Na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa?. Ni mwamba gani huo?(Mathayo 16:18)

Na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa?. Ni mwamba gani huo?(Mathayo 16:18)

Jibu: Tusome,

Mathayo 16:16 “Simoni Petro akajibu akasema, WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.

17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, NA JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU; WALA MILANGO YA KUZIMU HAITALISHINDA

Kufuatia andiko hilo mwamba unaozungumziwa hapo ambao kanisa litajengwa juu yake sio Petro!!.. kanisa la Mungu halijawahi kujengwa juu ya mtu  wala kujengwa na mtu.

Bali Mwamba uliokuwa unazungumziwa hapo ni huo ufunuo Petro alioupokea wa YESU kuwa NI KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.

Juu ya ufunuo huo ndio kanisa lake litajengwa..Yesu Kristo ndio Msingi wa kanisa, YEYE NDIO MWAMBA IMARA  ambao kanisa litajengwa juu yake..na si juu ya mtu mwingine. Ndio maana waumini wa kanisa la Mungu wanajulikana kama Wakristo, sio waPetro…Kwasababu msingi sio Petro bali ni Kristo.

Ili tulithibitishe hilo vizuri, tusome mistari ifuatayo.

1 Wakorintho 3:10 “Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.

11 Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, YAANI YESU KRISTO”.

Umeona msingi huo ni nani??

Si mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO (MKUU WA UZIMA!!). Na ndio maana utaona mitume wote walimhubiri Yesu, ikiwemo Petro mwenyewe..(Na wala Petro hajawahi kusema popote kwamba yeye ndiye Mwamba).

Zaidi sana katika waraka wake kwa kinywa chake mwenyewe aliandika na kusema na kushuhudia kwamba Yesu ndiye, Mwamba na tena ndiye Jiwe kuu la pembeni.

Tusome,

1 Petro 2:3-8 “ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.

4 Mmwendee yeye, JIWE LILILO HAI, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.

5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.

6 Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.

7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,

Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na MWAMBA WA KUANGUSHA maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo”.

Huyo ni Petro, anayesema maneno hayo!..Sasa ingekuwa ndio ule mwamba bao kanisa litajengwa juu yake, si angejitaja wazi kabisa hapo kuwa yeye ndio huo mwamba!!!..lakini tunaona anaushuhudia mwamba mwingine ambao ni YESU!.

Zaidi sana tafsiri ya jina Petro sio Mwamba bali ni “jiwe”..tena “jiwe dogo, la kurusha”..

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba Yesu ndio Mwamba, na si Petro, au kuhani yeyote au mwalimu yeyote, au mchungaji yeyote, au padri yeyote, au papa yeyote au kasisi yeyote au mtu mwingine yeyote.

Mtu anayechukua nafasi hiyo ya Kristo na kusema yeye ni mwamba basi huyo ni mpinga kristo.

Lakini swali ni je!..umemwamini Yesu, na kutubu na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu?.

Kama bado ni vizuri ukafanya hivyo sasa, kabla nyakati za hatari hazijafika.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Ngome ni nini?  Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?

Gumegume ni nini? (Isaya 50:7)

Ni kweli hakuna mtu aliyewahi kuuona uso wa Mungu Zaidi ya Bwana Yesu?

JIWE LILILO HAI.

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Very powerful msg

Isaya Moshi
Isaya Moshi
1 year ago

Asante Kwa neno zuri , ubarikiwe sana

Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
2 years ago

Mwalimu kwa kweli nakosa hata la kusema,yani najihisi kukuelewa sana.Mafundisho unapofundisha ni kama vile unaniamsha kutoka kwenye usingizi wa ujinga afu maluweluwe yote yanatoweka kisha nakuwa macho katika KWELI.Barikiwa sana mwalimu.