Tofauti kati ya mwonaji na Nabii ni ipi?

Tofauti kati ya mwonaji na Nabii ni ipi?

Katika biblia mtu ambaye alipokea taarifa iliyofichwa kutoka Kwa Mungu na kuiwasilisha Kwa watu aliitwa mwonaji. Alipokea aidha kupitia, maono, ndoto, au kufunuliwa dhahiri, Mfano wa Hawa alikuwa ni Samweli…

1 Samweli 9:9-12

[9](Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.)

[10]Basi Sauli akamwambia mtumishi wake, Umesema vema; haya! Twende. Wakaenda mpaka mji ule aliokuwamo mtu wa Mungu.

[11]Hata walipokwea kwenda mjini, wakakutana na wasichana, wanatoka kwenda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko?

[12]Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu watu wana dhabihu leo katika mahali pa juu;

Lakini baadaye watu Hawa walikuja pia kuitwa Manabii kama tunavyosoma kwenye vifungu hivyo

Isipokuwa Maana ya Nabii ni Pana zaidi sio tu kupokea taarifa kutoka Kwa Mungu na kuiwasilisha Bali pia alisimama kufundisha na kuwarejesha watu, katika Sheria ya Mungu.ikiwemo kukaripia na kukemea, na kuonya. Mfano wa Hawa ni Isaya, Yeremia, Ezekieli, Yona, Hosea, Mika, Hagai, Malaki na wengine.

Hivyo nabii ni lazima pia awe mwonaji, kwamba apokee pia taaarifa za Moja Kwa Moja kutoka Kwa Mungu, na kufichua Siri zilizositirika lakini mwonaji haikuwa lazima afanye kazi ya kinabii,  Bali ni kusema tu kile anachoelezwa, au kufichua Siri zilizojificha, au kuomba mwongozo wa  Roho wa Mungu, Kwa ajili ya jambo/tatizo Fulani.

Hivyo kuhitimisha ni kwamba Kuna maandiko mengine yanawataja waonaji, lakini yalimaanisha pia ni manabii, na mengine yanabakia kumaanisha walewale tu waonaji.

Mfano wake ni Samweli, ambaye alikuwa ni mwonaji lakini pia ni Nabii.

1 Mambo ya Nyakati 29:29

[29]Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji;

Soma pia vifungu hivi, kufahamu zaidi.

(2Samweli 24:11, 2Nyakati 16:7, 29:30,)

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

IELEWE SAUTI YA MUNGU.

TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.

NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA.

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?

NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA

Tofauti kati ya ndoto na Maono ni ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments