Title May 2021

Je Musa yupo anawashitaki watu..kulingana na Yohana 5:45?

Tusome,

Yohana 5:45  “Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.

46  Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.

47  Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?”

Mstari huo haumzungumzii Musa kama Musa, kwamba yupo mahali Fulani mbinguni, anawashitaki watu..hapana!! bali unazungumzia maneno ya Musa (yaani mahubiri yake). Hayo ndiyo yayowashitaki watu sasa, na yatakayowashitaki watu siku ya hukumu, ndio maana hapo katika mstari wa 47 unamalizia kwa kusema.. “Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?”.

 Sasa Ni kwa namna gani maneno ya Musa yanawashitaki watu sasa?, tutakuja kuona mbele kidogo, lakini sasa tuangalie kwa ufupi ni jinsi gani yatawashitaki watu siku ya hukumu…

Bwana Yesu alisema mahali Fulani maneno haya..

Yohana 12:47  “Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu

48  Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, ANAYE AMHUKUMUYE; NENO HILO NILILOLINENA NDILO LITAKALOMHUKUMU SIKU YA MWISHO.

49  Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.”

Umeona? hapo Bwana Yesu anasema..”Neno analolihubiri ndilo litakalohumu siku ya mwisho”.

Hivyo hata Musa naye, hasimami kumhukumu mtu, bali injili yake ndiyo itakayohukumu watu siku ya mwisho..Kama Musa alitabiri kwamba “Atakuja Masihi”, na Masihi alipokuja kweli kulingana na huo unabii, watu wakamkataa Masihi huyo, basi siku ile ya hukumu, Unabii ule alioutoa kwa uwezo wa Roho utawahukumu wale watu, waliomkataa Masihi. Kwasababu Musa alisema kitu alichoonyeshwa na Mungu, na wala si kwa nafsi yake.

Na si maneno ya Musa tu peke yake, bali na ya Mitume wote wa Mungu na Manabii katika biblia takatifu.

 Kwamfano utaona mahali Fulani Mtume Paulo alisema maneno yafuatayo kwa uwezo wa Roho…

1Wakorintho 6:9  “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? MSIDANGANYIKE; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,  wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi”

Na mtu akausikia mstari huo aliouzungumza Paulo kwa ufunuo wa Roho, lakini akaudharau, na kuona kama kasema hayo kwa akili zake, siku ile ya hukumu, Maneno hayo ya Mtume Paulo yatamhukumu. Ndio maana Mtume Paulo mwenyewe alisema tena maneno yafuatayo..

Warumi 2: 16 “katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, SAWASAWA NA INJILI YANGU, kwa Kristo Yesu”.

Hapo anasema “sawasawa na Injili yangu”.. maana yake tutahukumiwa kulingana na Injili ya Paulo, na mitume wengine kwenye biblia, ndio maana nyaraka za Mitume, Roho Mtakatifu kazifanya leo kuwa ni Neno lake.  Chochote kilichozungumzwa na Mtume Paulo katika biblia, au Mtume Petro, au Yohana, au Mathayo kimekuwa ni NENO LA MUNGU KAMILI, na wala si la huyo mtume, na ndicho siku ile ya hukumu, kitakacho hukumu watu.

Mtume Paulo alisema  kwa ufunuo wa Roho…“  Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika kama sina upendo mimi si kitu”. Maana yake kama hatutatafuta upendo kwa bidii, na kujitumainisha kwa karama tulizo nazo, kama lugha au unabii,  siku ile hatutaurithi uzima wa milele, kwasababu Neno hili litasimama kutuhukumu, kwamba tulipaswa tuwe na upendo na si karama tu peke yake.

Lakini pamoja na hayo, Maneno yote ya Watumishi wa Mungu waliopo katika Biblia, yanasimama pia kutuhukumu leo, Maana yake ni kwamba Injili ya Musa, Paulo, Petro, Yohana, na wengine wengi katika biblia, yapo yanatuhukumu wakati huu.

Sasa yanatuhukumu kwa namna gani?

Jibu ni rahisi, kwa njia ya MASHITAKA!.

Mtu anayejiita ameokoka, na huku anajua kabisa katika biblia Mtume Paulo aliandika kwa uwezo wa Roho katika..

1Wakorintho 6:16  “Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja”

Na kwa kulijua hili neno, akakaidi na kwenda kufanya uasherati makusudi, moja kwa moja Shetani analichukua hili andiko na kwenda nalo mbele za Mungu, kumshitaki mtu huyo, atakachosema ni hichi>> “Bwana Mungu Yule mtu, anayesema amekupokea wewe, tazama anafanya uzinzi na kahaba makusudi na ilihali anajua kabisa katika maandiko yako umesema, yeye ajiunganishaye na kahaba ni mwili mmoja naye,”.

Kwa mashitaka kama hayo, shetani anashinda hoja juu yako, na hivyo unahesabika kuwa na hatia juu ya hilo andiko… Ni heri ungekuwa hujaokoka halafu unafanya hayo, shetani asingekuwa na hoja nyingi juu yako, lakini unasema umempokea Yesu lakini unafanya uasherati, hapo ndipo unakabidhiwa shetani na Adui yako shetani anaweza kukufanya lolote kuhakikisha kuwa unakuwa mwili mmoja na Yule unayezini naye… Maana yake matatizo yake yote na laana anazobeba huyo unayezini naye, zinakuja kwako (kwasababu mmeshakuwa mwili mmoja), hata kama anamapepo basi na wewe ni rahisi kuyashiriki. Ndio maana kuna hatari kubwa sana ya kulipuuzia Neno la Mungu, hata tukiwa hapa duniani, kabla hata ya kufika siku ya hukumu.

Hivyo ni muhimu sana kulifuata na kulishika Neno la Mungu, na wala si la kulidharau, kwasababu  ndilo tutakalohukumiwa nalo siku za Mwisho na ndilo linalotushitaki sasa kupitia adui yetu shetani. Na neno la Mungu linapatikana katika kitabu kimoja tu! Kinachoitwa Biblia yenye vitabu 66, na si kwenye kitabu kingine chochote.

Kama hujampokea Yesu leo, huu ndio wakati wako, shetani hakupendi kama unavyodhani, anachokitaka kwako ni ufe katika dhambi zako, siku ile ukahukumiwe na kutupwa katika lile ziwa la Moto. Huko tumwache aende peke yake, lakini sisi tujiokoe roho zetu kwa kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo, na kutubu dhambi zetu, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu, na kupokea Roho Mtakatifu, ili tujiweka salama na tuwe na uhakika wa uzima wa milele.

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI, AU KUTOA TALAKA?

MMESIKIA KWAMBA IMENENWA?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

NJIA YA KUPATA WOKOVU.

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya usimfunge ng’ombe kinywa apurapo nafaka!.(Kumbukumbu 25:4)

Jibu: Neno kupura maana yake ni “kutenganisha mbegu ya nafaka kutoka katika suke lake”. Kwamfano tunapozitoa punje za ngano, au mchele kutoka katika masuke yake, hapo tunakuwa tumezipura hizo nafaka, tunapotoa maharage kutoka katika yale maganda yake, hapo tumepura maharage.

Sasa zipo njia nyingi za namna ya kupura nafaka,  zamani njia maarufu  zilizokuwa  zinatumika ni aidha kutumia watu au wanyama. Lakini katika zama zetu hizi, zipo mashine za kufanya hivyo.

Kwahiyo njia hiyo ya kwanza ya kutumia watu, ni pale watu wanapoyatwaa masuke makavu na kuyatwanga au kuyachapa na kitu mfano wa fimbo nzito, njia hii ilikuwa ni ya kuchosha kidogo kwasababu ilihitaji nguvu na watu, na ilikuwa inachukua muda mrefu. Lakini pia ilikuwepo njia ya wanyama, ambapo anyama kama ng’ombe analazimishwa kupita juu ya  masuke ya nafaka hizo kavu, na anapozikanyaga, zile mbegu zinatengana na masuke yake. Hivyo njia hii ilikuwa ni rahisi, kwasababu ilikuwa haitumii nguvu, na ilikuwa ni ya muda mfupi!. Ni sawa na kilimo cha mkono na kile cha kutumia ng’ombe. Kile cha ng’ombe ni rahisi Zaidi kuliko cha mkono.

Sasa wakati wa kupura kulikuwa na tabia ya watu kuwafunga ng’ombe midomo wakati wa kuzipura nafaka!, ili wasizile zile nafaka. Kwahiyo mtu yupo tayari kumfanyisha ng’ombe kazi ya kupura tani kadhaa za nafaka, lakini hataki hata aonje katika kile kidogo, wakati anazipura. Sasa kwa tabia hiyo ndipo Mungu akawapa amri wana wa Israeli kwamba wakati wa kupura nafaka wasiwafunge ng’ombe vinywa, maana yake wawaache na wenyewe wale katika hizo nafaka zinazopurwa.

Kumbukumbu 25: 4 “Ng’ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa”.

Sasa kwanini Mungu aliitoa hiyo sheria?. Ni kwasababu ng’ombe hata iweje hawezi kumaliza tani nzima ya nafaka, atakula kidogo tu atashiba!, hiyo nyingine ataacha, hivyo haiwezi kuleta athari yoyote wala hasara yoyote kwa mzigo ule wote wa nafaka. Kwasababu mpaka umeamua kutumia ng’ombe kupuria na si mkono wako, maana yake mzigo wa nafaka ulio nao ni mwingi. Kwahiyo kumnyima ng’ombe chakula kidogo tu katika hicho, ambacho ni anakila tu hapo hapo, na wala hakipeleki ghalani, ni kukosa utu na huruma.

Mithali 12:10 “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili”.

Sasa ufunuo wa mstari huo ni nini?..Mtume Paulo kwa uweza wa Roho alitoa ufafanuzi

Tusome, 1Wakorintho 9:9, (zingatia vipengele vilivyoainishwa kwa herufi kubwa)

1Wakorintho 9:9 “Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, USIMFUNGE KINYWA NG’OMBE APURAPO NAFAKA. JE! HAPO MUNGU AANGALIA MAMBO YA NG’OMBE?

10 Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini, naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake.

11 IKIWA SISI TULIWAPANDIA NINYI VITU VYA ROHONI, JE! NI NENO KUBWA TUKIVUNA VITU VYENU VYA MWILINI?

12 Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo.

13 HAMJUI YA KUWA WALE WAZIFANYAO KAZI ZA HEKALUNI HULA KATIKA VITU VYA HEKALU, NA WALE WAIHUDUMIAO MADHABAHU HUWA NA FUNGU LAO KATIKA VITU VYA MADHABAHU?

14 NA BWANA VIVYO HIVYO AMEAMURU KWAMBA WALE WAIHUBIRIO INJILI WAPATE RIZIKI KWA HIYO INJILI”.

Katika mfano huo, ng’ombe kafananishwa na Mtumishi yeyote wa kweli wa Mungu, au anaweza kuwakilisha kanisa la Kristo, maana yake ni kwamba kama kuna sehemu unanufaika kiroho aidha kanisani au kupitia mtumishi wa Mungu, kwamba kupitia yeye au hilo kanisa, pamechangia pakubwa sana kupata mafanikio yako ya kiroho na kimwili, hupaswi kuzuia chochote katika vile Mungu alivyokubariki, yaani kumbariki yule mtumishi au lile kanisa, au ile huduma. KWASABABU HATAKULA CHOTE!, ni kidogo tu.. Ng’ombe anapokusaidia kupura tani zako za nafaka, anachotaka kutoka kwako kama ujira wake, ni kile chakula cha siku tu!..wala hahitaji ghala lako zima, utakuwa usiye na utu kama utamnyima hata hicho!!. Kwasababu hicho ndicho kitakachompa nguvu ya yeye kuendelea kukusaidia kuzipura hizo nafaka.

Kadhalika utakuwa ni mtu wa ajabu sana, kama utakuwa unanufaika na Baraka za kimbinguni kupitia watumishi wa Mungu, halafu hujigusi hata kidogo!!!.. Ni biblia ndio inasema hivyo, kwamba  hao wahubirio injili, wapate riziki kupitia hiyo. Lakini kama utaona ni sawa wewe kunufaika kiroho lakini si sawa kuchangia chochote!.. Hapo unajipunguzia thawabu zako tu! Za rohoni na mwilini. Biblia inasema wewe ni mkatili! Na mwovu! (Mithali 12:10).

Ametumia mfano mrahisi tu! Wa ng’ombe apurapo nafaka!… ili tuweze kuelewa ni jinsi gani ilivyo ni jambo la kikatili, kuzuilia fedha yako au chochote Mungu anachokubariki,  katika kuipeleka kazi ya Mungu mbele, na ilihali unanufaika na hicho kitu kwa asilimia kubwa.

Unaweza kusoma tena juu ya jambo hilo hilo katika 1Timotheo 5:18.

 Je! Wewe ni miongoni mwa wanaowafumba vinywa ng’ombe zao wapurapo nafaka?..wewe ni mmoja wao wa watu wakatili na waovu??. Kama ni mmoja wao basi tubu!..kwasababu ulikuwa unafanya dhambi, na anza kuwa mwenye huruma, na mtu unayejali. Mtolee Mungu kwa moyo pasipo kulazimishwa, kwasababu pumzi unayovuta hulipii chochote, uzima ulionao anakupa bure!, injili unayoipata kila siku hautozwi chochote, sasa kwanini na wewe usijali pasipo kuambiwa, wala kulazimishwa.

Bwana akubariki.

Kumbuka Kristo anarudi, na dalili zote zimeshatimia, hivyo kama hujampokea Yesu, ni vizuri ukafanya hivyo leo na wala si kesho!.

Luka 12:35 “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka;

36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara”

Maran atha!.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

NGUVU YA SADAKA.

MTEGO HUTEGWA BURE, MBELE YA MACHO YA NDEGE YE YOTE.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Chamchela ni nini kwenye biblia?(Zaburi 58:9, Amosi 1:14)

Uga ni nini? Na kazi yake ni ipi kibiblia?

Rudi nyumbani

Print this post

Kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe.

SWALI: Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema kwa herufi gani hii kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe?

Wagalatia 6:11 “Tazameni ni kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe”!


JIBU: Ili tufahamu vizuri ni vema tukatazama maudhui ya kitabu cha Wagalatia ilikuwa ni nini, Kitabu hichi Mtume Paulo aliwaandikia wagalatia, kanisa ambalo alilizaa yeye mwenyewe katika Kristo. Kulingana na kitabu kuna wakati ambapo aliondoka, lakini akiwa huko mbali alipata taarifa kuwa Wagalatia wameiacha Imani aliyowaachia hapo mwanzo na kuigeukia injili ya namna nyingine, Ambayo kimsingi ililetwa na baadhi ya wayahudi waliotoka Yerusalemu.

Wagalatia 1:6 “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.

7 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo”.

Wayahudi waliowashurutisha watu wa mataifa waliokoka, kuwa ni lazima watahiriwe kama sheria ya Musa inavyosema ndio ukristo wao utakubalika mbele za Mungu, na sio kutahiriwa tu bali pia wazishike sheria nyingi zote, kama torati inavyosema vinginevyo Mungu hawatambui.

Na kweli baadhi ya wagalatia hao wakaanza kuishi kama wayahudi walivyoishi, wakaanza kuzishika sabato, kutahiriwa, kutawadha kabla ya kula, n.k. mambo ambayo hapo kabla walikuwa hawayafanyi na Kristo alikuwa pamoja nao.

Lakini mtume Paulo kujua hilo wameshageukie injili ya aina nyingine ndio akawaandikia huo waraka kwao, mpaka kufika hatua ya kuwauliza ni nani ALIYEWALOGA?.

Wagalatia 3:1 “Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?

2 Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na Imani”?

Walikuwa wanaenenda vizuri, wamepokea Roho Mtakatifu, iweje sasa, wanayarudia mafundisho manyonge ya awali ya wayahudi ya kuishi katika mwili tena? Msiguse, msishike, msionje..(Wagalatia 2:21). Jambo hilo lilimshtusha sana mtume Paulo.

Sasa mwishoni kabisa baada ya maonyo mengi, mtume Paulo ndio anahitimisha kwa kusema..

Wagalatia 6:11 “TAZAMENI NI KWA HERUFI GANI KUBWA nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe!

12 Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu.

Kusema hivyo, ni kuonyesha msisitizo wa waraka wake, wa maneno aliyoyasema kuwa yupo makini na alichokisema, na anamaanisha..na ndio maana waraka huo akauandika kwa maneno makubwa, tofauti na nyaraka zake nyingine, kuonyesha kuwa maagizo aliyowapa ni sahihi.

Ni kama leo hii tu, ukikutana na habari fulani halafu katikati ukakutana na sentensi imeandikwa kwa herufi kubwa, utafahamu kuwa mwandishi anawekea msisitizo hicho alichokisema, ndicho alichokifanya Paulo wakati ule, waraka ule aliundika katika herufi kubwa(au maneno makubwa), kuonyesha msisitizo wa alichokisema.

Leo hii natamani pia baadhi ya madhehebu kama vile sabato watambue waraka huu, kwasababu kulikuwa na sababu kubwa sana ya Paulo kuandika maneno hayo, kwasababu alijua kabisa mambo haya bado yanaweza kupuuziwa na baadhi ya waaminio, hata siku za mwishoni, Lakini cha kusikitisha ni kuwa wagalatia wengi bado wapo  leo hii  miongoni  mwa wakristo.

Kitendo cha kuichagua siku Fulani na kuifanya kuwa takatifu Zaidi ya nyingine na kusema hiyo ndio muhuri wa Mungu, wakati biblia inatuambia muhuri wa utakatifu wetu ni Roho Mtakatifu (Waefeso 4:30), tujue kuwa tumeshalogwa na injili nyingine ambayo sio ile tuliyoachiwa na mitume.

Kitendo cha kusema nyama Fulani ni najisi, kwamba tukiila hiyo, tunamkosea Mungu, tujue tayari tumeshachukuliwa na mafundisho ya injili nyingine.

Turudi kwenye misingi ya Neno bila kujali madhehebu yetu yanatufundisha nini. Hapo ndipo tutakapokuwa salama. Vinginevyo tutakuwa tumeshachukuliwa na roho zidanganyazo ambazo zilizotabiriwa kutokea siku za mwisho za kuwazuia watu wasile vyakula ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani soma (1Timotheo 4:1-5).

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.

Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari?”

MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.

FAHAMU UWIANO MUNGU ANAOHITAJI KUUONA KWETU.

“Yodi” ni nini kama tunavyoisoma katika Mathayo 5:18?

Rudi nyumbani

Print this post