JIBU: Tusome,
Mithali 10:10 “Akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka”.
Kukonyeza ni ishara inayojulikana kama ya undanganyifu au ya kupoteza uaminifu. Ni jambo la kawaida tumekuwa tukiliona hata katika maisha ya kawaida, kwa mfano, labda mteja, mmoja amekwenda kununua bidhaa Fulani kwa muuzaji sokoni, Sasa ikatokea, ghafla muuzaji mwingine akakatiza anauza bidhaa kama ile ile, Ni kawaida ya mnunuzi kutaka kuulizia bei halisi ya hiyo bidhaa kwa muuzaji mwingine, Sasa kama kweli yule muuzaji wa kwanza aliambiwa bei halali ,hatoonyesha chochote, lakini kama alitaka kumuuzia kwa bei ya juu Zaidi kuliko ilivyo kawaida, yule muuzaji wa kwanza atatumia ishara Fulani, aidha kumkonyeza muuzaji mwenzake, ili akae kimya..Asimwambie bei halali.
Sasa hiyo ni dalili ya kukosa uaminifu.
Mfano mwingine, utakuta labda mtu na familia yake wamealikwa kwenye sherehe fulani, na kule kwenye sherehe pengine baba wa familia hiyo akakutana na wanawake wengine wazuri, akawatamani, sasa njia ambayo anaweza kutumia kuwasiliana nao, kirahisi ili pengine baadaye wakutane, ni kwa kumkonyeza,..Huo ni mfano tu.
Umeona kitendo hicho kimetumika kama ishara ya udanganyifu.
Biblia inasema..
Mithali 6:12 “Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu. 13 HUKONYEZA KWA MACHO, hunena kwa miguu, Huwaashiria watu kwa vidole vyake”
Mithali 6:12 “Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu.
13 HUKONYEZA KWA MACHO, hunena kwa miguu, Huwaashiria watu kwa vidole vyake”
Na kukonyeza kwa siku hizi kumezidi hata kule kunakojulikana kwa kutumia jicho, zipo ishara nyingi za kukonyeza inategemea na mahali husika. Wakati mwingine hata lugha Fulani inaweza kutumika kukonyeza.
Sasa biblia inasema watu wa namna hiyo huleta masikitizo. Na masikitizo hayo huja kote kote, kwake, pamoja na kwa yule aliyemkonyeza. Ikiwa na maana mwisho wake hauwi mzuri sikuzote. Ni uchungu na majuto.
Biblia inatuonya tusiwe watu wa hila, za kutumia ishara za udanganyifu kuleta madhara, au uharibifu kwa wengine.
Hilo ni kosa.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
Wale mamajusi walikuwa ni wakina nani?
THAWABU YA UAMINIFU.
Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)
Herode aliliwa na chango, Je, chango ni nini kibiblia?
Nini maana ya “katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni”.
Mfalme Ahazia alianza kutawala akiwa na umri gani?
Rudi nyumbani
Print this post
Kabisa
Leave your message