Njuga ni nini (Isaya 3:16, Zekaria 14:20)?

Njuga ni nini (Isaya 3:16, Zekaria 14:20)?

Njuga ni kengele ndogo ndogo zinazofungwa miguuni au mikononi, na wakati mwingine shingoni, wanavishwa watoto, au watu wanapotaka kucheza ngoma, au wanyama, kama vile ngamia, na farasi n.k..tazama picha

Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyolitaja Neno hilo;

Isaya 3:16 “Bwana akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;

17 Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na Bwana ataifunua aibu yao”.

Zekaria 14:20 “Siku hiyo katika njuga za farasi yataandikwa maneno haya, WATAKATIFU KWA Bwana; navyo vyombo vilivyomo ndani ya nyumba ya Bwana vitakuwa kama mabakuli yaliyoko mbele ya madhabahu”.

Kutoka 28:33 “Nawe katika pindo zake utatia makomamanga ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na ya rangi nyekundu, kuzunguka pindo zake kotekote; na njuga za dhahabu kati ya hayo makomamanga pande zote;

Kutoka 28:34 “njuga ya dhahabu na komamanga, njuga ya dhahabu na komamanga, katika pindo za joho kuizunguka pande zote. 35 Nayo itakuwa juu ya Haruni akitumika; na sauti ya hizo njuga itasikilikana hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele ya Bwana na hapo atokapo nje, ili kwamba asife.

36 Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa machoro ya muhuri, MTAKATIFU KWA Bwana”.

Soma pia;

Kutoka 38:25-26, Isaya 3:18.

Maana yake rohoni ni ipi?

Njuga zinafanya kazi kuu mbili, ya kwanza ni zinafungwa  ili mtu au mnyama asipotee, kwasababu kule anapotembea zile kengele zinalia kumtambulisha yupo wapi.
Na pili zinatumika kama zana za muziki, katika tamaduni nyingi watu wanaocheza ngoma walikuwa navaa njuga.

Vivyo hivyo kila mmoja wetu ni lazima awe amevishwa njuga za Bwana, ili tusipotee usoni pa Bwana, na pili ili kumwimbia Mungu sifa, za kweli.
Hivyo anakuwa amevikwa njuga hizi, pale anapojazwa  Roho Mtakatifu. Swali ni je sisi tumejazwa Roho Mtakatifu?

Shalom.

Tazama tafsiri ya maneno mengine ya ki-biblia chini.

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Mjanja ni mtu wa namna gani kwenye biblia?(Mathayo 27:63)

Rangi ya samawi ni ipi kibiblia(Kutoka 36:37)?

Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?

Shokoa ni nini katika biblia?

Je kuweka mapambo kama mikufu, vikuku na kutoboa pua ni dhambi?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments