Je kuweka mapambo kama mikufu, vikuku na kutoboa pua ni dhambi?

Je kuweka mapambo kama mikufu, vikuku na kutoboa pua ni dhambi?

SWALI: Ezekiel. 16:11 “Nikakupamba kwa mapambo pia nikakutia vikuku mikononi mwako na Mkufu shingoni mwako 12.nikatia Hazama puani mwako na pete masikioni mwako na Taji nzuri juu ya kichwa chako.

1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri pamoja na adabu nzuri na moyo wa kiasi si kwa kusuka nywele wala kwa dhahabu na lulu wala kwa nguo za thamani 10.bali Kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wanao ukili uchaji wa mungu”

Swali! Ni kosa kwetu kujipamba au Kuna aina ya mapambo tunayopaswa na mengine hatupaswi naomba ufafanuzi wako?”


JIBU: Mstari huu wa Ezekiel 16, ndio unaotumika na wengi wanaoamini kuwa kujipamba na kujitia wanja na kutia mapambo na kutoboa pua na masikio sio dhambi, kwasababu Mungu kahalalisha hapo kwenye Ezekieli..Hali kadhalika wanaoamini sio sahihi kwa mwanamke wa kikristo kujipamba na kuwa kama mwanamke wa kidunia, wanasimamia mstari huo wa 1Timotheo 2:9.

Kwa ufupi biblia haijichanganyi, kwasababu Mungu ni mkamilifu, na kila anachokizungumza ni Kweli, hivyo kinachojichanganya ni ufahamu wetu sisi… Sasa hilo andiko la kwenye Ezekieli na hilo la Timotheo yote ni maneno ya Mungu hakuna lililokosewa, wala hakuna linalokinzana na lingine, unaokinzana ni uelewa wetu na si Neno la Mungu. Sasa tofauti iliyopo katika hiyo mistari miwili ni kwamba katika Ezekieli ule ni mfano na katika Timotheo ni Agizo…

Katika Ezekieli ukianza kusoma kuanzia juu mstari wa kwanza, utaona Mungu alikuwa analifananisha Taifa la Israeli(na mji wake mkuu Yerusalemu) na mwanamke, na katika mfano huo akatumia utaratibu wa wanawake wa kidunia jinsi wanavyopambwa na kupendezwa na kuvalishwa vikuku, na kuvishwa mikufu, na kuvalishwa pete za masikio wanapoolewa…na Mungu akajiweka katika nafasi hiyo jinsi alivyolipenda Taifa hilo kama mwanamke aliyepambwa katika roho…lakini kama vile wanawake wa kidunia wasio waaminifu wanavyozisaliti ndoa zao kwa kiburi cha uzuri wao, ndivyo Yerusalemu ilivyofanya mbele za Mungu, na sio sehemu moja Mungu analifananisha Taifa la Israeli na mwanamke,

Utaona sehemu nyingine nyingi analiita binti Sayuni, Ukisoma katika Hosea utaona analifananisha taifa hilo na mwanamke aliyemwacha mumewe n.k..Hivyo huo ulikuwa ni mfano tu! Na sio amri, hivyo haimaanishi kwamba wanawake wanapaswa wajitie mapambo, watoboe pua na masikio na kujifananisha na wanawake wa kidunia. Hapana bali mapambo yao yanapaswa yawe ya rohoni, kama biblia inavyoagiza.

Ili kuelewa vizuri kuwa mfano sio amri, turudi tena kutafakari mfano mwingine katika Agano jipya, ambao huo utatufumbua macho zaidi.

Tuutafakari mfano ule wa wanawali kumi…ambao tunaupata katika Mathayo 25, katika mfano ule kama wengi wetu tunavyoujua, kulikuwa na Bwana mmoja mwenye wanawali 10, (maana yake mabikra)..Hawa wote walikuwa wameposwa tayari kwa kuolewa na Bwana huyu mmoja…lakini baadhi yao walikuwa werevu na wengine wapumbavu…

Sasa katika mfano huo, Bwana Yesu ndiye aliyejifananisha na huyo Bwana harusi kwenye mfano huo, na wale wanawali 10, ndio sisi kanisa lake, ambao miongoni mwao wapo werevu na wapumbavu…Sasa kwa mfano huo basi wa mtu mmoja kuwa na wake 10, kwamba Bwana Yesu alikuwa anahalalisha ndoa za mitara…Kwamba kila mmoja sasa ni sawa kwenda kuoa wanawake 10 si Bwana alisema pale?…Unaona? Ule Bwana alioutoa ni mfano tu!..ambapo alitumia desturi za watu wa mataifa za kuoa wake wengi ili kupitisha tu ujumbe…na sio kutoa amri kwamba na sisi tupose au tuoe wanawake 10.

Na ndio maana Bwana Yesu mwenyewe alisema katika Marko

Marko 10:5 “Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.

6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.

7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;

8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja”.

Umeona?..kwahiyo si sahihi kutumia mfano na kuufanya kuwa amri au Agizo (huko ni kutafsiri maandiko vibaya)…Pia utaona Bwana Yesu alitoa mfano mwingine kwamba atakuja kama mwivi usiku wa manane, hiyo haimaanishi kuwa wizi ni halali, au haimaanishi Bwana Yesu ni mwizi…hapana!. Anatumia matukio ya kiduni na kujiweka yeye au watu wake katika hizo nafasi, ili kufikisha tu ujumbe Fulani..

Kwa mantiki hiyo basi, ndio maana Mtume Paulo kwa kulijua hilo kwa ufunuo wa Roho …hakuchanganyikiwa na hayo maandiko ya kwenye Ezekieli kama sisi tulivyochanganyikiwa baadhi yetu sasa…ndio maana akatuandikia..kwamba

“…wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujistri pamoja na adabu nzuri na moyo wa kiasi si kwa kusuka nywele wala kwa dhahabu na lulu wala kwa nguo za thamani, bali Kwa metendo mema kama iwapasavyo wanawake wanao ukili uchaji wa mungu” .

Hivyo wewe mama/binti/mwanamke wa kikristo usidanganyike na uongo wa shetani uliozagaa huko na kule, mtaani kwamba Mungu haangalii mavazi na anapendezwa na wanawake wanaojichubua uso, au wanaopaka rangi mdomoni, au wanaotoboa masikio na pua, au wanaopaka wanja…au wanaovaa nguo za nusu uchi na za kubana. Wote wafanyayo mambo kama hayo ni machukizo na wanajifungulia milango ya kuingiliwa na maroho ya adui, na hatimaye kuishia katika jehanamu ya moto. Nyakati hizi ni za hatari na tunaishi katika siku za mwisho, mafundisho ya uongo yametabiriwa kuzagaa…shetani anafanya juhudi nyingi sana kuwavuta watu kwake, kwasababu anajua muda wake ni mchache sana.

Hivyo geuka leo, baada ya kuyaelewa haya maandiko…Mpe Yesu Kristo maisha yako kama bado hujaokoka, na upokee Roho Mtakatifu. Kwasababu Roho mtakatifu akishaingia ndani yako ndio atakufundisha hili andiko kuwa mwanamke anapaswa ajipambane ndani kwa matendo mema ya haki na sio nje kama wanawake wakileo wanavyofanya..

1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao”.

Bwana akubariki sana.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Je! ni vibaya kutaja Huduma kwa kujipa cheo? Mfano Mighty Prophet, Chief Apostle n.k.?

LOLOTE ATAKALOWAAMBIA FANYENI.

Mwaloni ni nini? Na je unafunua nini rohoni?

Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?

LULU YA THAMANI.

INJILI YA KRISTO HAITANGAZWI KWA HATI MILIKI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Meshack-sindotuma-gwanse-mbonye
Meshack-sindotuma-gwanse-mbonye
2 years ago

Nashukuru kwa kupewa mwanga wa maandiko ya MUNGU

Enock
Enock
2 years ago

Nimebarikiwa Sana nanyi. Mungu azidi kuwafunulia. Kanisa lipo katika vita kuu na shetani. Watumishi wa uongo katika kulipotosha kanisa kwa kuruhusu vitu vidogo vidogo vitendeke wamejaa.

Moses Shonza
Moses Shonza
2 years ago

Nimependa haya mafundisho
Niliyahitaji pia kutumiwa na mengineyo nami nipate kushare na wenzangu

WhatsApp number 0659-990-833