Maseyidi 12 wa Ishmaeli, ni wakina nani?.2)Taa ya Mungu ambayo ilikuwa haijazima wakati wa Eli ni ipi?

Maseyidi 12 wa Ishmaeli, ni wakina nani?.2)Taa ya Mungu ambayo ilikuwa haijazima wakati wa Eli ni ipi?

SWALI: Naomba kuuliza watumishi wa Mungu katika Mwanzo 17:20 anaposema kwa habari ya Ishmaeli atazaa maseyidi 12, hao ndio akina nani kwa Sasa?

2) Pia katika 1samweli 3:3 anasema kipindi Samweli anaitwa na Mungu taa ilikua haijazimika bado Nia taa gani hiyo? Asante Sana Ni hayo.


JIBU: 

  1. Tusome..

Mwanzo 17:18 “Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.

19 Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.

20 Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu”.

Neno Seyidi linamaanisha  mtawala, hivyo hapo biblia ilimaanisha kuwa Ishmaeli atazaa watawala 12.. ambao  utaona wakitajwa kwa majina  katika Mwanzo 25:13

Mwanzo 25:13 “Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu,

14 na Mishma, na Duma, na Masa,

15 na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema.

16 Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao, katika miji yao, na katika vituo vyao, maseyidi kumi na wawili kwa kufuata jamaa zao.

Katika historia  wana hawa wa Ishmaeli walikuwa watu wakuu sana, na ndio chimbuko la mataifa ya kiharabu tunayoyaona sasahivi  kule mashariki ya kati.

2) Je ni Taa ipi hiyo inayozungumizwa katika 1Samweli 3:1?,

Tusome.

1 Samweli 3:1 “Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri.

2 Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona),

3 na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu;

Inadhaniwa kuwa hiyo ni ile taa ya hekaluni, lakini ukitafakari kwa ukaribu, utaona kuwa biblia haikumaanisha ile taa ya hekaluni au ile ya kwenye hema ya kukutania, bali ilimaanisha pumzi au uhai wa Eli, ukikumbuka kuwa habari iliyokuwa inazungumziwa hapo juu ni kuhusu uzee wa Eli, ambapo inasema umri wake ulikuwa umeshaenda sana mpaka macho yake yalikuwa yameshaanza kupofuka.

Biblia inasema..

Mithali 20:27 “Pumzi ya mwanadamu ni taa ya Bwana; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake”.

Unaona? Hivyo hapo ilimaanisha kuwa Pumzi ya uhai wa Eli ilikuwa bado haijamuacha.

Hiyo ni kutukumbusha pia, kuwa upo wakati na sisi Taa ya Mungu itazima ndani yetu. Na kama tunavyojua taa ikizimika huwa kunakuwa na giza na sikuzote gizani hakuna shughuli yoyote inayoendelea. Vivyo hivyo na siku ambayo kila mmoja wetu atakufa, huko atakapoenda hakuna jambo lolote la kimaendeleo atakalolifanya, Hatakuwa na nafasi ya pili ya kutubu ikiwa alikufa katika dhambi, hatakuwa na nafasi ya pili ya kufanya marekebisho ikiwa alizembea zembea katika masuala ya wokovu wake akiwa hapa duniani. Atakachokuwa anasubiria huko ni hukumu tu.

Mhubiri 9:5 “kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa”.

Hivyo tunapaswa tujithamini maisha yetu tunamalizaje mwendo tukiwa hapa duniani? . Kwasababu huko ng’ambo hakuna nafasi ya pili.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments