Mofa ni nini? na inafunua nini kiroho?(1Samweli 28:24).

Mofa ni nini? na inafunua nini kiroho?(1Samweli 28:24).

Jibu: Tusome,

1Samweli 28:24 “Naye yule mwanamke alikuwa na ndama aliyenona nyumbani; akafanya haraka kumchinja; akatwaa na unga, akaukanda, akafanya MKATE WA MOFA kwa unga huo”.

Mkate wa Mofa ni mkate uliotengenezwa bila kuwekwa “Hamira”.  Hamira kwa lugha ya kibiblia inaitwa “Chachu” kazi yake ni kuchachusha au kuumua unga uliokandwa, kama biblia inavyosema katika..

Mathayo 13:33  “Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia”

Na tena biblia inasema.. “Chachu kidogo huchachua donge zima (Wagalatia 5:9)”

Kwahiyo Mikate ya Mofa ni mikate iliyotengenezwa bila kuwekwa hamira, mfano wa chapati. Kwa  wayahudi baada ya sikukuu ya pasaka kupita, sikukuu iliyokuwa inafuata ilikuwa ni sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu (yaani Mofa),  Ndani ya siku 7 Wana wa Israeli waliambiwa wale mikate ya Mofa, na mtu yeyote ambaye alionekana anakula mikate mingine zaidi ya hiyo, aliuawa kulingana na sheria ya torati.

Na ndani ya kipindi hicho pia mtu yeyote akionekana na Viungo vya Hamira ndani kwake, hata kama atakuwa hajaviweka kwenye unga, kitendo tu cha kuiweka ndani ilikuwa pia adhabu yake ni kifo

Kutoka 12: 15 “Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli”.

Soma pia Walawi 23:5-6.

Lakini je! Mkate wa Mofa unawakilisha nini kiroho?

Mkate wa Mofa unawakilisha Mwili wa Bwana wetu Yesu Kristo,  Na ndio uliotumika na wakristo wa kanisa la kwanza katika kushiriki Meza ya Bwana, na ndio unapaswa utumike hata sasa katika kushiriki meza ya Bwana, na si biskuti au maandazi!.

Luka 22:19  “Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu”.

Sasa kwanini Bwana Yesu achague mkate wa Mofa, kuwakilisha Mwili wake?

Ni kwasababu Mwili wa Bwana Yesu haubadiliki wala hauwezi kubadilishwa maumbile. Hamira/chachu kazi yake ni kubadilisha maumbile ya vitu, ndio maana inapowekwa kwenye unga uliokandwa baada ya muda Fulani utakuta ule unga umeumuka!

  Sasa mwili wa Kristo hauumushwi, wala hauwezi kubadilishwa kimaumbile..bali siku zote ni ule ule!(Waebrania 13:8).. Maana yake kanuni za Bwana Yesu ni zile zile, hazibadilishwi na mazingira wala na mtu, Neno lake ni lile lile jana na leo na hata milele.

Hatuwezi kutia hamira Neno la Mungu, Neno la Mungu likisema ulevi ni dhambi!, hatuwezi kuliwekea hamira hapo na kusema ulevi sio dhambi!..likisema “mtu anapaswa avae mavazi ya kujisitiri” hatuwezi kulitia hamira kwa kusema “Mungu haangalii roho bali anaangalia mwili (1Timotheo 2:9)”

Na mambo mengine yote, biblia iliyoyataja ni lazima tuyazingatie yabaki kama yalivyo bila kuumuliwa na hamira za mafundisho ya uongo.

Bwana Yesu atusaidie katika hayo.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.

Je ni lazima kushiriki Meza ya Bwana?

Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zilikuwaje?

HII NDIO TABIA YA WATU WA KEILA, USIIGE

HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments