Paulo alikuwa anamaanisha nini kusema “Mnatenda vema kuvumiliana naye” (2Wakorintho 11:4).

Paulo alikuwa anamaanisha nini kusema “Mnatenda vema kuvumiliana naye” (2Wakorintho 11:4).

Jibu: Tusome,

2Wakorintho 11:4 “Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, MNATENDA VEMA KUVUMILIANA NAYE!”

Ukiisoma sentensi hiyo kwa haraka ni rahisi kutafsiri kuwa Paulo anawafundisha watu kuwavumilia watu wanaohubiri injili nyingine, au kumhubiri Yesu Mwingine..Lakini sivyo, bali ni kinyume chake!.. alikuwa anawashangaa kwanini wanawavumilia hao wanaohubiri injili nyingine!.

Sasa sentensi hiyo ili ieleweke vizuri tunaweza kuiweka hivi .. “Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, MNAVUMILIANA NAYE VIZURI SANA”..

Hivyo Neno “Kutenda vema” hapo jinsi lilivyotumika, limemaanisha “kufanya vizuri”..kwamfano badala ya kusema “mtu yule anaimba vizuri” pia ni sawa na kusema “mtu yule anatenda vema kuimba”.

Paulo alikuwa anawaonya hawa Wakorintho, kwa kuyavumilia mafundisho ya kipepo, na injili za kuzimu.. Kwamba hawapaswi kuyavumilia wala kuchukuliana nayo..

Na maonyo hayo yanatuhusu pia sisi kwamba hatupaswi kuwavumilia watu wanohubiri Injili nyingine, au yesu mwingine au roho mwingine.

Na hatuwavumilii kwa namna gani?

  • KWA KUTOENDELEA KUDUMU KATIKA KUISIKILIZA INJILI ZAO.

Tunapoijua kweli, hatuna budi kuachana na yale mafundisho ya uongo ya manabii wa uongo na Kama tumeshajua kuwa ULEVI ni dhambi, hatuna haja ya kuendelea kusikiliza mafundisho au kuwasikiliza wahubiri wanaofundisha kuwa Ulevi si dhambi!!…kwasababu injili yao ni injili nyingine, ambayo si ya YESU WA NAZARETI.

Tunapojua kuwa IBADA ZA SANAMU ni dhambi!, hatuna budi kuachana na mafundisho ya kipagani ya ibada za sanamu, yanaohubiriwa na wachungaji wa uongo, na maaskofu wa uongo, na vile vile kuacha kufuatilia mafundisho yao kwasababu wanahubiri roho nyingine tofauti na Roho Mtakatifu.

  • KWA KUWAONYA NA KUZIDHIHIRISHA KAZI ZAO HADHARANI KUWA NI MBOVU.

Tunapogundua kuwa yupo mtu au watu, wanafundisha kinyume na kweli, tena kwa makusudi, na huku wanajua kabisa wanachokifanya sio sawa..hapo hatupaswi kuivumilia injili yao.. badala yake kuupinga uharibifu wao hadharani..ili kusudi wasiendelee kuwapotosha wengine wasiojua..

Wagalatia 1:6 “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia INJILI YA NAMNA NYINGINE.

7 WALA SI NYINGINE; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka KUIGEUZA INJILI YA KRISTO

8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo TULIYOWAHUBIRI, NA ALAANIWE.

9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote ISIPOKUWA HIYO MLIYOIPOKEA, NA ALAANIWE”.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

FANYA KAMA UONAVYO VEMA.

NI YESU YUPI UMEMPOKEA?, NI ROHO IPI UMEIPOKEA? NA INJILI IPI UMEIPOKEA?

Je Mungu ana njia ngapi za kuzungumza?

NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?

Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments