Kujazi maana yake ni kulipa.
Kwamfano tusome Neno hilo jinsi lilivyotumika na kumaanisha katika maandiko;
Mathayo 6:2 “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. 3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; 4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Mathayo 6:2 “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Maana yake ni kwamba, unapokuwa mtu wa kutoa sadaka bila kuwa na nia ya kuonekana mbele za watu, basi Mungu atakulipa kwa utoacho.
Mathayo 6:6 “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Mathayo 6:17 “Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; 18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Mathayo 6:17 “Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Vilevile unapokuwa mtu wa kuomba na kufunga, lengo lako likuwa ni kujisogoza mbele za Mungu na sio kufanya mashindano, au kuonekana na watu kuwa ni wa kiroho sana, basi Mungu atakulipa kwa hicho ukifanyacho.
Ruthu 2:11 “Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikilia watu usiowajua tangu hapo. 12 Bwana akujazi kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake”.
Ruthu 2:11 “Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikilia watu usiowajua tangu hapo.
12 Bwana akujazi kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake”.
Tunaona pia hapa Boazi akimbariki Ruthu, kwa wema wake aliomfanyia mkwewe, na kumwambia Bwana akulipe kwa kazi yako njema.
Lakini ni ujumbe gani Bwana anapitisha katika haya?
Ni kuonesha kuwa hakuna tendo jema tutakalomfanyia Mungu asirudishe malipo, endapo tutafanya ipasavyo. Kama kweli utaomba mbele zake, utafunga kwa ajili yake, utamtolea sadaka zako, kama kweli utatenda wema wowote, fahamu kuwa hilo Bwana atakulipa tu kwa wakati wake, thawabu yako haitakupita.
Hivyo atukuzwe Mungu awezaye kutuona na kuturehemu na kutubariki. Sifa, heshima na utukufu vina yeye milele na milele. Amina.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Sadaka ya kutikiswa ilikuwaje?
Nini maana ya ampokeaye Nabii atapata thawabu ya Nabii? (Mathayo 10:41).
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)
HERI WAPATANISHI, MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU
Mapooza ni nini? Na je! Twawezaje kuepukana nayo?
Nini maana ya huu mstari? “Yeye mwenyewe ataokolewa lakini ni kama kwa moto”
Rudi nyumbani
Print this post