NI WAPI UTAKUTANA NA MALAIKA WA BWANA?

NI WAPI UTAKUTANA NA MALAIKA WA BWANA?

Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo aliye Bwana na mwokozi wetu. Utukufu na uweza ni vyake milele na milele. AMEN.

Leo tuone ni nini Bwana anasema nasi tena nyuma ya  tukio la Hajiri kijazi wa Sarai alipomtoroka bibi yake..

Kama tuonavyo katika maandiko mateso yalipozidi, alikimbilia jangwani..lakini akiwa kule jangwani, alilia sana  Bwana, amsaidie kwasababu kama tujuavyo jangwani ni mahali ambapo hakuna mahitaji yoyote ya kijamii..ukizingatia na yeye alikuwa mjamzito, hawezi kujihudumia kwa lolote.

Lakini upo uamuzi ambao hajiri aliuchukua ambao kama asingeuchukua kwa wakati ule, haijalishi angemlilia Mungu namna gani asingepata msaada wowote, wala asingeisikia sauti ya Mungu, ilipokuwa inamtafuta kusema naye kule jamgwani..

Na uamuzi wenyewe ulikuwa ni ule wa kukimbilia kwenye CHEMCHEMI YA MAJI. 

Mwanzo 16:6-12

[6]Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.

[7]MALAIKA WA BWANA AKAMWONA KWENYE CHEMCHEMI YA MAJI katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri.

[8]Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.

[9]Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake.

[10]Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.

[11]Malaika wa BWANA akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana BWANA amesikia kilio cha mateso yako.

[12]Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.

Ni vizuri tukaona kitu hapo…kumbe malaika alikuwa anamtafuta hamwoni…lakini alipofika katika ile chemchemi ya maji ndipo akamwona Hajiri kisha akazungumza naye na kumpa maagizo.

Hata sasa, watu wengi wanamlilia Mungu kweli awasaidie, wapo katika majangwa ya namna mbalimbali, na Mungu kweli anawasikia, lakini pale ambapo malaika wa Bwana wanatumwa kuwapa majibu yao hawawaoni, kwasababu hawapo katika chemchemi ya maji…wapo kwenginepo.

Na maandiko yanasema Yesu ndiye chemchemi ya maji ya uzima..

Yohana 4:13-14

[13]Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;

[14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.

Ni mara ngapi tunakuwa wepesi wa kumlilia Mungu atusaidie, lakini kumuishi Kristo katika maisha yetu inakuwa ngumu.

Hatuna Muda wa kusoma Neno, hatuna muda wa kuomba, hatuna muda wa kufanya ibada, na kushuhudia habari njema, hatuna muda wa kudumu katika chemchemi ya maji ya uzima..lakini wakati huo huo tunalia Bwana tusaidie! Bwana tutetee! Bwana tubariki!, Bwana tuponye..tukiwa katika biashara zetu, katika kijiwe vyetu, katika mitandao ya kijamii tunachat, katika tv, tunaangalia movie, na tamthilia, katika party na starehe, tunakesha kila mwisho wa wiki, lakini kukesha kanisa mara moja kwa wiki hatuwezi. 

Tusahau kumwona malaika wa Bwana, akileta majibu ya maombi yetu..kwasababu macho yao hayaoni mahali pengine zaidi ya penye chemchemi ya maji ya uzima. Ndivyo walivyoumbwa, Kamwe malaika hawezi kukufuata kwenye kijiwe chako, au kwenye mihangaiko yako, kukupa majibu ya maombi yako. Atakuona tu, pindi uwapo uweponi mwa Kristo, hilo tu!…hawana shughuli na mambo ya ulimwengu huu.

Tumaanishe sasa kumrudia Bwana, kwa mioyo yetu yote..tujifunze kudumu uwepo mwa Kristo, Kuna faida nyingi. Ondoa uvivu wako katika masuala ya wokovu wa Roho yako. Ikiwa utaamka kila siku alafajiri kwenda kazini, kwanini uone uvivu kuhudhuria mikesha na ibada?

Bwana atusaidie…

Je umeokoka? Je! Unatambua ya kuwa tunaishi katika kizazi ambacho kinaweza kushuhudia tukio la kurudi kwa pili kwa Kristo duniani? Kwasababu dalili zote zimeshatimia. Na kanisa tunaloishi ndio la mwisho lijulikanalo kama Laodikia?

Umejiwekaje tayari, ikiwa upo tayari kumkabidhi Kristo maisha yako. Na unahitaji mwongozo huo, au utapenda kupata ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi 

+255693036618/ +254789001312

Bwana akubariki shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

WEWE U MUNGU UONAYE.

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.

NUNUA MAJI YA UZIMA.

Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)

KISIMA CHA MAJI YA UZIMA NI KILE KILE CHA ZAMANI.

KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Devis Julius administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Athanas Mabala
Athanas Mabala
5 months ago

Namba yangu ya Wasap ni 0658162774 niunganishe jina ni Athanas Mabala