Dinari ni nini na Rupia ni nini (Mathayo 20:2,Ufunuo 6:6)

by Admin | 28 September 2023 08:46 pm09

Dinari ilikuwa ni sarafu ya kirumi yenye thamani ya (utumishi wa kibarua wa siku nzima)..Kwamfano leo hii tuseme kibaru atalipwa kwa siku shilingi elfu 20, na ukawa ndio utaratibu wa nchi nzima, kuwalipa vibarua kiasi hiko kwa siku kama mshahara, basi kiasi hiko cha fedha kingekuwa na thamani sawa na Dinari kwa wakati huo.

Tutalithibitisha hilo Zaidi katika ule mfano Bwana alioutoa wakulima walioajiriwa katika shamba la mizabibu..

Mathayo 20:1  “Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu

2 Naye alipokwisha kupatana na wakulima KUWAPA KUTWA DINARI, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu”.

Kwahiyo “ malipo ya utumishi wa kutwa nzima wa kibarua” ndiyo yaliyokuwa na uthamani wa “Dinari”  na uzito wa sarafu ya Dirani ulikuwa ni “gramu 3.85”,

Kwa urefu kuhusiana na vipimo hivyo fungua hapa  >>>VIPIMO VYA KIBIBLIA

Lakini tukirudi katika “Rupia”.. tunaisoma sehemu moja tu katika kitabu cha Ufunuo 6:6

Ufunuo 6:5  “Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.

6  Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa NUSU RUPIA, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu RUPIA, wala usiyadhuru mafuta wala divai”.

“Rupia” ni sarafu nyingine yenye thamani sawa na “Dinari”.. ambayo ilikuwa inatumiwa zaidi namataifa mengine tofauti na Rumi (uthamani wake ulikuwa ni sawa na mshahara wa kibarua wa kutwa)… Na mpaka sasa bado baadhi ya mataifa yanatumia Rupia!.

Lakini ni somo gani tunalolipata kutoka katika thamani hii ya fedha (Dinari na Rupia)?

Somo kubwa tunalolipata si lingine Zaidi ya lile tunalolisoma katika Mathayo 20:1-16, kuwa thawabu za Mungu hazichunguziki.

Kwa urefu unaweza kusoma hapa >>KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)

AINA TATU ZA WAKRISTO.

GHARAMA YA UFALME WA MBINGUNI.

SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.

Je! Ni sawa kuingia katika shamba la mtu mwingine na kula jinsi utakavyo?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/09/28/dinari-ni-nini-na-rupia-ni-nini-mathayo-202ufunuo-66/