Ni kwa namna gani, upendo husitiri wingi wa dhambi? (1Petro 4:8).

Ni kwa namna gani, upendo husitiri wingi wa dhambi? (1Petro 4:8).

Tusome,

1 Petro 4:8 “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi”.

Awali ya yote ni muhimu kufahamu maana ya neno “kusitiri” na vile vile ni muhimu kufahamu ni nani ambaye anayesitiriwa dhambi zake, je! ni yule anayependa au anayependwa?.

Neno “kusitiri” maana yake “kufunika au kuficha”..mtu aliyevaa nguo za kuufunika mwili wake wote, maana yake “kavaa nguo za kujisitiri mwili wake, ili asibakie kuwa tupu”. (Kauficha mwili wake).

Sasa tukirudi kwenye huo mstari wa kwenye 1Petro 4:8, maandiko yanasema upendano husitiri wingi wa dhambi.

Sasa dhambi zinazositiriwa/kufichwa si za yule anayependa bali yule anayependwa.
Sasa zinasitiriwa kwa namna gani?

Neno la Mungu linasema katika kile kitabu cha 1Wakorintho 13:4-5.

1 Wakorintho 13:4 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; Mwisho kabisa anasema “UPENDO HAUHESABU MABAYA”.

Kutokuhesabu mabaya ndio “Kusitiri dhambi”.

Maana yake ni kwamba mtu mwenye upendo, maisha yake yote ni ya kusamehe tu na kutoweka kumbukumbu ya mambo mabaya anayofanyiwa.

Mathayo 18:21 “Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?

22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini”.

Mfano mzuri wa Mmoja aliyeweza kusitiri wingi wa dhambi nyingi, ni Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe.

Kwa Upendo wake mwingi alijitoa nafsi yake sadaka ili sisi tupate kusitiriwa dhambi zetu. Kwake yeye tumepata ondoleo la dhambi. Tukiwa dhani yake hatuhukumiwi.

Mtume Paulo anazidi kuliweka wazi hilo katika kitabu cha Warumi.

Warumi 4:7 “Heri waliosamehewa makosa yao, Na waliositiriwa dhambi zao.

8 Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi”.

Je na wewe leo dhambi zako zimesitiriwa na kuondolewa kabisa?? Kumbuka dhambi zako haziwezi kuondolewa kama haupo ndani ya pendo la Kristo, kwasababu ni upendo tu ndio unaositiri wingi wa dhambi, maana yake kama haupo ndani upendo wa Kristo, basi hauna msamaha wa dhambi.

Sasa utauliza, unaingiaje katika pendo hilo na kupata msamaha?.

Unaingia katika pendo hilo kwa kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa jina la Yesu Kristo na kumpokea Roho Mtakatifu.

Baada ya hapo dhambi zako zote zitaondolewa na kuwa mrithi wa ahadi za Mungu.

Na vile vile unapowahubiria wengine habari za Pendo la Kristo, na hata wao wakaingia katika pendo hilo, (kwa kutubu na kuacha dhambi)basi utakuwa umewasaidia dhambi zao kufunikwa na pia kuwaokoka na adhabu ya ziwa la moto, sawasawa na maandiko yafuatayo.

Yakobo 5:19 “Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza;

20 jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.

Bwana atubariki sote.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Osward Ngowi
Osward Ngowi
1 year ago

Nimependa mafundisho yenu
Ningependa kujua zaidi juu ya huduma yenu na mahali mnapatikana

Osward Ngowi
Osward Ngowi
1 year ago

Nimebarikiwa sana masomo mazuri yanayohusu upendo haswa neno linalosema upendo wa Mungu unatubidisha