Lipo jiwe Yakobo aliloliweka chini ya kichwa chake kabla ya kulala na baada ya kuamka alilisimamisha likanyanyuka.
Jiwe hili lilibeba ufunuo wa YESU KRISTO, ambao napenda tuutazame leo.
Kipindi Yakobo anamkimbia Esau ndugu yake, alifika mahali fulani ambapo ni pa kawaida, lakini baadaye pakawa si pa kawaida.
Kabla ya kulala, alitwaa jiwe na kuliweka chini ya kichwa chake kama mto, huenda aliliona tu ni kama jiwe la kawaida lakini baada ya kuamka aligundua limebeba ufunuo mkubwa.
Mwanzo 28:10 “Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. 11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. 12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. 13 Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako…………… 16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. 17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni. 18 Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. 19 Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. 20 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi”.
Mwanzo 28:10 “Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani.
11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale.
12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.
13 Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako……………
16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.
17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.
18 Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.
19 Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.
20 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi”.
Unaona?..baada ya Yakobo kuamka usingizini aliona jiwe lile halipaswi tena kuwa kama Mto wa kulalia bali nguzo inayosimama.
Je na wewe jiwe hii umelisimamisha au unaendelea kulilalia tu.
Na Jiwe hilo si mwingine zaidi ya Bwana YESU.
1 Petro 2:4 “Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima”.
Jiwe hilo lililofungua ufahamu wa Yakobo na akamwona Mungu na Malaika wake usiku ule na hilo akalifanya kuwa NGUZO.
Akalifanya kuwa Nguzo ya nadhiri zake, akalifanya kuwa nguzo za hekalu la Mungu.
Je na wewe jiwe hili (YESU) umelisimamisha katika maisha yako au umelilaza?.
Kama jiwe hili limelala chini yako basi matokeo yake kwa nje ni tufani na maangamizi ya ibilisi, lisimamishe kuanzia leo.
Mitume wa Bwana YESU walijua umuhimu wa kulisimamisha Jiwe Bwana YESU katika ile tufani ilipotokea baharini..
Marko 4:35 “Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo. 35 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye. 37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. 38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? 39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu”
Marko 4:35 “Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo.
35 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.
37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.
38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?
39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu”
Ukiwa Yesu uliye naye ni yule wa kidini tu, yule wa kurithi kwa wazazi….basi fahamu kuwa ni Jiwe lililolala chini yako.
Ukiwa ukristo wako ni ule wa mazoea tu, usio na hofu na Mungu, basi jua kuwa unalo jiwe lililo lala.
Ikiwa ukristo wako ni ule wa ndoto na maono tu, na hutaki kujifunza Neno la Mungu basi fahamu ya kuwa jiwe lako limelala.
Yakobo baada ya kuona maono yale hakuendelea kulifanya lile jiwe kuwa Mto badala yake alilisimamisha mbele yake, lakini utaona wakristo wa leo baada ya kuona maono mawili matatu ya kiMungu, basi hata Neno la Mungu halisomwi tena, wanabaki tu kuendelea kuishi kwa ndoto na maono, jambo ambalo ni hatari sana.
Lisimamishe jiwe, lisimamishe jiwe.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
Print this post