NI UTUKUFU WA MUNGU KUFICHA JAMBO.

NI UTUKUFU WA MUNGU KUFICHA JAMBO.

Jina la Mkuu wa Uzima, Simba wa kabila la Yuda na Mungu katika mwili, YESU KRISTO libarikiwe!.

Kuna mambo ambayo ni muhimu kuyajua sisi kama watu wa Mungu ili tuende sawa na Mungu na pia ili tuwe na amani kama maandiko ya avyotuelekeza katika Ayubu 22:21.

Ayubu 22:21 “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia”

Ipo tabia moja ya Mungu ambayo ni muhimu kuijua ili tuishi kwa amani.

Na tabia yenyewe ni kuficha jambo/mambo. Biblia inasema hivyo katika…Mithali 25:2

Mithali 25:2 “Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo…”.

Mpaka mwenyewe anasema kuwa ni utukufu wake kuficha jambo…maana yake ni kuwa hiyo ni fahari yake yeye kufanya hivyo, hatuwezi kumbadilisha…

Kwahiyo ukiona ni kwanini kakuficha jambo fulani usilijue au usilipate kwa wakati fulani unaotoka wewe ni kwasababu ndivyo ilivyompendeza, anafanya hivyo kwa utukufu wake.. Na anafanya hivyo kwa watu wote wala hana upendeleo.. Wala usijione unayo mikosi unapojikuta hujui kitu au kinapokuwa ni kigumu kukipata.

Ukiona ni kwanini humwoni Mungu sasa kwa sura na mwonekano…ni kwasababu ni utukufu wake yeye kufanya hivyo..

Sasa ni nini anachotaka kwetu kutokana na hiyo tabia yake.

Anachotaka kutoka kwetu ni sisi TUTAFUTE KWA BIDII MPAKA TUPATE.

Luka 11:9 “Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa”

Ukitaka kumjua Mungu kwa viwango vya juu, haiwezi kuwa ni jambo la kulala na kuamka tu!..hapana! Inahitajika bidii sana katika kumtafuta..

Yeremia 29:12 “Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.

13 Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote”.

Vile vile ukitaka kuwa Mkamilifu si suala la kufumba na kufumbua tu, bali inahitajika bidii sana kuutafuta utakatifu na ukamilifu..kujazwa na Roho Mtakatifu ni hatua ya awali, baada ya hapo ni kuongeza juhudi kila siku, ndivyo maandiko yanavyosema katika Waebrania 12:14.

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”

Na mambo mengine yote ya KiMungu yaliyo mazuri yamefichwa na Mungu mwenyewe Na hayapatikani kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kwa kutafuta kwa bidii.

Na hatuwezi kumwuliza kwanini ayafiche hivyo!…ni fahari yake yeye na kwa utukufu wake

Tukitaka kuyavumbua basi ni sharti tuyatafute.

Dada/kaka anza leo kumtafuta Mungu kwa bidii sana, kwasababu anapatikana..adhimia kumtafuta kama Daudi…..

Zaburi 27:8 “Uliposema, Nitafuteni uso wangu, Moyo wangu umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta”

Tumia muda mwingi katika kutafuta kuliko kungoja, tumia muda mwingi katika kutafuta kuliko kunung’unika. Na Bwana atakufunulia.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TAFUTA KWA BIDII KUWA MTAKATIFU.

Kwanini Eliya alijulikana kama “Eliya Mtishbi”?

Sadaka ya Amani ilikuwaje?

Je Mungu ana njia ngapi za kuzungumza?

Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
7 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
keneth
keneth
8 months ago

mnaptikana wapi semina hikowapi barikiwasa

Antelm Barack
Antelm Barack
1 year ago

Mungu nitie nguvu za kukutafuta kwa bidii

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Asante tunashukuru

Anonymous
Anonymous
9 months ago
Reply to  Anonymous

Amen