni mwetu leo hii, atakutumia
wahubiri pale mahali ulipo, kwa kukusihi umfungulie moyoni mwako
aingie…akiona bado humsikii ataongeza watumishi kila mahali
utakapokwenda hata kwenye mitandao utakutana na Neno lake, sauti yake
utaisikia kila mahali ikikuita, utakapoitii ataingia, na vitu alivyokuja
navyo kukuletea hutaamini macho yako kuvioona..Lakini endapo unajua
kabisa huyu ni Kristo ananiita kupitia mahubiri, na kuwa hii ni sauti
yake kabisa na unafanya makusudi kutokumfungulia…basi ataondoka na Neema
hiyo itakwenda kwa wengine..
Ndugu
usidanganyike kuwa utatubu uzeeni, Sauti ya Mungu itarudia kuita kwa
wale watu ambao wakati Bwana amegonga wapo usingizini…wale watu ambao
nguvu za giza zimewafunga kiasi kwamba hawawezi kuisikia injili…hao ndio
Bwana ataendelea kuwaita kila wanapokwenda, mpaka watakapoamka
usingizini, na kundi hili mara nyingi ni lile kundi ambalo halijawahi
kabisa kupata nafasi ya kuujua msingi wa Imani ya kikristo, wale watu
ambao wamezaliwa katika familia za kipagani, au familia za watu wasio wa
dini, na hawamjui Kabisa Kristo…hawa ni sawa wapo usingizini au wapo
kwenye makelele ya ulimwengu kiasi kwamba hawawezi kuisikia sauti ya
Bwana Yesu..Hivyo Bwana ataiongeza sauti yake mpaka wasikie.Watapata
Neema kubwa Zaidi.
Lakini
kwa wengine ambao wamezaliwa katika Ukristo tangu udogoni, wamehubiriwa
vya kutosha kuhusu msalaba, na wanaielewa kabisa sauti ya Yesu
inapoita, na wengine mpaka wamemwona Bwana katika maono, na wamepewa
ishara kadha wa kadha, Bwana akiwaita na hawataki kusikia…Kristo
ataondoka kwao na asirudi tena kamwe. Wengi hawapendi kusikia hivi
lakini huu ndio ukweli maandiko yanasema hivyo..Wana wa Israeli Taifa la
Mungu yaliwatokea hayo, si Zaidi watu wa mataifa.. Bwana Yesu
aliwaambia waisraeli maneno haya, baada ya kuwaonya mara nyingi na
kushupaza shingo zao haya ndio aliyowaambia:
Mathayo 23:37 ‘’Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!
38 Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.
39 Kwa maana nawaambia, HAMTANIONA KAMWE TANGU SASA, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana’’.
Aliwaambia
‘’hamtaniona kamwe tangu sasa’’..Hili Neno ni kali sana na
linaumiza…’’kutengwa na Mungu milele’’..Si ni afadhali tutengwe na
wanadamu kuliko Mungu…Ni heri wanadamu wote wanichukie na kunitenga
lakini sio Mungu, ni heri nichokwe na wanadamu wote lakini sio Mungu.
Hebu tafakari leo hii Kristo anakwambia haya maneno ‘HUTANIONA TENA KAMWE TANGU SASA’!!!…Yaani wewe na Kristo ndio Basii!!…
Leo
hii usikiapo maneno haya kwenye mtandao, na bado hutaki kuacha dhambi
na ulimwengu, kumbuka haukuwa mpango wa Mungu usikie injili yake kwa
njia hii ya mitandao..Mpango wake ulikuwa siku ile ile ulipoisikia
injili kwa mara ya kwanza ulipohubiriwa na mtu aliyeshika biblia mkononi
ungeamini, kulikuwa hakuna sababu ya wewe kuja kusikia tena injili
hapa……lakini kwasababu Moyo wako ulikuwa mgumu, ndio maana amekufuata
kwa njia nyingine hii ya mtandao..ili awe na uhakika kabisa unaisikia
sauti yake. Lakini unaidharau..pengine hii ndio sauti yake ya mwisho
kwako, isikie ufungue, asije akakwambia kama alivyowaambia wayahudi ‘HUTANIONA TENA KAMWE TANGU SASA’….Maneno
haya yalizungumzwa na Kristo yule yule aliyesema ‘njooni kwangu nyinyi
nyote’….hapa anasema ‘hamtaniona tena kamwe’…sehemu nyingine anasema
‘tokeni kwangu’.
Pale
ulipo mwambie Bwana natubu dhambi zangu zote, na kukusudia
kutokuzifanya tena, tubu kabisa kwa kudhamiria kabisa kuacha
kuzifanya.Mfungulie mlango na yeye ataingia ndani yako haraka kukugeuza,
hataanza kukulaumu kwanini nimegonga muda wote huo ukufungua, yeye si
kama sisi, moja kwa moja atazungumza na wewe na muda wa kula ukifika
atakufungulia hazina zake alizokuletea mshiriki pamoja, atakupa baraka
zote za mwilini na rohoni, na kukufundisha maneno yake ya uzima. Utakuwa
na tumaini la uzima wa sasa na ule wa baadaye.
Lakini usipotaka ataondoka, na siku moja atakuja kama mwivi, siku hiyo hatokuja kwako tu bali atakuja kwa ulimwengu mzima, atavunja atavunja mlango na kuwaiba waliowake ndani, na kwenda nao mbinguni, huku nyuma moto utawaka. Usitamani uwepo hicho kipindi cha dhiki kuu. FIKIA TOBA LEO!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789 001 312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Ni maombi yangu kuwa utakitendea kazi ulichokisikia. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!
USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.
UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?
JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.
Rudi Nyumbani
Print this post