Zipo aina tatu za Utakatifu, na leo tutaangalia moja baada ya nyingine, na tutajua ni upi unaotufaa sisi.
Aina hizi za utakatifu ni kama ifuatavyo.
1.UTAKATIFU WA MWILINI
2. UTAKATIFU WA ROHONI
3. UTAKATIFU WA MWILINI NA ROHONI.
1.UTAKATIFU WA MWILINI.
Ni ile hali ya kuuweka mwili katika viwango vya kumpendeza MUNGU, ikiwemo kuvaa vizuri kiasi kwamba mtu akikutazama basi anaona ushuhuda wa Kristo katika uvaaji wako na mwonekano wako.
Vile vile utakatifu wa mwilini unahusisha, kujilinda na matendo yote ya mwili yanayotajwa katika Wagalatia 5:19-20…ikiwemo uasherati, ulevi, kujichua, kujichubua na mengineyo.
Mtu anaweza kuwa na utakatifu huu wa mwilini na ule wa rohoni akaukosa. Anaweza kuwa na mwonekano mzuri sana wenye ushuhuda lakini akaukosa ule wa rohoni.
Sasa utakatifu wa rohoni ni upi?.
2. UTAKATIFU WA ROHONI.
Utakatifu wa rohoni ni ule unaohusisha, matendo yote ya rohoni yanayompendeza MUNGU.
Ikiwemo kuomba, kutoa sadaka (Mathayo 6:4), kumwabudu Mungu katika roho, kujifunza na kutafakari Neno la Mungu, vile vile upendo, uvumilivu, utu wema, kiasi.
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.
Mtu akiwa na matunda hayo basi kibiblia ni mtakatifu rohoni.
Sasa ni rahisi sana mtu kuwa mtakatifu mwilini na asiwe mtakatifu rohoni, lakini ni jambo la Nadra sana kukuta mtu mtakatifu rohoni na mwilini akawa si mtakatifu.
Watu wengi wenye utakatifu rohoni halafu nje mwonekano wao hauna ushuhuda, wengi wao ni watu wanaovaa viatu vinavyowabana, huwa wanajua kabisa kuwa mionekano yao haina ushuhuda kwasababu ya Roho Mtakatifu aliye ndani yao, isipokuwa kuna mazingira yanayowafanya wabaki katika hiyo hali.
Na mazingira hayo yamegawanyika katika sehemu mbili.
Sehemu ya kwanza: Viongozi wao wa kiroho wanawachanganya.
Wengi wanaotamani kubadili mionekano yao ya nje, wanapowatazama viongozi wao wa kiroho kuwa ndio watu wanaoongoza katika kuvaa ovyo, wanachanganyikiwa na kubaki kufikiri kwamba wao wana makosa na viongozi wao wapo sawa, hivyo wanabaki katika hali ya ubumbuazi wa kiroho, wanashindwa kujua nini cha kufanya na wanaishia kupokea yale viongozi wao wanayoyasema na kuyatenda.
Dada/kaka kama upo katika hili kundi, basi sikia sauti ya Roho Mtakatifu leo. KAMILISHA UTAKATIFU WAKO WA MWILINI, ni kweli matendo yako ya rohoni ni mema na mazuri, sasa umebakisha hilo moja tu la Rohoni, ondoa hayo mapambo ya kidunia mwilini mwako, ondoa hizo hereni, ondoa hiyo mikufu, ondoa hizo bangili, ondoa hizo rangi usoni, ondoa huo mtindo wa nywele na uvaaji usio na ushuhuda, na utapanda viwango vingine vya kiroho.
Usichanganywe na miujiza inayofanywa na viongozi wako wa kiroho, hata kama ndiye aliyekuleta kwa Kristo, basi asikuogopeshe na kukufunga usilifuate Neno la Mungu.
Hata kama ana hubiri vizuri, usiogope, hata kama aliwahi kukuombea ukapona, bado uasiogope..Neno la MUNGU ni nyundo na upanga ukatao kuwili, na Bwana alisema wengi watakuja siku ile na kusema walitoa pepo na kufanya miujiza kwa jina lake lakini atawafukuza.
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”
Sehemu ya pili: Wazazi na Ndugu.
Wazazi na ndugu ni sehemu kubwa na kuuzia utakatifu wa mwilini kwa mtu, kwani wengi wanapoona na kusikia ushauri wa ndugu, bali ule ushauri unaweza kuwa mzito sana zaidi hata ya mtu mwingine yeyote.
Utakatifu wa mwilini na rohoni ni ile hali ambapo mtu anakuwa na ushuhuda wa ndani roho yake na nje ya mwili wake. Na huu ndio utakatifu Mungu anaouhitaji kwetu.
1 Wakorintho 7:34 “….. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho….”
Utakatifu wa mwilini na rohoni ndio msingi wa sisi kumwona Mungu sawasawa na ile Waebrania 12:14.
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”.
Timiza utakatifu wako Mteule wa MUNGU..
2 Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”
VIWANGO VYA UTAKATIFU.
Katika kuwa watakatifu wa mwilini na rohoni ni lazima viwango vyetu viwe juu zaidi ya watu wasio wa Kristo.
Mathayo 5:20 “Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”.
Maana yake ni kwamba kama kumcha Mungu basi ni lazima tuwazidi wa imani nyingine, kama kuvaa kwa staha ni lazima tuwazidi watu wengine wote wasio wa Imani n.k.
Bwana YESU atusaidie sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
Print this post
Blessings