Kupwelewa maana yake nini? (Matendo 27:26).

Kupwelewa maana yake nini? (Matendo 27:26).

Tusome,

Matendo 27:25 “Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.

26 Lakini hatuna budi kupwelewa katika kisiwa kimoja”.

Kupwelewa maana yake ni “kusafiri katika kina kifupi”. Meli au Mashua inaposafiri katika maji yenye kina kifupi, maana yake Meli hiyo au boti hiyo “inapwelewa”.

Katika safari ya Paulo kuelekea Rumi chini ya kikosi cha maaskari, maandiko yanatuonyesha safari ile ilikuwa ni ya misuko-suko mingi baharini, kwasababu wale mahabaria hawakulisikiliza shauri la Paulo ambalo aliwashauri wasing’oe nanga lakini wenyewe hawakusikia hivyo. Mwishowe wakakutana na misuko suko mikuu baharini, mpaka wakakata tamaa ya kuokoka.

Matendo 27:10 “akawaambia, Wanaume, naona kwamba safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia.
11 Lakini yule akida akawasikiliza nahodha na mwenye merikebu zaidi ya yale aliyoyasema Paulo”.

Wakiwa katika hiyo misukosuko, Paulo alitokewa na Malaika na kuambiwa kuwa hakuna atakayekufa katika safari hiyo, kwani ni lazima Paulo afike salama Rumi ili akalishuhudie Neno la Mungu na kule nako. Na jambo lingine aliloambiwa na Malaika yule ni kwamba Merikebu itapwelewa (yaani itasafiri katika kina kifupi) kando kando ya kisiwa kimoja, mpaka watakapofika kwenye hicho kisiwa.

Na kweli ufunuo huo mahabaria waliuhakiki kwani muda mfupi tu walipoanza kupima kina cha maji waliona kinaanza kupungua kwa jinsi walivyokuwa anaendelea mbele.

Matendo 27:27 “Hata usiku wa kumi na nne ulipofika, tulipokuwa tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria, kama usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia nchi kavu.

28 Wakatupa bildi wakapata pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakapata pima kumi na tano”.

Ni nini tunachoweza kujifunza katika safari hiyo ya Paulo?

1.Mungu atakuwepo na sisi hata katikati ya majaribu
Paulo, alikuwa amefungwa lakini katika kufungwa kwake, bado Mungu alikuwa naye, akimwongoza katika mapito yake, utaona pia wakati akiwa gerezani bado Bwana alikuwa naye, na kila mahali Bwana alikuwa naye, vile vile na sisi tunapokuwa katika majaribu, ambayo tunajua kabisa ni Mungu kayaruhusu basi hatupaswi kuwa na woga wala kukata tamaa, kwasababu Mungu atakuwa Pamoja nasi, na zaidi sana yeye alisema “hawezi kutuacha tujaribiwe kupita tuwezavyo”

2. Wokovu wa Mungu ni hata kwa maadui zetu.

Tunapokuwa katikati ya majaribu ni muhimu kujua kuwa Mungu katuweka pale kwa wokovu wa wengine, Utaona Paulo kafungwa lakini Mungu anamwokoa yeye Pamoja na wale Mabaharia, na wafungwa na watesi wake, anawaokoa na Mauti vile vile na sisi Mungu anapotuweka mahali ni ili tuokoke na wale tulio nao, haijalishi ni maadui zetu au watesi wetu.

Matendo 27:22 “Sasa nawapeni shauri, iweni na moyo mkuu, kwa maana hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu atakayepotea, ila merikebu tu.

23 Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami,

24 akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.

25 Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.

26 Lakini hatuna budi kupwelewa katika kisiwa kimoja”.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Kaanani ni nchi gani kwasasa?

SI KWA MATENDO BALI NEEMA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments