Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?

Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?

SWALI: Biblia inasema mshahara wa dhambi ni Mauti, (Warumi 6:23) je wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?

Jibu: Ni vizuri kufahamu kuwa katika maandiko kuna Mauti za aina mbili. Mauti ya kwanza ni mwili uliokufa na kutupwa katika kaburi!, na mauti ya pili ni roho kutupwa katika ziwa la moto.

Bwana Yesu alisema maneno haya..

Mathayo 10:28  “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum”

Umeona?, mwili unaangamizwa katika dunia hii, ndio hapo mtu anakufa na mwili wake kuzikwa,  lakini roho ni katika jehanamu ya moto…  Hii mauti ya pili ya kuiangamiza roho katika ziwa la moto, ndio mshahara wa dhambi biblia inayoizungumzia katika Warumi 6:23

Warumi 6:23 “KWA MAANA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”

Hivyo mshahara wa dhambi ni Mauti ya Pili, na si ya kwanza, Katika mauti ya kwanza watakatifu wengi wamekufa, wataendelea kufa wengi.. lakini watafufuliwa na kuurithi uzima wa milele, hivyo biblia haikumaanisha kabisa mauti ya mwili huu kuwa ndio mshahara wa dhambi, vinginevyo mpaka sasa kungekuwa hakuna mwenye haki. Maana watakatifu wote waliotangulia tayari wamekufa!. Kwahiyo mauti iliyomaanishwa hapo katika Warumi 6:23 ni MAUTI YA PILI, yaani lile ziwa la moto, mahali roho ya wanadamu waovu zitakapoangamizwa..

Sasa labda unaweza kuuliza ni wapi tena katika maandiko, pametajwa mauti hii ya pili kuwa ni katika ziwa la moto..

Tusome..

Ufunuo 20:14 “Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.

15  Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”

Hivyo hatuna budi kujitenga na dhambi!, kwa kadri tuwezavyo ili tusije tukakubwa na mauti ya pili kwa kutupwa katika lile ziwa la moto, kama maandiko  yanavyosema..

Ufunuo 2:11 “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya MAUTI YA PILI”.

Lakini kama hatutaishinda dhambi, kwa kumwamini Yesu, na kutubu na kubatizwa katika ubatizo sahihi na wa kimaandiko, basi tufahamu kuwa, mshahara wake utakuwa ni Mauti ya piil, ambayo ndio ziwa la moto..kama Bwana alivyosema..

Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, SEHEMU YAO NI KATIKA LILE ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. HII NDIYO MAUTI YA PILI”.

Je umempokea Yesu?, kama bado unangoja nini?, je unatamani kukumbwa na mauti ya pili?.. je unatamani kuingia jehanamu ya moto..mahali ambapo utateswa usiku na mchana, kwa maangamizi ya milele?

Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho na Bwana Yesu yupo mlangoni sana kurudi!.. siku yoyote parapanda inalia na ngano zitakusanywa ghalani, na magugu yote yatakusanywa na kwenda kuchomwa moto.

Bwana azidi kutubariki.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Nini maana ya “Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai?

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

OLE WAKO KORAZINI NA BETHSAIDA.

Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments