Nini maana ya ampokeaye Nabii atapata thawabu ya Nabii? (Mathayo 10:41).

Nini maana ya ampokeaye Nabii atapata thawabu ya Nabii? (Mathayo 10:41).

Je! Ni thawabu gani inayozungumziwa hapo?.

Jibu: Ili tuelewe vizuri, labda tuanzie kusoma kuanzia mstari wa 40

Mathayo 10:40 “Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.

41 Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki”

Sasa swali, ni thawabu gani inayozungumziwa hapo?..Jibu la swali hili tutalipata katika mstari unaofuata wa 42

Mathayo 10:42 “Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, HAITAMPOTEA KAMWE THAWABU YAKE”.

Kumbe thawabu inayozungumziwa hapo ni THAWABU KUTOKA KWA MUNGU kwa jinsi sisi tunavyowakaribisha watumishi wake!. Yaani kiwango utakachompimia Mtu wa Mungu,(yaani kumbariki) na jinsi utakavyomchukulia,  ndicho na Mungu pia atakachokupimia wewe!..

Kama umempokea Mtumishi wa Mungu, kama mtu wa heshima sana, na ukambariki sana.. Ndivyo Mungu na yeye atakavyokuchukulia wewe kama mtu wa Heshima sana, na mwenye kustahili thawabu nyingi.

 Lakini kama umempokea kama mtu wa kawaida, kwamba ni mtu mzuri tu!..basi na Mungu naye atakuchukulia wewe kama mtu mzuri tu, na kukupa thawabu kama hiyo hiyo uliyompimia huyo mtu wa Mungu.. Na kama umemlaani mtumishi wa Mungu, na Mungu naye atakulaani.

Bwana Yesu sehemu nyingine alisema maneno haya..

Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, NDICHO WATU WATAKACHOWAPA VIFUANI MWENU. KWA KUWA KIPIMO KILE KILE MPIMACHO NDICHO MTAKACHOPIMIWA”.

Unaona hapo?..anamalizia hapo kwa kusema, KIPIMO MPIMACHO NDICHO MTAKACHOPIMIWA!!..

Mfano wa Mwanamke aliyepata thawabu ya Nabii ni yule mwanamke wa Sarepta aliyemkaribisha Nabii Eliya na kumpikia chakula, ale..kwakuwa alimpokea yule kama Nabii na kumpa chakula, kama mtu wa heshima sana, Mungu naye akampa heshima kwa kulizidisha pipa lake la unga siku zote wakati Israeli yote ina njaa. (1Wafalme 17:9-16)

Kwahiyo na sisi tujitahidi siku zote kupima kipimo kizuri kwa watu wote, hususani walio watumishi wa Mungu, ili na sisi tupimiwe kipimo kilicho kikubwa na Mungu

Bwana atajalie tuwe miongoni mwa watu wa kubariki, ili na sisi tubarikiwe.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Nini maana ya huu mstari? “Yeye mwenyewe ataokolewa lakini ni kama kwa moto”

Nitamjuaje nabii wa Uongo?

Je Mungu anaweza kumdanganya mtu?

TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Prisca komba
Prisca komba
2 years ago

Amina

M
M
2 years ago

Ubarikiwe mtumishi wa Mungu