Kibiblia mapepo yanafananishwa na inzi.
Inzi siku zote huvutiwa na mazingira ya aina mbili. Ya kwanza ni uchafu. Mahali palipo na uchafu hapakosi inzi, Na ndio maana Bwana baada ya kuhakikisha taifa la Misri linanuka uvundo, kwa harufu na uchafu wa wale vyura waliokufa, akawaanda na inzi waje juu yao ili wayafurahie mazingira yao. Ndio hapo utaona akawaleta wengi sana juu ya wamisri wakawa kero kubwa sana kwao.
Kutoka 8:24 “Bwana akafanya; wakaja wingi wa mainzi kwa uzito sana, wakaingia nyumbani mwa Farao, na katika nyumba za watumishi wake, tena katika nchi yote ya Misri; nayo nchi iliharibiwa kwa ajili ya wale mainzi”
Lakini sio hilo tu, watu wengi wanapuuzia wakidhani kuweka mazingira tu safi ndio kutawafukuza. Lakini pia inzi wanavutiwa na mazingira ya vidonda. Palipo na vidonda, utaona inzi wengi wanakusanyika kwenye eneo hilo.
Maana yake nini? Rohoni ukiwa na majeraha ambayo hayajafunikwa au kutibiwa, kunaweza kukusababishia kuvuta uwepo wa mapepo juu ya maisha yako, Unaweza kweli ukawa umejitahidi kuwa mbali na uchafu wa rohoni na mwilini, huibi,huzini, unaishi maisha ya utakatifu, unatumika kanisani n.k.
Lakini kama una majeraha rohoni mwako,ambayo hayajatibiwa, bado mapepo yanaweza kupata nafasi ya kukusumbua. Una kinyongo cha muda mrefu na mwenzako, hujaachilia, hujasemehe, una uchungu, una wivu, una hasira zisizoachilika,. Fahamu kuwa hayo ni mazingira mazuri ya mapepo.
Ndio hapo utaona mkristo, ameokoka halafu analipuka mapepo, au anasumbuliwa na nguvu za uovu. Unajiuliza mbona huyu hana maisha machafu lakini yanamkuta haya? Sababu kubwa ni eneo hili. Ndio maana biblia inatuambia tulinde sana mioyo yetu kuliko vyote tuvilindavyo. Moyo hukaribisha roho za nje kiwepesi.
Tibu moyo wako, jiachie kwa Yesu, kubali kujikana nafsi, kubali kujishusha, kubali kusamehe, kubali hata kupoteza hicho ulichonacho, ili uiponye nafsi yako. Wivu, hasira, chuki, visitawale kabisa maisha yako. Viwe na adui wako.
Unaweza kusema hizi hali nitazishindaje? Jibu ni kuwa yote hayo yanawezekana endapo tu, utaishi maisha ya kumtazama Kristo, zaidi ya nafsi yako. Macho yako yakielekea kwa Yesu tu daima ukajifunza kwake, kidogo kidogo utaona tabia za mwilini zinaanza kukuachia, unajifunza tabia za Yesu. Na yeye mwenyewe atakusaidia kukuponya kabisa kabisa kwasababu aliahidi hivyo katika Neno lake.
Hosea 6:1 “Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu. 2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake”.
Alisema pia..
Yeremia 30:17 Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.
Jeraha zetu za rohoni ameahidi kuziponya. Na Neno lake ni kweli halitanguki, limethibitishwa. Hivyo anza sasa kumkaribia Kristo na kujifunza kwake.(Mathayo 11:28-29)
Bwana akubariki.
Maombi yangu:
Ee, Baba tumejifunza jinsi adui yetu ibilisi anavyopata nafasi katika mioyo yetu pale tunaposhindwa kuzitibu jeraha zetu. Lakini leo tumetambua makosa yetu, nasi tunatubu mbele zako. Tunaomba utusamehe Baba yetu, Tumedhamiria kutoka katika mioyo yetu kukufuata wewe, na kujifunza kwako, Tunaomba ututibu majeraha yetu yote, yaliyodumu kwa muda mrefu na mfupi, ondoa hasira, ondoa vinyongo, kutokusamehe, wivu, ndani yetu. Nasi tunaamini tangu siku ya leo unatukamilisha. Asante Baba kwa kutusikia. Tunaomba tukishukuru katika jina la Yesu Kristo. Amen.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
Kwanini wakristo walipomuona Petro akigonga walisema “Ni malaika wake”?
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.(Opens in a new browser tab)
KUOTA UNA MIMBA.(Opens in a new browser tab)
KATAA KUWA EUTIKO, WA KUSINZIA IBADANI.
Dina akatoka kuwaona binti za nchi. (Mwanzo 34:1)
Kama Kristo alizichukua dhambi zetu na kutusamehe kwanini kila siku tunatubu?
Rudi nyumbani
Print this post
Bwana Yesu apewe sifa!! mimi nina swali. Ikiwa niliokoka nikabatizwa na kunena kwa lugha mbeleni nikaja kuanguka dhambin je ninaweza kulejea wokovuz? na je tobayangu itaitaji ubatizo upya kama mlango bado upo wazi wa wokovu?