Historia ya wimbo wa tenzi – Ndio dhamana Yesu wangu

Historia ya wimbo wa tenzi – Ndio dhamana Yesu wangu

Historia ya wimbo wa tenzi – Ndio dhamana Yesu wangu. (Blessed assuarance)


Wimbo huu ulindikwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Fanny Crosby, Mwanamke huyu japo aliishi kwa miaka 95 akiwa kipofu,lakini hakuacha kuitumia neema Mungu aliyompa kutangaza injili kwa njia ya Nyimbo zenye muundo wa Tenzi za rohoni na nyinginezo, katika maisha yake alifanikiwa kuandika nyimbo zaidi ya 8000, Na hii nyimbo  “Ndio dhamana Yesu wangu” Ikiwa mojawapo, Nyingine inayojulikana sana mpaka leo ni “Usinipite mwokozi” yeye pia ndio aliyeiandika nyimbo hii alipokuwa amewatembelea wafungwa gerezani(angalia historia yake chini).

Phoebe Knapp

Phoebe Knapp

Sasa Siku moja  alipokuwa amemtembelea rafiki yake nyumbani kwake  aliyeitwa Phoebe Knapp, ambaye alikuwa ni mtunzi wa sauti za nyimbo, wakiwa  nyumbani kwake Phoebe alianza kupiga mdundo wake aliokuwa ameutunga, kisha baada ya muda alimuuliza Fanny, Je unaweza kuniambia mdundo huu ni wa nyimbo gani?

Ndipo Fanny akamwambia “Ndio dhamana Yesu wangu”. Basi hapo ndio pakawa mwanzo wa mdundo na utunzi wa wimbo huo (1873).

Ndio dhamana Yesu wangu.

Ndiyo dhamana, Yesu wangu;
Hunipa furaha za mbingu;
Mrithi wa wokovu wake,
Nimezawa kwa Roho wake.
 
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.
 
Kumsalimu moyo wangu,
Mara namwona raha yangu;
Aniletea malaika,
Wananilinda, tutaokoka.
 
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.
 
Sina kinyume; nashukuru,
Mchana kutwa huja kwangu;
Usiku kucha kuna nuru;
Mwokozi wangu; ndimi nuru.
 
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.
 
Hali na mali; anitwaa!
Mara namwona anifaa,
Nami nangonja kwa subira;
Akiniita, nije mara.
 
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.

*****

Uimbapo wimbo huu  kumbuka ni kipofu ndiye aliyeuandika, nawe pia unaposema “Ndio dhamana Yesu wangu” Basi awe kweli  wokovu wako. Mpende yeye bila unafki na kumtumikia kwasababu ndiye aliyekufa kwa ajili yako.

Je! Umeokoka? Unajua kuwa Unyakuo upo karibu sana, kwasababu tunaishi katika kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia? Na kwamba hatutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hili? Siku hizi zimekwisha, Hivyo kama upo tayari kumpa Yesu maisha yako leo ili wimbo huu uwe na maana kweli kwako. Basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye  namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

USINIPITE MWOKOZI Lyrics

YOTE NAMTOLEA YESU_Tenzi za Rohoni.

BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics

CHA KUTUMAINI SINA lyrics

KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

MPINGA-KRISTO

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

UFUNUO: Mlango wa 1

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments