Mapooza ni nini? Na je! Twawezaje kuepukana nayo?

Mapooza ni nini? Na je! Twawezaje kuepukana nayo?

Mapooza ni kitu/vitu/mambo yote yasiyoweza kuzalisha chochote, au kufikia kilele chake cha kutoa matunda kamili.

Neno mapooza limetokana na neno kupooza. Kwamfano tunaposema mtu amepooza mkono, maana yake ni kwamba anao mkono lakini hana uwezo wa kufanya kazi ya mkono, yaana unakuwa kama vile umekufa tu lakini upo.

Nazi zote zinazotoka katika mti wa mnazi, si zote zinafaa kama kiungo, bali nyingine ni koroma, Sasa hizo koroma ndio mapooza yenyewe, japo kwa nje zinaonekana ni nazi.

Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi kwenye biblia;

Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,

13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.

6 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake”.

Katika habari hii ni Mungu anaifananisha ile siku ya Bwana, na kama mtini upukutishavyo mapooza yake. Yaani kama vile tunavyofahamu miti ya matunda, huwa si matunda yote yanakomaa wakati wa mavuno, bali kuna mengine huwa yanaendelea kubaki katika miti, hadi wakati wa msimu wa upepo mkali wa upukutishaji unapovuma ndipo yanapoondoka hayo yaliyosalia (ambayo ndio mapooza)..Hivyo siku ya Bwana ndivyo itakavyokuwa wakati ambapo Mungu anaiondoa mbingu, hakuna nyota hata moja itakayobakia juu.

Utalisoma pia, katika ile Habari ya Elisha..

2Wafalme 2:19 “Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza.

20 Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea.

21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.

22 Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.

Maana yake ni kwamba yale maji waliyokuwa wanayanywa au wanayatumia kwa mimea yalikuwa si mazuri yanazaa mapooza, yaani vitu vyake havistawi au kuleta matunda, mimba za wanawake zilikuwa zinatoka, mboga mboga zilizokuwa zinanyeshewa zilikuwa hazikuwi, ipasavyo, wala miti haikuivisha matunda yake,

Hivyo Elisha alipoagizwa na Mungu kutia chumvi katika yale maji, wakati ule ule yakaponywa. Hivyo kukawa hakuzaliwi mapooza tena katika ile nchi.

Utalisoma pia Neno hilo katika Ayubu 15:32.

Je, mapooza yapo hadi sasa?

Jibu ni ndio, kwamfano, wewe ni mwanamke halafu, kila unaposhika mimba, kabla hujajifungua inatoka, huwenda kuna mapooza nyuma yake.

Au unafanya shughuli Fulani, ambayo kwa muda mrefu sana, haijakuletea mafanikio yoyote, hayo pia ni mapooza,

Au unalihangaikia jambo lolote lile jema, lakini kwa muda mrefu, unaona kama kuna dalili njema zinaonekana lakini mwishoni linakufa. Ujue pia mapooza yapo hapo.

Una karama ya muda mrefu lakini haina matunda yoyote katika ufalme wa Mungu,

Je suluhisho ni nini?

Yapo mambo mawili makuu ya kuyafanya.. Hususani hili la kwanza, ukilipuuzia hili ukakimbilia hilo la pili, ufahamu kuwa hali yako haitaweza kuwa na mabadiliko.

  1. Jambo la kwanza, ni KUTIWA CHUMVI.

Kama vile Elisha, alivyoagizwa akatie chumvi ndani ya yale maji yaliyozaa mapooza, vivyo hivyo na wewe, huna budi kukubali kuwatiwa chumvi ili mapooza yaondoke ndani yako..

Hapa hatuzungumzii chumvi za upako, tunazungumzia Neno la Mungu. Mungu kumuagiza Elisha atie chumvi sio kwamba alikuwa anatuonyesha kuwa kuna upako ndani ya chumvi hapana, bali alikuwa anatoa taswira ya kufahamu chumvi ni nini katika ulimwengu wa roho, na sisi tunatiwaje chumvi..

Bwana Yesu alisema..

Marko 9:47 “Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;

48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.

49 Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto”.

Tafakari vema, jiulize, kwanini baada ya kutoa maagizo makali kama hayo, mwishoni akamalizia kwa kusema.. kila mtu atatiwa chumvi kwa moto..

Maana yake ni kuwa ili utiwe chumvi, huwezi epuka moto.. ili Maisha yako yaponywe, huwezi epuka kukata baadhi ya viungo vyako vinavyokukosea..

Viungo hivi ndio kama vipi..

  • marafiki wabaya: Watu wengi wana marafiki ambao, wamekuwa vyako vibaya vya kufikia maono yao. Wakikaa nao ni matusi, mashauri mabaya, kutenda dhambi n.k. Achana nao, wakimbie, ndio itauma kuwaacha lakini ndivyo chumvi inavyokuponya.
  • Kazi mbaya: Wapo watu ambao hawawezi kuishi bila kufanya biashara haramu, kuhonga, halafu muda huo huo anataka Yesu amsaidie, katika hiyo hiyo kazi, kamwe huwezi fanikiwa.

Hivyo hiyo ndio njia ya kwanza yenye matokeo.. Kataa kwa nguvu zote, kuacha watu/vitu/mambo ambayo yanakufanya usiwe safi mbele za Mungu.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba unapaswa uokoke kwa kumaanisha kabisa kumfuata Yesu Kristo. Hakikisha umejitwika msalaba wako. Hii ndio njia kuu ya kuondoa mapooza yoyote ndani yako.

        2.   Na jambo la pili baada ya hapo ikiwa tayari umeshajikana.. basi kinachofuata ni maombi ya uponyaji.

Hivyo nitaomba Pamoja na wewe.. Kisha kwa Imani Bwana atakufungua, wewe ambaye, tayari umeshampokea Yesu na kumfuata, au wewe ambaye unaahidi tangu sasa utafanya hivyo..

Hapo ulipo elekeza mawazo yako palipo na mapooza..kisha sema sala hii kwa sauti na kwa Imani, na kuanzia leo utaona mabadiliko yanakuja katika eneo hilo hilo unaloliombea..

PIGA MAGOTI, kisha sema maneno haya kwa sauti.

Mungu wangu, hakika nifahamu kuwa pasipo wewe mimi siwezi kuzalisha chochote, nami kama mwanao nakuja mbele zako, nikiomba msamaha unisamehe dhambi zangu zote, nilizokukosea, katika Maisha yako tangu nazaliwa. Nikakiri Yesu kuwa wewe ni Bwana na mwokozi na kiongozi wa Maisha yangu, wala Zaidi yako hakuna mwingine awezaye kuokoa. Tangu sasa naomba unifanye kiumbe kipya, na jina langu uliandike  katika kitabu cha uzima, unipe uwezo wa kufanyika mwana wako kweli kweli, nami nimekubali tangu sasa kutiwa chumvi kwa maneno yako Bwana Yesu. Nakubali kuacha mambo/watu/vitu vyote viovu visivyokupendeza wewe bila kujali vitanigharimu kiasi gani.Najua wewe ni mwaminifu na utanisaidia, sawasawa na Neno lako ..Naomba Bwana unione tena katika hii shida yangu na uniponye (Taja eneo lako la mapooza). Asante Bwana Yesu kwa kuniponya.Naombi nikimaini. Amen.

Basi kama umeifuatisha hiyo sala ya Imani.. Fahamu kuwa Bwana ameshaanza kufanya muujiza katika hilo eneo lako la maishaa..Hivyo zingatia sasa kudhihirisha Imani yako kwa matendo kwa kujiepusha na mambo yote maovu yasiyompendeza Mungu, tangu leo, ishi maisha ya kujikana nafsi, mfuate Bwana Yesu. Hizi ni siku za mwisho, zidisha ukaribu wako kwa Bwana.

Bwana akubariki.

Amen.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

UKIOKOKA,HIZI FIKRA ZIKIJA NDANI YAKO, ZIKATAE.

Mti wa MLOZI alioonyeshwa nabii Yeremia 1:12 tafsiri yake ni nini?

Sadaka ya kinywaji ilikuwaje? Na inawakilisha nini?

USIWE MSIKIAJI TU! BALI MTENDAJI.

Hazina za gizani ni zipi? (Isaya 45:3).

AKAJIFUNGA VAZI LAKE, AKAJITUPA BAHARINI.

Nini maana ya “wazimu” katika biblia?

Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Victoria Jonathan
Victoria Jonathan
7 months ago

Bwana Yesu asifiwe. Nashukuru kwa mafundisho haya mazuri. Mtumishi naomba kuuliza swali; ni vibaya kutumia chumvi katika agano jipya?