CHA KUTUMAINI SINA, Swahili Lyrics. (My hope is built on nothing less)
Tenzi hii iliandikwa na mchungaji wa kanisa la kipatisti, aliyeitwa Edward Mote, raia wa nchi ya uingereza, mnamo mwaka 1834, Edward Mote alifanikiwa pia kuandika tenzi nyingine nyingi Zaidi ya 100, lakini iliyopata umaarufu mkubwa ni hii ijulikanayo kama “Cha Kutumaini sina”.
Tenzi hii aliibuni akirejea ule mfano alioutoa Bwana Yesu wa mjenzi mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba imara, Na yule mpumbavu ambaye aliijenga nyumba yake https://www.high-endrolex.com/2juu ya mchanga (Mathayo 7:24-27), Na kuonyesha ni jinsi gani mtu anapaswa aishi kwa kwa kumtegemea Kristo aliye mwamba salama, na ulio imara.
1Wakorintho 10:4 “wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo”
Na ndio hapo akaundika wimbo huu;
Cha kutumaini sinaIla damu yake Bwana,Sina wema wa kutoshaDhambi zangu kuziosha;
Kwake Yesu nasimama,Ndiye mwamba; ni salamaNdiye mwamba ni salama
Njia yangu iwe ndefuYeye hunipa wokovu;Mawimbi yakinipigaNguvu zake ndiyo nanga.
Damu yake na sadakaNategemea daima,Yote chini yakiisha,Mwokozi atanitosha.
Nikiitwa hukumuni,Rohoni nina amani;Nikivikwa haki yakeSina hofu mbele zake.
*****
Amen hata mimi na wewe, tukiwa ndani ya Kristo, tupo salama wakati wote, lakini tukimkosa yeye ndani yetu, basi hata kuimba kwetu ni bure, tutakuwa tu sawa na yule mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga..
Hivyo ukiwa unahitaji kuokoka ili Yesu leo awe kweli Mwamba ulio salama, basi fungua hapa kwa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
MWAMBA WENYE IMARA
MWAMBA WETU.
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
https://wingulamashahidi.org/2018/06/27/2-swali-kwanini-mtu-atoe-pepo-aombee-wagonjwa-wapone-asikie-sauti-ya-mungu-ikimwambia-hiki-na-kile-kuhusu-watu-na-yeye-mwenyewe-kufunua-siri-za-mioyo-yao-aone-maono-na-kutembea-na-malaika-katika/
Rudi Nyumbani:
Print this post
Yes send me bible lessons. May Lord bless you.
Habari zenu Mbarikiwe sana na Bwana nimependa na naomba mnitumie historia ya watunzi wa nyimbo zote za Tenzi za Rohoni
Nitafurahi sana mkianza leo
Bwana apewe sifa hongeren kwa kazi ya bwana natamani kuendelea kujifunza masomo yenu namba yangu ya whatsapp ni 0746870726
Habari watumishi wa mungu nimebarikiwa na huduma yenu, Nami natamani ,Niwe na pata neno la mungu kwa njia ya email au WhatsApp number +255 748 190 745
Tayari nimekuunga kwenye group la mafundisho, Bwana akubariki.