JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.

JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.

JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI
Wingu la Mashahidi
JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.
Loading
/

Jina kuu la Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu, Simba wa kabila la Yuda, na Mkuu wa wafalme wa dunia, Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze biblia, neno la Mungu wetu, lililo mwanga wa njia yetu, na taa iongozayo miguu yetu.

Upo wakati wakati ambao tutahitaji Bwana atuguse mara ya pili, lakini ni vizuri kujua kanuni ya kupokea Uponyaji pindi tunapomsihi Bwana atuguse tena…

Hebu tusome kisa kimoja katika biblia na kisha tutafakari na tujifunze, kanuni ya kupokea uponyaji mkamilifu.

Tusome Marko 8:22-26, (Zingatia maneno yaliyoanishwa kwa herufi kubwa).

Marko 8:22 “Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse.

23 Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, AKAMTEMEA MATE YA MACHO, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?

24 AKATAZAMA JUU, AKASEMA, NAONA WATU KAMA MITI, INAKWENDA.

25 Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, NAYE AKATAZAMA SANA; akawa mzima, akaona vyote waziwazi.

26 Akampeleka nyumbani kwake, akisema, Hata kijijini usiingie”.

Katika kisa hichi hebu tujiulize swali lifuatalo, kisha tuendelee mbele..

Je inawezekana mtu atazame juu halafu aone watu?, tena watu wenyewe wanatembea? Na tena wanatembea kwa kasi kama miti?… Nilitegemea hata angesema anaona “ndege wanaruka, wanakimbia kama miti”!! Lakini yeye anasema anaona watu!!……Bila shaka ulishawahi kusafiri na basi linalokwenda kasi, na njiani ukaona namna miti inavyoonekana kama inarudi nyuma kwa kasi sana…Ndivyo alivyoona huyu mtu alipotazama juu..aliona watu!..

Kwa kawaida, huu sio uponyaji!!.. Huyu mtu hakuwa amepata uponyaji wowote, bali alikuwa katika hatua za mwanzo za kupokea uponyaji..ni kama tu TV iliyowashwa ambayo bado haijakamata mawimbi!!..inakuwa inaonyesha tu chenga chenga…

Lakini tunaona tabia ya kipekee ya huyu kipofu baada ya kuguswa na Bwana mara ya pili.

Utaona huyu kipofu mara ya kwanza alipoguswa, alitazama juu hakutumia muda mrefu kutazama, badala yake, kwa haraka haraka akakimbilia kumjibu Bwana kwa kusema “anaona watu kama miti”….. lakini baada ya kuguswa na Bwana mara ya pili, ni kama alijifunza kitu kuwa hana budi kutokuwa na haraka ya mambo…utaona alitulia na KUTAZAMA SANA!! (pengine alitumia dakika kadhaa kutazama juu), akawa bado anaona ile ile miti, lakini hakuacha kutazama…..

Na alipozidi KUTAZAMA SANA, pengine akaanza kuona  ile miti inafutika kidogo kidogo, akaanza kuona anga linakuwa jeupe na kidogo kidogo akaanza kuona mawingu, na pengine akaanza kuona ndege wanaruka, na alipotazama mbele akamwona Bwana Yesu, ndipo akasema sasa ninaona!!! Haleluya.

Na sisi hatuna budi KUTAZAMA SANA!!..Tusiishie kutazama kidogo tu! tusiishie kuzungumza, wala kunung’unika, wala kukosoa, wala kutoa hitimisho, pale tunapoona uponyaji haujakamilika….bali turuhusu uponyaji wa Bwana ufanye kazi!… Tuwe na Subira huku tukiliamini Neno lake.

Kutazama sana, ni kudumu katika kumwamini Mungu, hata kama unaona lile tatizo bado halijatatuka… wewe endelea kumwamini Bwana na kusubiri, bila kutoa uso wako juu mpaka muujiza wako utakapokamilika..

Pengine ulimwomba Bwana kuhusu hali unayopitia ya kiroho au kimwili,  lakini uliishia kuona chenga chenga katika huo ugonjwa, au hilo tatizo..lakini sasa umeijua kanuni..Msii Bwana akuguse tena kwa mara nyingine, lakini safari hii USIRUHUSU IMANI YAKO IPUNGUE, WALA USIUKIRI UGONJWA.…Utaona muujiza wa ajabu, ukitendeka!!.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!

JINSI YA KUSOMA BIBLIA.

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?

JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.

Mwerezi ni nini?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments