SWALI: Bwana Yesu apewe sifa Ukisomo kitabu cha 2 WAFALME 2:24 napenda kuelewa mbona pale wanatokea dubu wawili wa kike mwituni na sio wa kiume?
2Wafalme 2:24 “Akatazama nyuma akawaona, akawalaani kwa jina la Bwana. Wakatoka dubu wawili wa kike mwituni, wakawararua vijana arobaini na wawili miongoni mwao”.
JIBU: Tofauti na sisi wanadamu, kwa upande wa wanyama, asilimia kubwa ya wanyama wenye asili ya kike (majike) huwa wanakuwa ndio wakali zaidi, na washapu kuliko wa jinsia ya kiume. Utaona kwa simba, Dubu na kadhalika. Majike ndio wawindaji n.k.
Ukisoma Mithali 17:12 inasema;
“Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake, Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake”.
Hapo imetumia mfano wa dubu mke, na sio dume, hii ni kuonyesha kuwa hao ndio wakali zaidi hususani pale wanapokuwa na watoto.
Utasoma tena sehemu nyingine Mungu alijifananisha na dubu mke, kwa hasira yake atayaoichia juu ya Israeli kwasababu ya makosa yaliyofanya kinyume chake. Akaifananisha hasira yake na hasira ya dubu jike.
Hosea 13:7 “Basi nimekuwa kama simba kwao; kama chui nitavizia njiani; 8 nitakutana nao kama dubu aliyenyang’anywa watoto wake; nami nitararua nyama ya mioyo yao; na huko nitawala kama simba; huyo mnyama mkali atawararua. 9 Haya ndiyo maangamizo yako, Ee Israeli, ya kuwa wewe u kinyume changu mimi, kinyume cha msaada wako”.
Hosea 13:7 “Basi nimekuwa kama simba kwao; kama chui nitavizia njiani;
8 nitakutana nao kama dubu aliyenyang’anywa watoto wake; nami nitararua nyama ya mioyo yao; na huko nitawala kama simba; huyo mnyama mkali atawararua.
9 Haya ndiyo maangamizo yako, Ee Israeli, ya kuwa wewe u kinyume changu mimi, kinyume cha msaada wako”.
Ni nini tunajifunza? Kwanini walitumiwa dubu wa kike na sio wa kiume?
Hiyo ni kuonyesha uwezo wa jamii ya kike , kuwa wanawake, wanaweza kuwa vyombo viteule vya kumponda ibilisi kwa Bwana, ikiwa tu watasimama katika nafasi zao katika wokovu. Wanawake waliosimama ibilisi anawaogopa sana, kwasababu anajua madhara yatakayoyasababisha katika ufalme wake.
Hivyo ikiwa wewe ni mwanamke unapaswa usimama sasa, uwe na ushujaa kama wa dubu jike, rarua, angamiza, teketeza kazi zote za shetani bila kuona huruma yoyote, kwasababu uwezo huo unao ndani yako.
Zaburi 68:11 “Bwana analitoa neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa;”
Bwana akubariki
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.
KIAMA KINATISHA.
HIZI NI NYAKATI ZA KUJIINGIZA KWA NGUVU.
TUMEPEWA MAMLAKA YA KUKANYAGA NG’E NA NYOKA.
SALA YA UPONYAJI/MAOMBI YA UPONYAJI.
Rudi Nyumbani:
Print this post