Kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe.

Kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe.

SWALI: Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema kwa herufi gani hii kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe?

Wagalatia 6:11 “Tazameni ni kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe”!


JIBU: Ili tufahamu vizuri ni vema tukatazama maudhui ya kitabu cha Wagalatia ilikuwa ni nini, Kitabu hichi Mtume Paulo aliwaandikia wagalatia, kanisa ambalo alilizaa yeye mwenyewe katika Kristo. Kulingana na kitabu kuna wakati ambapo aliondoka, lakini akiwa huko mbali alipata taarifa kuwa Wagalatia wameiacha Imani aliyowaachia hapo mwanzo na kuigeukia injili ya namna nyingine, Ambayo kimsingi ililetwa na baadhi ya wayahudi waliotoka Yerusalemu.

Wagalatia 1:6 “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.

7 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo”.

Wayahudi waliowashurutisha watu wa mataifa waliokoka, kuwa ni lazima watahiriwe kama sheria ya Musa inavyosema ndio ukristo wao utakubalika mbele za Mungu, na sio kutahiriwa tu bali pia wazishike sheria nyingi zote, kama torati inavyosema vinginevyo Mungu hawatambui.

Na kweli baadhi ya wagalatia hao wakaanza kuishi kama wayahudi walivyoishi, wakaanza kuzishika sabato, kutahiriwa, kutawadha kabla ya kula, n.k. mambo ambayo hapo kabla walikuwa hawayafanyi na Kristo alikuwa pamoja nao.

Lakini mtume Paulo kujua hilo wameshageukie injili ya aina nyingine ndio akawaandikia huo waraka kwao, mpaka kufika hatua ya kuwauliza ni nani ALIYEWALOGA?.

Wagalatia 3:1 “Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?

2 Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na Imani”?

Walikuwa wanaenenda vizuri, wamepokea Roho Mtakatifu, iweje sasa, wanayarudia mafundisho manyonge ya awali ya wayahudi ya kuishi katika mwili tena? Msiguse, msishike, msionje..(Wagalatia 2:21). Jambo hilo lilimshtusha sana mtume Paulo.

Sasa mwishoni kabisa baada ya maonyo mengi, mtume Paulo ndio anahitimisha kwa kusema..

Wagalatia 6:11 “TAZAMENI NI KWA HERUFI GANI KUBWA nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe!

12 Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu.

Kusema hivyo, ni kuonyesha msisitizo wa waraka wake, wa maneno aliyoyasema kuwa yupo makini na alichokisema, na anamaanisha..na ndio maana waraka huo akauandika kwa maneno makubwa, tofauti na nyaraka zake nyingine, kuonyesha kuwa maagizo aliyowapa ni sahihi.

Ni kama leo hii tu, ukikutana na habari fulani halafu katikati ukakutana na sentensi imeandikwa kwa herufi kubwa, utafahamu kuwa mwandishi anawekea msisitizo hicho alichokisema, ndicho alichokifanya Paulo wakati ule, waraka ule aliundika katika herufi kubwa(au maneno makubwa), kuonyesha msisitizo wa alichokisema.

Leo hii natamani pia baadhi ya madhehebu kama vile sabato watambue waraka huu, kwasababu kulikuwa na sababu kubwa sana ya Paulo kuandika maneno hayo, kwasababu alijua kabisa mambo haya bado yanaweza kupuuziwa na baadhi ya waaminio, hata siku za mwishoni, Lakini cha kusikitisha ni kuwa wagalatia wengi bado wapo  leo hii  miongoni  mwa wakristo.

Kitendo cha kuichagua siku Fulani na kuifanya kuwa takatifu Zaidi ya nyingine na kusema hiyo ndio muhuri wa Mungu, wakati biblia inatuambia muhuri wa utakatifu wetu ni Roho Mtakatifu (Waefeso 4:30), tujue kuwa tumeshalogwa na injili nyingine ambayo sio ile tuliyoachiwa na mitume.

Kitendo cha kusema nyama Fulani ni najisi, kwamba tukiila hiyo, tunamkosea Mungu, tujue tayari tumeshachukuliwa na mafundisho ya injili nyingine.

Turudi kwenye misingi ya Neno bila kujali madhehebu yetu yanatufundisha nini. Hapo ndipo tutakapokuwa salama. Vinginevyo tutakuwa tumeshachukuliwa na roho zidanganyazo ambazo zilizotabiriwa kutokea siku za mwisho za kuwazuia watu wasile vyakula ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani soma (1Timotheo 4:1-5).

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.

Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari?”

MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.

FAHAMU UWIANO MUNGU ANAOHITAJI KUUONA KWETU.

“Yodi” ni nini kama tunavyoisoma katika Mathayo 5:18?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments