JIWE LILILO HAI.

JIWE LILILO HAI.

Kwa kawaida Mawe, hayaishi.. ni vitu visivyo na uhai.. Kwasababu tabia mojawapo ya viumbe hai ni kukua, na nyingine ni kuzaliana na kuwa na hisia (yaani muitikio kwa mazingira ya nje).

Lakini Mawe tunayoyaona yote hayazai.. Hakuna jiwe linaloweza kuzaa..wala mawe hayakui, yapo vilevile siku zote..kwahiyo ni vitu visivyo hai.

Lakini biblia inasema lipo Jiwe moja la kipekee ambalo LINAISHI!!.. Hilo ni tofauti na mawe mengine,  mawe mengine ni magumu lakini hayaishi, ni mazuri kimwonekano lakini hayana uhai, ni ya gharama sana, lakini hayana uzima, hayakui, hayazai, hayaongezeki. Lakini lipo jiwe moja la gharama sana, na gumu sana, na lililo hai, linalokua na kuzaa..na jiwe hilo si jingine zaidi ya YESU KRISTO.

1Petro 2:4 “Mmwendee yeye, JIWE LILILO HAI, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima”.

Jiwe hili lilianza dogo sana, katika tumbo la Bikira Mariamu.. likazidi kukua katika uweza na nguvu.  Mpaka kufikia miaka 33 na nusu, liliongezeka nguvu, na thamani baada ya kushinda mauti, na sasahivi limeunuliwa juu sana, na siku moja litarushwa kutoka juu mpaka chini duniani na kuvunja vunja falme zote za ulimwengu, na litakuwa Mlima mkubwa, na litazaa milima mingine mingi, ambayo ndiyo sisi.

Danieli 2:34 “Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande……………………

36 Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme.

44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni ATAUSIMAMISHA UFALME AMBAO HAUTAANGAMIZWA MILELE, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali UTAVUNJA FALME HIZI ZOTE VIPANDE VIPANDE NA KUZIHARIBU, NAO UTASIMAMA MILELE NA MILELE.

45 NA KAMA VILE ULIVYOONA YA KUWA JIWE LILICHONGWA MLIMANI bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.”.

Jiwe hilo lililo hai ni YESU KRISTO. Linaishi, ndio maana unaona hapo katika maandiko, linaonekana kukua na kuwa mlima mkubwa, na hatimaye kuzaa mawe mengine na hayo mawe kuwa milima mingine mingi… na milima hiyo ndio sisi tuliomwamini, ambao tutakaokuja kutawala pamoja naye katika utawala wa miaka elfu.

1Petro 2:5 “NINYI NANYI, KAMA MAWE YALIYO HAI, MMEJENGWA MWE NYUMBA YA ROHO, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo”

Lakini wote ambao hawatamwamini Yesu katika maisha haya, Jiwe hili litakuja kuwaponda ponda..

1Petro 2:6 “Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.

7 BASI, HESHIMA HII NI KWENU NINYI MNAOAMINI. BALI KWAO WASIOAMINI, JIWE WALILOLIKATAA WAASHI, LIMEKUWA JIWE KUU LA PEMBENI.

8 TENA, JIWE LA KUJIKWAZA MGUU, NA MWAMBA WA KUANGUSHA, KWA MAANA HUJIKWAZA KWA NENO LILE,WASILIAMINI,NAO WALIWEKWA KUSUDI WAPATE HAYO”.

Litumainie hili jiwe lililo hai, mengine yote yana thamani lakini hayana uzima, Wafalme wa dunia wana thamani lakini hawana uhai, ni mawe yasiyoishi, Wakuu na wenye mamlaka ni mawe magumu kama almasi yenye thamani nyingi lakini hayana uhai…(kwasababu almasi ijapokuwa ni ya thamani kuliko mawe yote, lakini si kitu kinachoishi). Lakini Yesu ni Jiwe lililo hai, tena lenye thamani, na linaloharibu. Hilo ndilo la kulitumainia na kulitafuta.

Kama umelipata hilo, basi wewe nawe ni jiwe kama yeye Bwana Yesu alivyo, katika ulimwengu wa roho unavunja vunja  na kuponda ponda ufalme wa giza na kuharibu na kuteka nyara kila kitu. Na unao uwezo wa kuzaa mawe mengine, kwasababu nawe ni jiwe lililo hai.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Group la whatsapp Jiunge na Group letu ya whatsapp, la masomo ya kila siku kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika..

CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

Je Lutu alikwenda kuwahukumu watu wa Sodoma na Gomora? Kulingana na Mwanzo 19:9?

JIWE LA KUSAGIA

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Antelm Barack
Antelm Barack
2 years ago

Habari hizi ni njema sana kwa kweli.. Mungu azidi kuwainua watumishi wa Bwana

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Uko sawa mtumishi