Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe daima, karibu tujifunze Biblia Neno la Mungu wetu lililo taa ya miguu yetu na Mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).
Maandiko yanatuonyesha kuwa si lazima watu wote wanene kwa lugha (1Wakorintho 12:30 na 14:23), kana kwamba ndio uthibitisho pekee wa mtu kuwa wa kiroho…lakini pia kuna faida kubwa ya kunena kwa lugha ikiwa mtu atajaliwa hilo.
Na pia kunena kwa lugha si jambo ambalo mtu anaweza kuamua, kwamba sasa naanza kunena, la! Kunena kwa lugha ni msukumo ambao Roho Mtakatifu anaushusha ndani ya mtu pasipo mtu kutaka au kupanga!.. Ni kama mtu anavyopokea unabii, au anavyopokea ndoto au maono.. hakuna mtu anayeweza kupanga unabii au maono au ndoto (labda awe nabii wa uongo)!.. kwani mambo hayo yanakuja tu yenyewe kutoka kwa Mungu, kwajinsi apendavyo Mungu… Na kunena kwa lugha ni hivyo hivyo, si lazima iwe kila siku au kila saa, bali ni wakati maalumu tu ambao Roho atalishusha jambo hilo ndani ya mtu.
Sasa zipo lugha za wanadamu, na vile vile za Malaika (Soma 1Wakorintho 13:1), Zozote kati ya hizo mtu aliyejazwa Roho anaweza kuzinena. Na zote zina faida katika kuzinena… Katika kunena lugha za wanadamu ni pale ambapo mtu haijui lugha Fulani ya jamii fulani ya watu, lakini ghafla anajikuta anaanza kuizungumza ile lugha vizuri sana.. Vile vile katika kunena lugha za malaika, ni pale ambapo anajikuta anazungumza lugha ambayo ni mpya kabisa isiyotumiwa na wanadamu mahali popote.
Na maneno anayoyazungumza yanakuwa aidha ni maneno ya unabii, au maonyo au ya kumsifu Mungu.. kwahiyo kama ni ujumbe kwa kanisa ni lazima awepo mfasiri..
Vile vile kama ni lugha Mpya inayozungumzwa, maana yake ambayo haitumiki na jamii yoyote ya wanadamu, na ni ujumbe kwa kanisa, basi anahitajika pia mfasiri, lakini kama mtu yupo katika maombi yake binafsi na lugha hiyo ikamjia ndani yake, basi hapo hahitaji mfasiri bali anakuwa ananena maneno ya siri na Mungu wake.
Na leo tutaangalia faida moja kubwa ya kunena lugha mpya, uwapo wewe binafsi katika maombi yako ya faragha.
MAZUNGUMZA YAKO YANAKUWA NI YA SIRI.
Hii ndio faida kuu na ya kwanza. Kikawaida mazungumzo ya siri yanakuwa na upinzani mchache kuliko mazungumzo ya wazi!.. na njia mojawapo ya kuficha mazungumzo ni kutumia lugha nyingine!..
Kwamfano utaona Waarabu wawili, au Wachaga wawili, au wamasai wawili, au wasukuma wawili, wanapokutana mahali Fulani ili waongee kwa uhuru zaidi utaona wanatumia lugha zao za asili , lengo ni kuficha mazungumzo na pia kuzungumza mambo yao yale mambo ya ndani kwa uhuru zaidi.. watu walio kando kando inakuwa ngumu kuelewa na hivyo wazungumzaji wanakuwa wamefunga milango mingi.
Na sisi tunapozungumza na Mungu wetu, KUNA WAKATI TUNAHITAJI USIRI.. Maneno yetu tunayoyazungumza si lazima yaeleweke na watu wa kando yetu au na mapepo katika ulimwengu wa roho. Ili kuzuia vita visivyokuwa na msingi.
Shetani asipoelewa kile tunachoomba kwa Mungu, inamwia vigumu kwake kupanga mashambulizi, kwasababu hajui ni nini tunamwomba Mungu kwa wakati huo, hivyo anabaki tu hapo katikati, lakini akisikia unamwomba Mungu akupe Amani, au akupe riziki Fulani, tayari na yeye kashajua ni eneo gani aende kukupiga vita ili usipokee kile ulichomwomba Mungu. Ndio maana Mtume Paulo kwa ufunuo wa roho aliliona hilo na akawaandikia watakatifu..
1Wakorintho 14:2 “Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake”.
Hivyo usijizuie kunena kwa lugha kama umejaliwa hilo.. itakusaidia kuzuia vita vingi katika ulimwengu wa mwili na wa roho.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE.
JIBU: Maandiko hayaweki wazi ni katika umri gani Yeremia aliitwa isipokuwa watafiti wengi ya Biblia wanakadiria Yeremia aliitwa katika umri wa miaka 20, au chini kidogo ya hapo, pengine 17
Biblia inachosema tu..alipoitwa aliitikia kwa kusema mimi ni MTOTO…Ikiwa na maana kuwa alijiona umri wake ulikuwa bado haujakidhi vigezo vya kumtumikia Mungu..
Yeremia 1:4 “Neno la Bwana lilinijia, kusema, 5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. 6 Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto. 7 Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru”.
Na hiyo pengine kwasababu aliona historia ya manabii wengi walioitwa walikuwa tayari ni watu wazima,
Pili Yeremia yeye alizaliwa katika familia ya kikuhani, na alijua umri wa kuhani kutumika Mungu ni kuanzia miaka 25 na kuendelea sawasawa na (Hesabu 4:3). Hivyo huwenda yeye hakuwa katika umri huo, ndio maana akawa na ujasiri wa kumwambia Mungu mimi bado ni mtoto.
Hivyo na sisi tunajifunza nini?
Kwa Bwana hakuna umri maalumu au wakati maalumu wa kuitwa..Uonapo unavutwa umwamini Yesu, saa hiyo hiyo itikia wito huo, kama Yeremia, neema hiyo haitadumu milele. Ikiwa utapuuzia kwa kusema Aah, Muda bado ngoja kwanza nifikishe umri Fulani, ngoja kwanza nijenge nyumba, ngoja kwanza nipate kazi, ngoja kwanza niondoke kwa wazazi. Fahamu kuwa una dalili kubwa ya kuipoteza neema ya Mungu. Saa ya wokovu ni sasa, wakati uliokubalika ndio huu. Maneno ya Mungu yanapokuchoma, tambua huo ndio wakati wako. Itikia sauti hiyo, badilika, tumika, tii. Na Bwana atayashughulikia hayo yaliyosalia.
Bwana akubariki
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?
Raheli aliwalilia vipi watoto wake?
Historia ya wimbo wa tenzi – Ndio dhamana Yesu wangu
Je ni kweli miaka yetu ya kuishi ni 80 tu (kulingana na Zaburi 90:10).
Nabii Elisha alikuwa ana maana gani kulia na kusema”Gari la Israeli na wapanda farasi wake”?
Ikiwa unafanya matendo mazuri yanayompendeza Mungu, basi mshukuru Mungu kwa hayo lakini USIJISIFU wala kujigamba hata kidogo kwa hayo. Kwasababu wakati unadhani kuwa umefanya 100 yanayompendeza Mungu kwa siku moja, yapo mengine 200 uliyoyafanya yasiyompendeza Mungu, kwa kutokujua.
Laiti tukifunguliwa macho na kuona makosa yetu yote tunayoyafanya bila sisi wenyewe kujua, tusingeendelea kujitamani hata kidogo, tusingeendelea kujivuna, tusingeendelea kujisifia vimema vichache vichache tunavyovitenda kwa siku!!!…Kwaufupi maisha yetu yamejaa makosa mengi kuliko mema!, hata kama tutajiona kama tuna mema mengi kuliko kasoro.. Lakini uhalisia utabakia pale pale kwamba makosa yetu yamezidi mema yetu..
Kwahiyo kama Mungu ni wa haki, basi ni haki yake atulipe mabaya mengi kuliko mema.
Kama ukimlazimisha Mungu akuhese haki ya kukubariki kwa sadaka yako uliyotoa jumapili, vile vile anapaswa akuhesabie haki ya kuadhibiwa kwa mawazo yako ya kutamani na kwa hasira uliyomwonea ndugu yako siku hiyo hiyo ya jumapili. Na maandiko yanasema mtu amwoneaye ndugu yake hasira ni mwuaji, kwahiyo unapaswa uhukumiwe kama mwuaji..
Lakini kama hutaki Mungu atazame udhaifu wako huo na hutaki akuadhibu kwa makosa yako basi usilazimishe akulipe kwa matendo yako mazuri unayomfanyia. Bali kinyume chake nyenyekea!!!.. Fanya tu yakupasayo kufanya sawasawa na Luka 17:10.
Luka 17:10 “Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya”.
Na kama tukiingia mkataba huo na Mungu wa kupokea haki yetu kwa matendo yetu, basi tunazo sababu nyingi za kulipwa mabaya kuliko mema. Kwasababu Mungu siku zote ni wa haki.
Lakini kama mara nyingi Mungu anatuvumilia kwa mabaya yetu tunayoyafanya sawasawa na Zaburi 130:3 “Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe”…basi na sisi hatuna budi kutoyatumainia mema yetu tunayoyafanya!.
Ndio hapa sasa panazaliwa kitu kinachoitwa NEEMA!... Neema tafsiri yake ni upendeleo maalumu usiokuwa na sababu. Kwamba unapokea tu kitu kutoka kwa Mungu pasipo matendo yako.. Yaani Mungu anapenda tu kukupa si kwasababu wewe ni mtenda mema, au ni mwombaji sana, au ni mfungaji sana, au ni mhubiri mzuri… La!, bali anakutendea tu mema bila kwa upendo wake tu!, na huruma zake na kupenda kwake.
Ndio maana hatuna budi kila siku KUOMBA NEEMA YA MUNGU ije juu yetu. Kwasababu tukiipata hiyo tumepata kila kitu.
Usijivune, bali omba neema kwasababu Mungu huwapinga wenye kiburi na kuwapa wanyenyekevu Neema yake (1Petro 5:5).
Afya uliyonayo ni kwa neema tu, Uzima ulio nao ni kwa Neema tu, karama uliyo nayo ni kwa neema tu, zaidi sana hata Wokovu ulio nao ni kwa Neema tu na wala si kwa matendo yako.
Waefeso 2:8 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”
Na zaidi ya yote pia Roho Mtakatifu tunampokea kwa Neema..
Wagalatia 3:2 “Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani”
Omba Neema!!.. omba Neema!, Omba Neema…usitumainie matendo yako..
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.
Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?
Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe.
Karibu tujifunze biblia, leo tujikumbushe historia fupi ya tafsiri ya biblia ya King James.
King James au kwa Kiswahili “Mfame Yakobo” wa Uingereza, alikuwa ni mmoja wa wafalme ambao hawakuwa maarufu sana kwa wakati wao. Lakini alikuja kufanya jambo la kishujaa ambalo mpaka leo yupo katika rekodi ya watu maarufu na wakihistoria waliowahi kutokea Uingereza.
Mwaka 1604 baadhi ya wanazuoni wa Kiprotestanti (Wapuriti) walipendekeza kuchapishwa kwa tafsiri mpya ya biblia, kuchukua nafasi ya ile iliyokuwepo ambayo ilijulikana kama tafsiri ya “Geneva”. Tafsiri ya Geneva ndio ilikuwa tafsiri ya kwanza kwa lugha ya kiingereza kuchapichwa huko Ulaya, iliyotumiwa na Waprotestanti.
Upungufu wa tafsiri hiyo ya Geneva, ni kwamba ilikuwa ina “maoni ya ziada” yaliyoongezwa ili kutilia mkazo kile kilichoelezwa katika biblia, na maoni hayo ya mkazo, yalilenga sana kuwakosoa viongozi wa kisiasa na kidini.
Hivyo baadhi ya waprotestanti hao, jamii ya Wapuriti, walitoa mapendekezo yao kuchapiswa biblia nyingine ambayo itaondoa hayo maoni ya watu na kuiacha yenyewe kama yenyewe, pasipo maoni ya watu. Na pia chapisho hilo litalenga pia kuitafsiri biblia nzima katika kingereza kizuri zaidi.
Wapuri hao baada ya kutoa hilo pendekezo, walilifikisha kwa Mfalme ambaye alikuwa anaitwa YAKOBO (King James).
Kikawaida wafalme wengi huwa hawajihusishi na masuala ya kiimani, zaidi sana huwa wanayapinga, lakini ikawa ni kinyume chake kwa huyu King James, badala ya kulipinga au kulikosoa wazo lao, yeye alikubali biblia mpya hiyo ichapishwe na tena akatoa sehemu kubwa ya hazina ya utajiri wake kusaidia zoezi zima la utafsiri mpya.
Tafsiri hiyo mpya ya Biblia hiyo mpya iliandaliwa kwa kipindi cha Miaka 7, na wanazuoni zaidi ya 47 kutoka kila mahali, Uingereza. Walianza kuitafsiri biblia upya kutoka katika Lugha ya kigiriki kwa agano la kale, na kiaramu kwa agano jipya. Walipomaliza kuitafsiri biblia yote wakaiita biblia hiyo KING JAMES BIBLE, Yaani biblia ya Mfalme Yakobo.
Baada ya kumaliza kutafsiri, kazi ile ilionekana kama dhaifu sana, lakini muujiza ni kwamba ndani ya kipindi kifupi, tafsiri hiyo mpya ya King James, ilianza kupendwa na watu wengi, kwani haikuwa na mchanganyiko wa maoni ya watu, na ilikuwa na kiingereza kikamilifu na haikuongeza neno wala kupunguza Neno.
Kufikika Mwaka 1611, tafsiri ya King James ilikuwa imeshasambaa katika bara la Ulaya yote, na baadaye duniani kote. Na tangu mwaka huo wa 1611 mpaka leo karne ya 21 ndio kitabu kinachoongoza kwa kuuzwa kuliko vitabu vyote duniani, na kumfanya Mfalme James, kuendelea kushika nafasi za juu za watu maarufu waliowahi kutokea.
Ni nini tunajifunza katika Mfalme Yakobo (King James).
Ni Mfalme ambaye alikuwa na hofu ya Mungu, ingawa hakuwa mkamilifu sana, lakini alitii na kuheshimu pendekezo la watu wa Mungu, ambao walimshauri aridhie ombi la kukitakasa kitabu kitakatifu cha Bwana, kwa kuondoa maoni ya watu na kukiacha kisafi kama kilivyo.
King James, aliruhusu pendekezo hilo pasipo kujua kuwa litaenda kuubadilisha ulimwengu. Mpaka Leo hii tafisiri bora ya kiingereza inayosomwa na wengi ni tafsiri hiyo ya King James. Na kwa kufanya hivyo Bwana akampa King James kumbukumbu la daima.
Ni wafalme wengi na mamalkia wengi wamekuja na kupita, wameandika vitabu lakini vitabu vyao vimepita, lakini kazi ya James mpaka leo inadumu na itaendelea kudumu hivyo mpaka Kristo anarudi.
Na sisi tukitaka tupate kumbukumbu la kudumu hatuna budi kumfikiri Mungu kwanza katika maisha yetu, haijalishi ngazi tuliyopo tuwe maskini, matajiri, tuwe wafalme tuwe watu wa kawaida.. tukimjali Bwana kwa mioyo yetu yote, na akili zetu zote na nguvu zetu zote, bali tuna kumbukumbu kubwa mbele zake si tu katika maisha haya, bali hata yale yajayo.
Malaki 3:13 “Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani?
14 Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za Bwana wa majeshi?
15 Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.
16 Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake.
17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye”.
Bwana atubariki.
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Dina akatoka kuwaona binti za nchi. (Mwanzo 34:1)
Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.
WHAT DOES IT MEAN TO BE A CHRISTIAN?
Je ni viatu gani Musa aliambiwa avivue? Vya mwilini au vya rohoni? (Kutoka 3:5).
NI UTUKUFU WA MUNGU KUFICHA JAMBO.
Tusome,
Mithali 13:2 “Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake; Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri”
Haini ni jina lingine la mtu ambaye ni “Msaliti”, mtu anayefanya usaliti juu ya mwingine ni sawa na kafanya “Uhaini”. Mtu anayeisaliti nchi yake mtu huyo ni Mhaini, vile vile mtu anayeisaliti Imani yake yenye kumfikisha mbinguni, kwa kurudia mambo machafu mtu huyo anafanya uhaini kwa Mungu wake.
Zaburi 78:57 “Bali walirudi nyuma, wakahaini kama baba zao; Wakaepea kama upinde usiofaa
58 Wakamkasirisha kwa mahali pao pa juu, Wakamtia wivu kwa sanamu zao.
59 Mungu akasikia, akaghadhibika, Akamkataa Israeli kabisa.”.
Na maandiko yanazidi kuonyesha kuwa Wahaini wote wa imani watapata adhabu..
Zaburi 119:158 “Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa, Kwa sababu hawakulitii neno lako”.
Mithali 22:12 “Macho ya Bwana humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini.”
Soma pia Mithali 13:15 na Zaburi 25:3.
Kama tayari ulikuwa umeyakimbia machafu ya ulimwengu, na sasa umeyarudi nyuma fahamu kuwa huo unafanya uhaini mbele za Mungu, kimbia haraka sana msalabani ukatubu, kama ulikuwa umeacha uzinzi na sasa umeurudia, tubu kwa machozi sana mbele za Bwana, leo hii ni nafasi yako ya kutubu na kumgeukia Mungu, usingoje kesho, na hakikisha unatubu kwa kumaanisha kabisa kutofanya hayo uliyoyafanya au unayoyafanya, na Bwana atakupokea lakini ukizidi kukawia upo hatarini sana…
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
Je ni kweli kila nafsi itaonja mauti kulingana na (Zaburi 89:48)?
USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.
MAGONJWA YAKUPATAYO MARA KWA MARA.
Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo.
Naamini kuwa ulishawahi kusoma katika maandiko kuwa kuna mahali Yesu alilala. Lakini ulishawahi kujiuliza ni kwanini habari ile iandikwe kulikuwa na umuhimu gani?
Kumbuka kila tukio lililoandikwa katika biblia limebeba somo kwetu sisi watakatifu.
Jambo pekee lililomfanya Yesu alale usingizi mzito namna ile, sio kuchoka kama wengi wanavyodhani, kuna nyakati nyingi Yesu alikuwa anachoka kuliko hata hapa, lakini alikuwa halali, anapanda mlimani kuomba…lakini ni nini kilichompelekea alale?
Jambo lililompa Yesu usingizi mzito, ni ile DHORUBA iliyoanza kule baharini.
Marko 4:36-39
[36]Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.
[37]Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.
[38]Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?
[39]Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
[40]Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?
Umeona hapo, hakuna mahali popote biblia inarekodi Yesu alipitiwa na usingizi, isipokuwa hapo kwenye dhoruba kuu.
Wakati wengine wanahangaika na matatizo, hawapati usingizi, wanapambana na changamoto zao..upande wa pili wa Yesu mambo ni tofauti,kule kuyumba kwa chombo kumbe ndio kulikuwa kunavuta usingizi vizuri.
Lakini ni nini Bwana anataka tujifunze juu ya tabia hii ya Kristo?
Ni kwamba hata yeye akiwa amejaa vizuri ndani yetu, tutadhihirisha tabia kama zake.
Ni kwanini leo hii tuna hofu ya maisha, tuna hofu ya kesho, tutaishije, tutakula nini, tutavaa nini? tuna hofu ya wezi, tuna hofu na kufukuzwa kazi, tuna hofu ya magonjwa?
Ni kwasababu Kristo hajajaa ndani yetu vizuri, ni kwasababu hatujapokea uhakika wa kuwa salama daima.
Wakristo wengi, wakiwa kwenye matatizo, mbalimbali hawana raha, wanapoteza utulivu..wanahangaika huku na kule kama wakina Petro. Hii ni hali ya kawaida ya kibinadamu. Lakini Yesu anaweza kukupa usingizi katikati ya tufani na dhoruba..endapo atajaa ndani yako vizuri.
Unachopaswa kufanya ni jiachie tu kwa Yesu, mwache yeye ahangaike na hiyo tufani, itaisha tu yenyewe, haitadumu muda mrefu, atakufungulia mlango wa kutoka katika hilo jaribu, haijalishi ni kubwa kiasi gani.
Jiachie tu kwa Yesu mtafakari yeye muda wote, muwaze yeye na uweza wake, Kama hujaokoka, hakikisha unafanya hivyo sasa, hivyo kwa jinsi utakavyokuwa unaendelea kumsogelea yeye ndivyo atakavyokupa wepesi kwa kukabiliana na mambo yote, na changamoto zote unazokutana nazo..Na hatimaye zitaisha tu bila hata kusumbuka kwasababu yeye yupo kazini.
Mkaribie Yesu sasa acha kuzitegemea akili zako mwenyewe..Naye atakusaidia, yeye mwenyewe anasema;
Mathayo 11:28-29
[28]Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
[29]Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu
Anasema pia..
Mathayo 6:31-34
[31]Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
[34]Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Mkaribie Yesu, Akutue mizigo. Akupe uzingizi, akupe raha.
Zaburi 127:2 “Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi”
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
FAHAMU JINSI KRISTO ANAVYOPONYA WATU ROHO.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
NA WATU WOTE WALIKUWA WAKIAMKA MAPEMA, WAENDE HEKALUNI.
Dia ni nini katika biblia? (Mithali 13:8)
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
KATAA KUWA EUTIKO, WA KUSINZIA IBADANI.
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
Jibu: Tusome,
Mithali 13:8 “Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake; Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote”.
Dia ni Kiswahili kingine cha neno “Fidia”, Kwahiyo hapo biblia inaposema “Dia” ya nafsi ya mtu ni utajiri wake, na maskini hasikii ogofyo lolote, maana yake ni kwamba “Fidia ya mtu anapokutana na matatizo ni itatoka katika vitu alivyonavyo” ikiwa na maana kuwa mtu anapokutwa na tatizo labda kasababisha hasara Fulani au kafanya kosa Fulani katika jamii, lililomsababishia apigwe faini, au kakutana na watu na kaingiliwa na wahalifu katika nyumba yake, basi Mali alizo nazo zinaweza kuwa fidia kwaajili ya uhai wake, maana yake anaweza kuwapa wale watu sehemu ya mali zake na akaisalimisha roho yake.
Lakini mtu asiye na kitu kabisa (yaani Yule maskini kikweli kweli), huwa hawezi kupokea vitisho vyovyote, hakuna jambazi yeyote anayefikiria kwenda kuvunja nyumba ya maskini akiwa na mtutu ili amwibie mali zake.. Ikiwa na maana kuwa, maskini siku zote yupo huru!.. hafuatiliwi na mtu, wala hakuna mtu ana habari na maisha yake (hapokei ogofyo lolote).
Ni hekima gani tunaipata hapo? Au ni nini tunajifunza hapo?
Ili tuelewe ni nini tunajifunza hapo, hebu tuanzie kusoma kuanzia mstari wa 7
Mithali 13:7 “Kuna mtu mwenye kujitajirisha, lakini hana kitu; Kuna ajifanyaye kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.
8 Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake; Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote”
Hii ni hekima ambayo inaweza kutusaidia kuwa salama..sio lazima tuwapo na mali, tujionyeshe kuwa na mali kwa watu!, ndio maana hapo biblia inasema “kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.”.. Unapokuwa mtu wa kujionyesha mbele za watu mali ulizo nazo, unajiweka katika hatari ya kutoa DIA (Fidia) kwaajili ya uhai wako, kwasababu kila mtu atatamani hizo mali ulizo nazo, utavutia watu waovu na wasio waovu, utavutia majambazi, utavutia wenye mamlaka na watu wapendao rushwa n.k
Hivyo hekima ni kujiweka katika maisha ya wastani, hata kama unazo mali nyingi, si lazima ujulikane wewe ni tajiri kuliko wote.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Azidishaye mali yake kwa riba, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.
Nini maana ya ampokeaye Nabii atapata thawabu ya Nabii? (Mathayo 10:41).
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
Watu wa kale walitumia wino, na kalamu pamoja na karasati kuweka kumbukumbu zao kama tunavyofanya sasa..
Isipokuwa wino wao, kalamu zao na karatasi zao zilikuwa tofauti na hizi tunazotumia sasa..
Mtume Yohana katika nyaraka zake aliandika hivi;
3 Yohana 1:13
[13]Nalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu.
Kuonyesha kuwa unandishi wao ulitegemea wino na kalamu, kama tu huu wetu.
Je! Wino wa kale ulitengenezwaje?
Tofauti na huu wa kwetu unaotengenezwa na kemikali mbalimbali..wino wa zamani ulikuwa unatengenezwa na MASINZI. Masinzi hayo yalikuwa yanavunwa aidha kutoka katika mafuta yaliyochomwa au kuni pale yanapoganda katika chombo kama sufuria kwa pembeni.
Sasa yalipokusanywa kama poda, baadaye yanachanganywa na gundi inayotoka katika mmea wa mpira..lengo la kufanya hivyo ni kuufanya wino huo ushikamane vizuri ili wakati wa uandishi wino usitapakae ovyo.
Hivyo mwandishi anapoununua wino huo anachofanya ni kuchanganya na maji, kisha kutumia kalamu yake kuchovya na kuandika katika hilo karatasi lao.
Je! Kalamu zao ziliundwaje
Tofauti na kalamu zetu hizi, ambazo zinatengenezwa kwa mirija ya pastiki na chuma. Kalamu za zamani ziliundwa na mmea ujulikanao kama MWANZI ambayo hata huku sehemu kadhaa hutumika.. Mianzi hii ilichongwa kwa pembeni kuacha ncha. Ili kuruhusu wembambea wa uandishi katika karatasi kama tu kalamu zetu za kisasa zilivyo.Tazama picha.
Je karatasi za kale zilikuwaje?
Karatasi za zamani zilfanana hizi isipokuwa zrnyewe zilikuwa ni nene, ziliundwa na mmea ujulikanao kama mafunjo(Ayubu 8:11).
Mmea huu ulichongwa kulingana na ukubwa wa karatasi, kisha kuchanjwa chanjwa katika vipisi vidogo, ambavyo baaadaye vililowekwa katika maji ili vilainike..kisha vinawekwa katika ubao ulionyooka, kisha vinalazwa kipisi kimoja baada ya kingine, na vingine kupita kwa kukatiza..kisha panawekwa ngozi ya mnyama kwa juu , na baada ya hapo kukandamizwa, ili vipisi hivyo vishikane,
Na kuachwa siku kadhaa, baadaye wakitoa, tayari karatasi hiyo nene hutokea… ngumu na imara kuliko hata hizi tulizonazo sasa. Ndizo walizotumia watu wa kale kuandikia.
Bwana akubariki.
Je! Umeokoka? Je! Unatambua kuwa unyakuo wa kanisa upo karibu? Umejiandaaje? Ikiwa bado hujafanya hivyo na unahitaji msaada huo, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi;
Maran Atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.
Kaniki ni nini katika biblia? (Yeremia 8:21).
KALAMU YENYE UONGO YA WAANDISHI IMEIFANYA KUWA UONGO.
Zaburi 147:3 Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao. 4 Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina. 5 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka.
Ukitazama juu unaona nyota nyingi sana zisizo na idadi, mbali na hizo zilizo ndani ya upeo wa macho yetu, lakini pia zipo nyingine tusizoziona ambazo idadi yake ni mabilioni kwa mabilioni, matrilioni kwa matrilioni,..
Lakini hapa Mungu anatupa siri ya uweza wake, anasema zote hizo amezihesabu na kuzipa majina,..
Sasa Kwanini atuambie jambo kama hilo?
Ni kutuaminisha kuwa ikiwa anazifahamu nyota zote zilizo mbali, nje-ndani, atashindwaje kutufahamu sisi? Atashindwaje kuziona taabu zetu na shida zetu, atashindwaje kuyaona mateso yetu na majeraha yetu?
Hivyo hapo anaposema ‘Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao’. Anamaanisha, huweza kutufanya upya, endapo tutamkaribia.
1Petro 5:7 ‘huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu’.
Mkaribie Kristo akuponye kwasababu yeye yupo karibu sana na wewe zaidi ya nyota za angani.
Utukufu na uweza vina yeye milele na milele amina.
Maombi Yangu:
“Baba mwema, tumeona uweza wako, juu ya ulimwengu wako uliouumba, kwamba hakuna lolote usilolijua,wala usiloliweza, na sasa ninakukaribia Baba wa Upendo, kama ulivyoahidi kwenye Neno lako kwamba utaziganga jeraha zangu, Naomba sasa niponye moyo wangu, na mwili wangu, nifanye upya tena, nisimame mbele zako, nikutumikie. Ni katika jina la Yesu naomba nikiamini. Amen.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?
MUNGU WETU, JINSI LILIVYO TUKUFU JINA LAKO DUNIANI MWOTE!
UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?
Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?
Mofa ni nini? na inafunua nini kiroho?(1Samweli 28:24).
NIMEOKOKA, ILA MUNGU NDIYE ANAYEJUA NITAKWENDA WAPI.
SWALI: Kwanini Mungu alimuadhibu Eli kwa kosa la kutowaonya watoto wake, angali tunasoma katika maandiko aliwaonya hapo kabla?
Tusome;
1Samweli 2:22 Basi Eli alikuwa mzee sana; naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi walivyolala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania.
23 Akawaambia, Mbona mnatenda mambo kama hayo? Maana nasikia habari za matendo yenu mabaya kwa watu hawa wote. 24 Sivyo hivyo, wanangu, kwa maana habari hii ninayoisikia si habari njema; mnawakosesha watu wa Bwana.
25 Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa Bwana, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu Bwana amekusudia kuwaua.
Lakini Hapa Mungu anasema…
1Samweli 3:12 Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli katika habari za nyumba yake, tangu mwanzo hata mwisho.
13 Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye HAKUWAZUIA.
14 Na kwa hiyo nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele.
JIBU: Kibiblia “Kuonya” sio tu kusema kwa mdomo, bali pia kuchukua hatua stahiki, endapo maonyo hayatatekelezwa. Eli ni kweli aliwaonya watoto wake, kwa dhambi walizokuwa wanazifanya madhabahuni pa Mungu, lakini aliendelea kuwaangalia, wakifanya mambo yao maovu bila kuwaondoa katika nafasi zao. Ndio maana hapo kwenye 2Samweli3:13 Mungu anamwambia Samweli, kwamba HAKUWAZUIA. Hakuwaondoa katika kazi ya utumishi, Pengine kwasababu ni watoto wake, warithi wake, akawastahi zaidi ya Mungu. Hivyo wakati wa adhabu ulipofika yeye naye alishiriki adhabu ile.
Hili ni funzo, pia kwa viongozi wote wa imani, nyakati hizi tunazoishi, kanisa limegeuzwa kama mahali pa kila mtu kujiamulia jambo lake, na viongozi wanaona wanafumbia macho. Utakuta mchungaji ni mzinzi, lakini askofu akipata taarifa, badala wamwondoe katika ofisi ile, wanamwonya tu, kisha wanamuhamisha dayosisi, wanamstahi, na akifika kule anaendelea na maovu yake, anahamishwa tena dayosisi.
Utakuta watoto wa wachungaji, ni walevi, hawana maadili, lakini wanaendelea kubaki katika nafasi za wazee wa kanisa au waimbaji kwaya. Mchungaji akiambiwa, anachokifanya ni kuwaonya tu, lakini bado wanaendelea kushika nafasi hizo za madhabahuni. Hii ni hatari. Mungu anataka hatua stahiki zifuatane na maonyo kama hakuna mabadiliko.
Hivyo kama wewe ni kiongozi, kumbuka maonyo yako ni lazima yaambatane na vitendo.
Bwana atusaidie.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kwanini Kuhani wa Mungu Eli alikufa kwa kuvunjika shingo?
NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.
NI NINI KINATOKA KINYWANI MWA MTOTO WAKO?
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?