KURUDI ISRAELI KWASASA NI KUGUMU, SIO KAMA KULE MWANZONI.

KURUDI ISRAELI KWASASA NI KUGUMU, SIO KAMA KULE MWANZONI.

Isaya 10:22 “Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki”.

Wana wa Israeli walidhani, kuchukuliwa tena utumwani na kurudishwa (Babeli na Misri)  kungekuwa ni kurahisi kama ilivyokuwa wakati ule walipotolewa Misri. Walidhani Mungu atakuja kuwatoa tena kama taifa kwa mkono hodari wa nabii kama Musa, na wote watarudi nchi yao.

Lakini mambo hayakuwa hivyo, Mungu aliwaonya mapema akiwaambia hilo jambo halitakuwepo, na ndio maana alitumia muda mrefu sana kuwasihi, watubu waache njia zao mbaya, lakini hawakusikia badala yake wakawa wanawapiga manabii wake na wengine kuwaua,

Lakini siku ya siku ilipofika, yale mataifa 10 yalichukuliwa utumwani Ashuru,  na biblia inatuonyesha hakuna hata mmoja aliyerudi hadi wakati huu wa sasa.. watu wote waliendelea kubaki kule kule,  hata na lile taifa moja la Yuda, ambalo lilikuja kuchukuliwa nalo baadaye Babeli na Nebukadreza, japokuwa nalo lilikuwa na watu wengi sana, lakini ni kikundi kidogo sana, yaani watu wachache sana ndio Mungu aliwarudisha, na hiyo ilikuwa tu ni kuwatunzia uzao vinginevyo wangefananishwa na Sodoma na Gomora, kwa jinsi ambavyo wangepotea wote.

Warumi 9:27 “Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.

28 Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.

29 Tena kama Isaya alivyotangulia kunena, Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao, Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora”.

Sasa biblia inasema mambo hayo yaliandikwa kwa mifano ili kututahadharisha na sisi tulio katika nyakati hizi za hatari (1Wakorintho 10:11). Kwasababu kanisa la Israeli la mwilini lilikuwa linawakilisha kanisa la Kristo la rohoni sasa hivi. Kumbuka mara baada ya Israeli kuingiliwa na ukengeufu,  pale walipoanza kuabudu miungu mingine, hapo ndipo Mungu alipokusudia kuwaangamiza wote, mikononi mwa maadui zao.

Vivyo hivyo na katika Kanisa la Kristo leo hii, Bwana alishatabiri kuwa kuwa kuna majira litaingiliwa na ukengeufu..ndio yale magugu yaliyopandwa na ibilisi ndani ya kanisa (Mathayo 13:24-30).. Sasa ukengeufu huu, ndio unaowafanya wakristo wengi wawe vuguvugu kupita kiasi, Hatushangai kuona idadi ya watu wanaojiita wakristo duniani ikizidi kuongezeka, sasa hivi ni Zaidi ya bilioni tatu.. Ni kama mchanga wa bahari tu, hata zaidi ya walivyokuwa Israeli.

Lakini hiyo sio tija kwamba wote tutaokolewa siku ile.  Ni mabaki tu ndio yatakayookoka, ambayo Yesu aliyafananisha na ‘kundi dogo’

Luka 12:32 “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme”.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema. Walioitwa ni wengi lakini wateule ni wachache. Hichi ni kipindi cha kurekebisha mienendo yetu kama wakristo, kwasababu kurudi Yerusalemu kwa sasa ni kugumu sio kama kule kwa kwanza. Nguvu ya kukuvuta umgeukie Mungu sasa sio kama ile ya kwanza ulipoanza kuamini.

Ni wachache tu ndio watakaorejea, na sisi tuwe miongoni mwa hao. Mungu anatuita kuache dhambi, tumgeukie yeye, tusiungalie ulimwengu, kwani unapoteza sana.. Kwasababu hizi ni nyakati za mwisho na Kristo yupo mlangoni, wakati huu ni ule wa kumalizia, siku yoyote, wakati wowote, tunaweza kushuhudia tendo hilo kuu la unyakuo. Ambapo kwa upande mmoja utakuwa ni furaha na shangwe, lakini kwa upande mwingine kilio na kusaga meno na majuto makubwa.

Bwana atusaidie.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Ni nani aliyesema “Nitume mimi”? katika (Isaya 6:8)

PINDO LA VAZI LAKE SASA LIMEREFUSHWA.

JE UPENDO WAKO UMEPOA?

Fuawe ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 41:7

EPUKA KUUNDA MATARAJIO YAKO, KWENYE AHADI ZA MUNGU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments