Watu wajikatao ni watu wa namna gani? (Wafilipi3:1).

Watu wajikatao ni watu wa namna gani? (Wafilipi3:1).

Tusome,

Wafilipi 3:1 ‘Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni mambo yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi.

2 Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na WAJIKATAO’’.

3 Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili’.

Watu wanaojikata wanaozungumziwa hapo ni watu wa ‘Tohara’.. Yaani watu wanaofanya tohara, na hao si wengine Zaidi ya wayahudi.. limetumika neno ‘wajikatao’ kufuatia kitendo chenyewe cha Tohara, ambacho kilihusisha KUKATA sehemu ya nyama ya mbele ya viungo vya uzazi vya wanaume..

Wayahudi hawa wajikatao waliwashurutisha watu wa Mataifa, waliomwamini Mwokozi Yesu, kuwa nao pia wanapaswa watahiriwe kama wao, kulingana na Torati. Na kwamba kama hawatatahiriwa basi Mungu hatawakubali. Ikiwa na maana kuwa kigezo cha mtu kukubali wana Mungu ni kufanyiwa tohara ya mwilini.

Jambo ambalo sio kweli kwa kipindi hichi cha agano jipya.. Katika agano jipya, tohara inayokubalika na Mungu si ya mwilini tena, bali ni ya rohoni, katika mioyo yetu, ambayo tohara hiyo ni UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU.

Roho Mtakatifu anapokuja ndani yetu, baada ya kumpokea Yesu na kutubu, anachofanya ni kuondoa sehemu ya uovu iliyoongezeka katika roho zetu, kama vile tohara ya mwilini inavyoondoa sehemu ya nyama iliyoongezeka…

Kadhalika Roho Mtakatifu anaondoa kiburi kilichoshikamanika na sisi tangu kuzaliwa, anaondoa uongo ulioshikamanika na sisi tangu kuzaliwa, anaondoa tamaa mbaya, na kila aina ya dhambi.. na kutufanya kuwa kiumbe kipya.

Kwahiyo kama vile katika Agano la kale mtu yeyote ambaye hakutahiriwa katika Mwili hakuwa mtu wa Mungu, kadhalika katika agano jipya mtu yeyote asiyetahiriwa katika roho, (maana yake asiye na Roho Mtakatifu), maandiko yanasema huyo sio wa Mungu.

Warumi 8:9 ‘Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, HUYO SI WAKE’.

Kwahiyo Mtume Paulo, aliwaonya wakristo ambao si wayahudi, kuwa Kutahiriwa katika mwili (yaani kujikata) si tiketi ya kukubaliwa na Mungu, Maana yake yule mtu aliyetahiriwa katika mwili na yule ambaye hajatahiriwa wote mbele za Mungu ni kitu kimoja…

Wagalatia 6:15 ‘Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya’.

Warumi 2:29 ‘bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu’.

Hiyo inatufundisha kuwa tujitahidi kwa hali na Mali kuzaliwa mara ya pili, kwasababu Bwana Yesu alisema, mtu yeyote asipozaliwa mara ya pili na kuwa kiumbe kipya hawezi kuuingia ufalme wa mbinguni.

Na kuzaliwa mara ya pili ni kumwamini Yesu, na kubatizwa katika ubatizo sahihi kwa maji mengi na kwa jina la Yesu, na kupokea Roho Mtakatifu.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

Mlima wa Mizeituni  unaumuhimu gani kwetu?

Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni  ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments