NA ROHO NA BIBI-ARUSI WASEMA, NJOO!

NA ROHO NA BIBI-ARUSI WASEMA, NJOO!

Shalom, nakukaribisha tuyatafakari Pamoja maneno ya uzima.

Katika hichi kipindi cha mwisho, kuna mwitikio mmoja tu, ambao utamtambulisha bibi-arusi wa kweli wa Kristo ni nani..

Kumbuka bibi-arusi ni tofauti na Suria, Sulemani alikuwa na Masuria 700 lakini wake au (bibia-arusi) walikuwa ni 300 tu. Tofauti ya mke na suria ni kuwa mke anauhalali wa vyote ikiwemo urithi na mali, lakini suria yeye anaweza kupewa vyote lakini sio urithi au jina..Jambo hilo utaliona kwa Ibrahimu, ambaye mbali na Isaka alikuwa pia na watoto wengine 7, lakini wao walipewa zawadi tu, mashamba, majumba n.k..Lakini Isaka peke yake ndiye aliyepewa vyote, zawadi pamoja na urithi na jina,..Na ndio maana mpaka leo, tunamtambua Isaka, na sio wale wengine..Hiyo ni kwasababu walikuwa ni wana wa Masuria na sio wana wa mke halali kama ilivyokuwa kwa Sara. (Kasome Mwanzo 25:5-6)

Ndivyo hivyo hata wakati huu wa mwisho, haya makundi mawili yapo, hivyo usifurahie tu, Mungu kukubariki, usifurahie tu Mungu kukupa hiki au kile..furahia pale unapokuwa na uhakika kuwa wewe ni mrithi wa ahadi za milele za Mungu baada ya Maisha haya..

Kwasababu Masuria sikuzote ni wengi kushinda wake.

Sasa tukirudi katika kitabu cha ufunuo, utaona sehemu nyingi, Bwana Yesu alianza kulitamka  hili Neno “tazama, naja upesi”;.. Utasoma..

Ufunuo 22:7 “Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki….

12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo”.

Hiyo ni kuonyesha kuwa wakati wake wa kurudi duniani umekaribia sana..

Lakini ukishuka chini kidogo utaona, wanaorodheshwa wawili walioitikia mwito huo, nao ni Roho Mtakatifu na bibi-arusi.

22:17 “NA ROHO NA BIBI-ARUSI WASEMA, NJOO! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.

Ni kwasababu gani bibi-arusi alikuwa na ujasiri wa kuitikia mwito huo “Njo Bwana Yesu”? Ni kwasababu, alijua urithi wake halisi upo karibu, ni kwasababu alikuwa na ajasiri wa Imani yake, kwa Yule Roho Mtakatifu aliye ndani yake.

Na ndio maana hata Mtume Yohana, aliposikia Bwana akiyarudia maneno hayo tena chini kidogo, naye pia aliitikia kwa ujasiri mkubwa na kusema amina na uje Bwana Yesu..

Ufunuo 22:20 “Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu”.

Maneno haya bibi-arusi tu peke yake aliyejazwa Roho Mtakatifu ndio atakayekuwa na ujasiri wa kuyasema wakati huu wa mwisho..

Swali la kujiuliza ni je! mimi na wewe tunaweza kuyasema maneno hayo? kumbuka Jibu halipo katika vinywa vyetu bali katika mioyo yetu. Kama hatuna ujasiri huo basi sisi sio bibi-arusi, haijalishi tutasema tumeokoka kiasi gani, sisi tutakuwa ni Masuria tu. Na siku ya unyakuo itakapofikia tutabaki hapa dunia, hatutanyakuliwa Pamoja na bibiarusi wa kweli.

Masuria kwa jina lingine ndio wale wanawali wapumbavu ambao walichukua taa zao, lakini hawakuwa na mafuta ya ziada katika vyombo vyao, Na Bwana arusi alipokuja walikutwa hawana mafuta ya kutosha (Mathayo 25)

Kwahiyo ndugu tusifurahie tu, kusema sisi ni wakristo, bali tufurahie kusema sisi ni bibi-arusi, tuliojazwa Roho Mtakatifu.. Kumbuka lile neno la Bwana “Waitwao ni wengi, ila wateule ni wachache”

Kama tulishaokoka, lakini bado tulikuwa tunaishi maisha ya uvuguvugu, basi  huu ni muda wetu sasa, kuzitengeneza taa zetu katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho.

Na Mungu atatujalia tufikie mwisho mwema kwa neema zake.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI, NA ZA KUZIMU.

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

Je! Shetani alitolea wapi uovu?

KARAMU YA MWANA-KONDOO.

MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Nicolas
Nicolas
3 years ago

Hongera mtumishi wa Bwana. Mungu akubariki, akutie nguvu.