Wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa.

by Admin | 24 February 2021 08:46 pm02

SWALI: Biblia inamaanisha nini iliposema “wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa;?

JIBU: Tusome vifungu vyenyewe..

2Petro 2:12 “Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;

13 Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, WAKIDHANIA KUWA ULEVI WAKATI WA MCHANA NI ANASA; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi”;

Hapa Mtume Petro, alikuwa anaeleza jinsi watu waovu wanavyoenenda katika tamaa za mwili, ukisoma tokea juu utaona akiwafananisha na watu wa Sodoma na Gomora..Na moja ya tabia zao ndio hiyo aliyosema “Wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa” akiwa na maana kuwa, wamefikia hatua ambayo kwao anasa zao kama ulevi hawazifanyi tena usiku, bali hata mchana.

Ikumbukwe kuwa anasa zote huwa zinajulikana kuwa zinafanyika usiku.. Na ndio maana wakati ule wa Pentekoste, Roho aliposhuka, wale watu waliwashutumu mitume kuwa wamelewa kwa mvinyo, Lakini Petro aliwaaambia, hakuna aliyelewa, kwasababu sasa hivi ni saa tatu ya mchana (akiwa na maana ni saa 9 alasiri), hakuna mtu anayelewa muda huo.

Matendo 2:13 “Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.

14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.

15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana”;

Soma pia..

1Wathesalonike 5:7 “Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku”.

Umeona, hivyo mpaka mtu imetokea anafanya anasa kama ulevi wakati wa mchana,. Ni mtu aliyevuka mipaka, haoni tena shida kufanya mambo yake maovu hadharani amewazidi hata  wenye dhambi wengine wafanyao mambo kama hayo.Ndivyo walivyofanya watu wa Sodoma na Gomora, walivuka mipaka waliuanika ushoga wao hadharani, bila aibu yoyote.

Ni kama vile tu leo hii, hakuna staha tena duniani, mambo ya giza yanafanyika wazi kwenye matamasha, kwenye TV, yanatumwa Whatsapp, yanaonekana Youtube na kwenye mitaa yetu.

Hii ni kuonyesha kuwa tunaishi katika majira ya kurudi kwa pili kwake Yesu Kristo. Wakati huu ni wa kuilinda mioyo yetu isilemewe na mambo ya kidunia, kama alivyofanya Lutu alivyokuwa Sodoma. Kwasababu ulimwengu huu utakwenda kuangamizwa kwa moto muda si mrefu, kama mtume Petro alivyomalizia kusoma katika waraka huo.

2Petro 3:10 “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?”

Je umeokoka? Je parapanda ikilia leo unaouhakika wa kwenda mbinguni?. Majibu sote tunayo.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/02/24/biblia-inamaanisha-nini-iliposema-wakidhania-kuwa-ulevi-wakati-wa-mchana-ni-anasa/