Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?

Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?

JIBU: Hakuna mahali popote katika biblia inamtaja Mikaeli kuwa ndiye Bwana Yesu. Kinyume chake, maandiko yanamtofautisha Yesu na Malaika hata kwa asili aliyoitwaa,  Biblia inasema.

Waebrania 2:16 “Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu”.

Ikiwa na maana, kudhihirishwa kwa Bwana Yesu kwa mara ya kwanza, kulikuwa ni katika asili ya mwanadamu na sio Malaika. Na ndio maana utaona, Malaika nao, walimwona na kumtambua kwa mara ya kwanza, siku ile alipozaliwa katika mwili.

1Timotheo 3:16 “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu”.

Ni kweli Mikaeli ni mmoja wa Malaika wakuu mbinguni,na pengine Zaidi ya wote, Lakini hana sifa yoyote ya kudhaniwa kuwa yeye ndiye Kristo, kwani  biblia inatuambia kuwa Kristo anaabudiwa sio tu na wanadamu, bali pia na malaika wote mbinguni(Waebrania 1:6), Lakini  hakuna Malaika yoyote anayeabudiwa.

Pia Kristo alikuwa na mamlaka ya kusamehe dhambi, Pamoja na kukemea pepo kwa uweza wake,lakini Malaika (akiwemo Mikaeli), hawana uwezo huo, wanajiona hawastahili mpaka wanasema Bwana mwenyewe na awakemee mashetani (Yuda 1:9)..

Na mwisho biblia inasema, hakuna mahali popote, Mungu alimwita Malaika yoyote “Mwanangu”, bali hao ni watumishi wake, watumikao kuwahudumia watakatifu, lakini kwa Bwana Yesu, Mungu alimwita mwana, kumtofautisha yeye na Malaika zake.

Waebrania 1:5 “Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?

Hivyo, Mikaaeli ni Malaika wa Bwana na atabakia kuwa hivyo. Lakini ikiwa utatamani kujua Zaidi aina za Malaika wa Mungu, na kazi zao na idadi zao, Fungua hapa >> Je! Kuna malaika wangapi mbinguni?

Swali Je! Unatambua kuwa Mungu ameshawaweka tayari Malaika zake kwa ajili ya mapigo ya siku hizi za mwisho? Una Habari kuwa unyakuo upo karibuni sana kutokea, kuliko unavyoweza kudhani?

Kumbuka paraparanda ya Mungu ikilia leo, basi, Malaika hao wa mapigo, Mungu atawaachilia ulimwenguni mwote, wataipiga dunia kwa kwa zile baragumu saba, na vitasa saba. Wakati huo kutakuwa ni nyakati za shida sana ulimwenguni. Soma Ufunuo 8 &16, ujionee mpendwa. Ni Malaika mahususi wa kuleta mabaya duniani.

Zaburi 78:49 “Akawapelekea ukali wa hasira yake, Ghadhabu, na uchungu, na taabu, Kundi la malaika waletao mabaya”.

Usitamani uwepo wakati huo ndugu yangu, Ni heri leo ukatubu na kumrudia muumba wako. Upokee uhakika wa kuurithi uzima wa milele. Ikiwa utataka kusoma juu ya mapigo hayo, fungua link hii>>

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Neno Saumu lina maana gani katika biblia?

UNYAKUO.

Ninawi ni nchi gani kwasasa?

AINA SABA (7) ZA UNAFIKI, AMBAZO UNAPASWA UJIEPUSHE NAZO.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments